DPP amfutia mashtaka ya ufisadi kigogo wa Maliasili | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

DPP amfutia mashtaka ya ufisadi kigogo wa Maliasili

Discussion in 'Habari na Hoja mchanganyiko' started by Ntemi Kazwile, Jun 17, 2010.

 1. Ntemi Kazwile

  Ntemi Kazwile JF-Expert Member

  #1
  Jun 17, 2010
  Joined: May 14, 2010
  Messages: 2,145
  Likes Received: 8
  Trophy Points: 135

  Na Hellen Mwango  17th June 2010
  [​IMG]
  Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa (Takukuru)  Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu, jijini Dar es Salaam, imemuachia huru Naibu Mkurugenzi wa Misitu na Nyuki, Dk. Ismail Kelly Alloo, baada ya Mkurugenzi wa Mashitaka (DPP) kusema kuwa hana nia ya kuendelea kumshitaki.
  Aidha, DPP amemfutia Mkurugenzi huyo mashitakiwa chini ya kifungu namba 91 cha Sheria ya Mwenendo wa Makosa ya Jinai (CPA), kinampa moja kwa moja mamlaka ya kumwondolea mashitaka mtuhumiwa.
  Bosi huyo wa Misitu na Nyuki, alifikishwa mahakamani hapo Novemba, mwaka jana ambapo alisomewa mashitaka mawili ikiwemo matumizi mabaya ya ofisi na kutoa taarifa za uongo kuhusu rushwa.
  Mashitaka hayo dhidi ya Alloo ambaye ni mtumishi wa Wizara ya Maliasili na Utalii, yalisomwa mbele ya Hakimu Mkazi Paul Kimicha.
  Mwendesha Mashitaka Kasuni Nkya kutoka Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa (Takukuru), aliyemsomea mashitaka hayo, alidai kuwa Mei 2, mwaka 2005, mshitakiwa anadaiwa kutenda kosa la matumizi mabaya ya ofisi kwa kuruhusu mauzo ya magogo kinyume cha sheria.
  Nkya alidai katika shitaka la pili kuwa Machi 17, mwaka 2005 katika ofisi za makao makuu ya Takukuru jijini Dar es Salaam, wakati wa uchunguzi wa matumizi mabaya ya rushwa, mshitakiwa alitoa taarifa za uongo kuhusu tangazo la mazao ya misitu mali ya Kampuni ya Aqeel Traders Ltd. Pamoja na kwamba upande wa Jamhuri ulidai upelelezi wa kesi hiyo ulikuwa umekamilika, kesi hiyo ilikuwa ikitajwa mahakamani hapo hadi alipofutiwa mashitaka na DPP.
  CHANZO: NIPASHE


  0 Maoni | Kuwa wa kwanza kutoa maoni
   
 2. Ntemi Kazwile

  Ntemi Kazwile JF-Expert Member

  #2
  Jun 17, 2010
  Joined: May 14, 2010
  Messages: 2,145
  Likes Received: 8
  Trophy Points: 135
  Hii ndiyo Tanzania yetu, wanaohusika na rushwa kubwa ndio hawana matatizo. Iba mihogo ukale uone. Utakaa rumande hata miaka minane ukisubiri uchunguzi kukamilika.
   
 3. K

  Kilembwe JF-Expert Member

  #3
  Jun 17, 2010
  Joined: Aug 19, 2009
  Messages: 1,132
  Likes Received: 45
  Trophy Points: 145
  Ukiona hivyo jua yeye alikuwa natumiwa tu, ni lazima alikuwa na backup ya mkubwa fulani....! Tanzania ni zaidi ya uijuavyo!
   
 4. Eng. SALUFU CA

  Eng. SALUFU CA Senior Member

  #4
  Jun 17, 2010
  Joined: May 12, 2010
  Messages: 146
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Hee!! Haya. Mola ndo atoaye hukumu ya haki lakini si wanadamu.
   
 5. N-handsome

  N-handsome JF-Expert Member

  #5
  Jun 17, 2010
  Joined: Jan 23, 2008
  Messages: 2,317
  Likes Received: 128
  Trophy Points: 160
  Hawaishi milele kama wao watalindana watoto wao na wajukuu watalipa tu
   
Loading...