DP World imeboresha nini kwenye bandari yetu ya Dar es Salaam?

Tajiri wa kinyankole

JF-Expert Member
Joined
Jun 12, 2019
Posts
1,975
Reaction score
4,908
Kampuni hii ilitangazwa kwa mbwembwe nyingi sana bungeni na kwenye media wa kwanza kuisfia kampuni hii alikuwa Musukuma, wakafuata Maulid Kitenge na wenzake pamoja na Prof. Makame Mbarawa

Sasa najiuliza nini kimeboreshwa katika bandari hiyo au DP World ni kiini macho cha wawekezaji wanaojichotea fedha za umma kwa mgongo wa DP World

Ile mitambo aliyosema msukuma iko wapi.

Pia soma > Nachojiuliza mkopo wa billion 864 nani analipa kama DP World wamepewa bandari ya Dar?
 
Ile mitambo aliyosema msukuma iko wapi
Nafikiri wale Watu wa-Tanzania wenzetu waliounga mkono na kuipigia chapuo ujio wa Kampuni hii wanapaswa wajitokeze hadharani Sasa ili wawaeleze wa-Tanzania kwa uwazi kabisa bila unafiki juu ya maboresho yaliyofanywa na DPW, faida, na hasara zinazopatokana baada ya Bandari zetu kugawiwa kwa hawa Waarabu wa DPW.

Tuanze kuwataja kwa Majina yao wale Watu wote kabisa ambao walishiriki kindakindaki katika kuunga mkono au kuwapigia kampeni hawa DPW ili wakabidhiwe Bandari zetu. Tuwataje majina yao na tuwaite ili wake watueleze kwa uwazi faida zinazopatikana Bandarini baada ya kukabidhiwa kwa DPW.
Mimi naanza kuwataja kwa Majina yao, tafadhali njooni huku ili mtueleze faida tunazopata kutoka kwa hawa DPW.
1. Mhe, Rais SSH,
Nilimsikia Mara nyingi wakati ule akiwasifia Hawa DPW na kudai kwamba wapewe bandari zetu.

Namuomba Mhe, Rais kwenye kila mikutano yake anayofanya kwenye ziara zake huko mikoani basi awe anawaelezea Wananchi juu faida tunazopata baada ya kugawa bandari zetu kwa DPW ili kuwaondolea wasiwasi wale wa-Tanzania waliokuwa wanapinga Mkataba wa DPW.
2. Makame Mbarawa.
Nawe jitokeze utueleze wa-Tanzania wenzako faida tunazopata kutoka kwa DPW.
3.Gerson Msigwa.
Nawe pia ujitokeze na utueleze, nilikusikia sana wakati ule ukiwapigia Kampeni DPW ili wapewe bandari zetu.
4....
 
Kampuni hii ilitangazwa kwa mbwembwe nyingi sana bungeni na kwenye media wa kwanza kuisfia kampuni hii alikuwa Musukuma, wakafuata Maulid Kitenge na wenzake pamoja na Prof. Makame Mbarawa

Sasa najiuliza nini kimeboreshwa katika bandari hiyo au DP World ni kiini macho cha wawekezaji wanaojichotea fedha za umma kwa mgongo wa DP World

Ile mitambo aliyosema msukuma iko wapi.

Pia soma > Nachojiuliza mkopo wa billion 864 nani analipa kama DP World wamepewa bandari ya Dar?
mahandsome men kutoka DUBAI faida kubwa ni kuoa watoto wa kipemba yakhe!!
 
Dpworld ilikuwa jina tu wenyewe ni ccm na wanaccm

Dp world ni mwavuli
 
Kila anaekuja anajikatia cha kwake anauza, anachukua chake, mpaka siku watanzania tunapiga chafya toka kwenye usingizi wa UMAUTI tuliolala, tutakuta tunamiliki udongo wa mfinyanzi tu.
 
Wadau tuache siasa za maji taka.Mmoja wenu aende pale bandari akaombe aingie ndani ya bandari ajionee mabadiliko makubwa waliyofanya DPW.
1.Wameleta mitambo ya kisasa ambayo bandari hawakuwa nayo.Mitambo hiyo ni ya kushushia na kupakia kontena katika meli.TPA walikuwa na mitambo ya kizamani na pia walitegemea mitambo ya kwenye meli zilizoleta kontena.
Hivo kupakia na kupaki kontena ilikuwa ni shughuli nzito hivo kusababisha meli kuchelewa.
2.Wameleta gari za kutosha kubeba kontena mara zinaposhushwa na meli.TPA walikuwa na gari za chache sana za namna hiyo ikasababishwa kontena kupangwa hovyo hivyo kupelekea kuchelewesha utoaji wa kontena bandarini.
3.Wamekuja na mpangilio mzuri wa huduma kiasi ambacho hata sisi tunaopewa huduma tunajiskia raha kufanya nao kazi
4.Mawasiliano kati ya wateja na DPW yamerahisishwa tofauti na wakati wa TPA.
5.imekuwa rahisi kutoa kontena bandarini ukiwa ofisni tofauti na wakati uliopita ilibidi ukapige kambi bandarini pamoja na kuwa umeshawalipa.Kwa maana ingine huduma yao lazima uinunue
6.Sasa hivi hakuna tena kusukumana bandari kama ilivokuwa kabla.Wakati ule unalipia huduma halafu unatoa na cha mbele na baado inabidi upiganie kupata huduma kwa sababu vifaa vilikuwa ni vichache na kila mtu alikuwa ni kambale.Yaani kila mtu bosi kuanzia messenjer, karani, supervisor ,dereva wa crane mpaka top kila mtu bosi katika nafasi yake.Hakukuwa na wakumfunga paka kengele
7.Msongamano bandari umepungua sana !
DPW wanafanya vizuri kuliko TICTS !
Sisi tunaofanya nao kazi (wateja) tunafurahi huduma zao .
Kwa hiyo nawashauri ombeni kwa uongozi wa TPA/DPW mwende mkajionee mabadiliko ya huduma sasa ni huduma bora kabisa
 
Jomo Kenyata alisema kweli watz ni maiti.kinachofanywa na dp world ni ujambazi Kwa Nchi yetu lakini Kwa kuwa viongozi wetu hawaoni tatizo Kwa kuwa ni sehemu ya wahusika wa huo mkataba haramu.wananchi tulitakiwa kuchukua hatua Kwa nguvu zote kuzuia huu mkataba wa kiporaji
 
Dah sijui hata niseme nini, acha maisha yaendelee ila hii bandari ni jipu na halina mkamuaji.
 
Tatizo mnaopiga kelele humu wala hamuiui bandari inafanyaje kazi ! Sasa mtu wa Mbeya kakulia Mbeya kasomea mbeya kama alikuja mjini kaishia mlimani wakati ule anashukia Ubungo Stand na kupandia Ubungo stand halafu leo eti anaizungumzia Bandari ? Hajui hata meli ikoje !
Jmani kazi za watu tuwaachie watu tuache porojo za mitaani !
 
Kampuni hii ilitangazwa kwa mbwembwe nyingi sana bungeni na kwenye media wa kwanza kuisfia kampuni hii alikuwa Musukuma, wakafuata Maulid Kitenge na wenzake pamoja na Prof. Makame Mbarawa

Sasa najiuliza nini kimeboreshwa katika bandari hiyo au DP World ni kiini macho cha wawekezaji wanaojichotea fedha za umma kwa mgongo wa DP World

Ile mitambo aliyosema msukuma iko wapi.

Pia soma > Nachojiuliza mkopo wa billion 864 nani analipa kama DP World wamepewa bandari ya Dar?
Mm binafs naona kitu kilicho badlika n jina kutoka TPA kwenda DP WORLD
 
Wadau tuache siasa za maji taka.Mmoja wenu aende pale bandari akaombe aingie ndani ya bandari ajionee mabadiliko makubwa waliyofanya DPW.
1.Wameleta mitambo ya kisasa ambayo bandari hawakuwa nayo.Mitambo hiyo ni ya kushushia na kupakia kontena katika meli.TPA walikuwa na mitambo ya kizamani na pia walitegemea mitambo ya kwenye meli zilizoleta kontena.
Hivo kupakia na kupaki kontena ilikuwa ni shughuli nzito hivo kusababisha meli kuchelewa.
2.Wameleta gari za kutosha kubeba kontena mara zinaposhushwa na meli.TPA walikuwa na gari za chache sana za namna hiyo ikasababishwa kontena kupangwa hovyo hivyo kupelekea kuchelewesha utoaji wa kontena bandarini.
3.Wamekuja na mpangilio mzuri wa huduma kiasi ambacho hata sisi tunaopewa huduma tunajiskia raha kufanya nao kazi
4.Mawasiliano kati ya wateja na DPW yamerahisishwa tofauti na wakati wa TPA.
5.imekuwa rahisi kutoa kontena bandarini ukiwa ofisni tofauti na wakati uliopita ilibidi ukapige kambi bandarini pamoja na kuwa umeshawalipa.Kwa maana ingine huduma yao lazima uinunue
6.Sasa hivi hakuna tena kusukumana bandari kama ilivokuwa kabla.Wakati ule unalipia huduma halafu unatoa na cha mbele na baado inabidi upiganie kupata huduma kwa sababu vifaa vilikuwa ni vichache na kila mtu alikuwa ni kambale.Yaani kila mtu bosi kuanzia messenjer, karani, supervisor ,dereva wa crane mpaka top kila mtu bosi katika nafasi yake.Hakukuwa na wakumfunga paka kengele
7.Msongamano bandari umepungua sana !
DPW wanafanya vizuri kuliko TICTS !
Sisi tunaofanya nao kazi (wateja) tunafurahi huduma zao .
Kwa hiyo nawashauri ombeni kwa uongozi wa TPA/DPW mwende mkajionee mabadiliko ya huduma sasa ni huduma bora kabisa
Kuna mtu personally ameacha kazi Bandari sababu sasa hivi akisha Sign in hawaruhusiwi kutoka Tena mpaka muda wa kazi uishe,

madereva hawaruhusiwi tena kushuka shuka kwenye magari na kuzagaa, ukifika unatoa karatasi zako, unaenda kwenye mzigo unapakia, kama upo kwenye foleni kaa kwenye Gari yako.

Wengi humu hata huko Bandari hawakujui.
 
Back
Top Bottom