Yes. This is a masterpiece. Huyu jamaa ni kichwa. Nimefurahia zaidi alivyochambua aina ya matatizo yanayotukabili kama taifa. Kutumia STI ni sawa, ila ni hicho ni kipengele kimojawapo tu. Najua asingeenda nje ya hapo kwa sababu ndiyo mada aliyoandaa, lakini tunachohitaji cha kwanza kabisa, hata kabla ya STI, ni mabadiliko ya mfumo wa utawala. Hakuna STI inayoweza kufanyika kwenye mazingira ya sasa ya ufisadi, kukosa uzalendo, na kukosa uelekeo wa kisiasa. Ametoa mfano mzuri wa Kagame. Ila ukweli ni kwamba Kagame mwenyewe kama rais ameamua kujenga nchi na kuachana na porojo. Tunachohitaji hapa Tz ni mtu kama Kagame. Ni bora wamuite dikteta lakini anajenga nchi. Kiongozi makini, asiyetaka porojo, akishakamata usukani, hizo STI zitajitokeza zenyewe tu kwa sababu vichwa na vipaji vipo. Yote kwa yote, huyu jamaa ametoa ujumbe mzito sana. Watu wengi tu wana mawazo mazuri kama haya, lakini linapokuja suala la utekelezaji kila kitu kinapwaya. Mungu atusaidie tupate viongozi wapenda nchi na wanaojali wengine. Bila uongozi madhubuti, mawazo kama haya yataishia tu kwenye makabrasha ya wakubwa maofisini. Wakati mwingine huwa watu wanaogopa kusema ukweli halisi kwa sababu inaweza kutia watu kiwewe na kukosa matumaini. Huyu jamaa ameongea ukweli halisi ulivyo, ingawa wanasiasa uchwara wasingependa kusikia mambo kama haya. Utawasikia wanasiasa uchwara, bila aibu wala haya, wakidai maisha ya Watz yamekuwa bora na kwamba "tumethubutu, tumeweza, na tunasonga mbele." Hakuna slogan ya kijinga kama hii. Wamethubutu upumbavu wakati nchi inaangamia?