Mgombea Urais kupitia Chama cha NLD Doyo Hassan Doyo ameutaja mfumo wa elimu ya Tanzania kuwa ni usio na maslahi kwa wananchi wake.
Doyo amezungumza hayo akiwa katika muendelezo wa kampeni zake Mkoa wa Rukwa katika Wilaya ya Sumbawanga Leo Oktoba 11, 2025 akisema mfumo huo unamfanya mwanafunzi asiweze kujitegemea na kuwa mbunifu huku akiahidi endapo akipewa ridhaa ya kuongoza nchi ataundoa mfumo huo.