Dovutwa amfananisha Lowassa na Kawawa

Dovutwa amfananisha Lowassa na Kawawa

sir.JAPHET

JF-Expert Member
Joined
May 18, 2012
Posts
699
Reaction score
137
Jumatano, Agosti 22, 2012 06:04 Na Khamis Mkotya

lowasa.jpg

Mbunge wa Monduli, Edward Lowassa

MWENYEKITI wa Chama cha United Peoples Democratic (UPDP), Fahmi Dovutwa, amemfananisha Mbunge wa Monduli, Edward Lowassa na Waziri Mkuu Mstaafu, marehemu Rashid Kawawa.
Katika taarifa yake kwa vyombo vya habari jana, Dovutwa alisema Lowassa hana tofauti na Kawawa, ambaye katika uhai wake akiwa waziri mkuu alibeba lawama za Serikali katika utawala wa awamu ya kwanza.

Dovutwa ambaye mwaka 2010 aligombea urais, alisema Lowassa hakuhusika katika kashfa ya rushwa iliyotokana na mkataba tata wa Richmond na kwamba alijiuzulu uwaziri mkuu ili kulinda heshima ya Serikali na si vinginevyo.

"Mwalimu Nyerere alipata kutoa hotuba siku moja akisema kwamba: ‘Namshukuru sana mzee Rashidi Mfaume Kawawa, amenisaidia sana.

‘Mambo yote ambayo amekuwa akilaumiwa Kawawa niliyafanya mimi na yeye (Kawawa) alibeba tuhuma hizo kwa ajili yangu', haya ni maneno ya Baba wa Taifa na hotuba zake hizi zipo," alisema Dovutwa akimnukuu Mwalimu.

Dovutwa aliongeza: "Kwa kauli hiyo ya Baba wa Taifa ni wazi Lowassa hakuhusika na kashfa ya Richmond. Kwa sababu maamuzi ya kiutendaji wa Serikali yako mikononi mwa Baraza la Mawaziri ambalo mwenyekiti wake ni Rais.

"Waziri yeyote hana uwezo wala mamlaka ya kuamua jambo bila ridhaa ya Rais. Lowassa aliwajibika ili kuilinda Serikali ya CCM chini ya Rais Kikwete isianguke na kupisha uchaguzi mwingine," alisema.

"Mwalimu Nyerere alielewa vizuri dhana ya uwajibikaji na Watanzania wengi hawakumwelewa Mwalimu Nyerere alipokuwa akiwarudisha baadhi ya watumishi ambao awali waliwajibika kwa tuhuma za kiutumishi.

"Kimsingi tuhuma alizokuwa amelaumiwa kiongozi mwandamizi wa Serikali zilikuwa ni tuhuma za kiongozi mkuu wa Serikali ambaye ndiye mwenye mamlaka ya kuamua kufanya jambo au kulikataa.

"Ili kuilinda Serikali na kiongozi mkuu wa Serikali ndipo hutokea mtumishi mmoja wa Serikali kubeba lawama na tuhuma za wizara yake kwa manufaa ya Serikali yenyewe.

Hivyo dhana ya kuwajibika ilieleweka vizuri kwa Mwalimu Nyerere kuliko wasomi walio wengi wa ndani na nje ya CCM," alisema Dovutwa.

Dovutwa alisema Lowassa ni kiongozi makini mwenye ujasiri ambaye aliweza kufanya mambo akiwa waziri mkuu, huku akiwatahadharisha wananchi kuwa makini na baadhi ya viongozi.

"Watanzania tusikumbuke kufanya mabadiliko ambayo huenda tukaondoa wala rushwa wadogo na kuingiza wala rushwa wakubwa zaidi," alisema.

Dovutwa aliwataka Watanzania kutafakari juu ya mwenendo wa vyama vilivyoko bungeni, hasa kutokana na Bunge kuchafuka kutokana na kashfa ya rushwa inayowahusisha wabunge.
 
Umenena ila urais hapati kwani zama za CCM zinaelekea ukingoni,tungependa atuongoze lakini chama chake tumekichoka na watanzania wanataka kubadili lishe.
 
Dovutwa mganga njaa ambaye hajui kusema na kichwa chake bali tumbo lake. Yeye ni nani kutumabia kwamba Lowassa hahusiki! Kafanya uchunguzi lini na ana mechanism gani? Ale ugali wake akalale!
 
Mpuuzi aliyemu-endorse jk leo anatuletea blahblah eti anamponda ni fisadi!!!!ignore this clown people..
 
Mgombea ubunge wa chama chake kule Igunga alizungumza maneno ya busara sana kuliko huyu bwana! (Nakumbuka maneno yake ya kuwataka vijana wasijianike kama "solar power", kuzinunulia shule "powertiller",( wasiende shuleni na majembe ya mkono kama baba Ubaya),mazao yao yatanunuliwa kwa paundi badala ya Tshs., na kuuza VX la ubunge kwa ajili ya maendeleo ya wana Igunga!
 
Ahaaaaaaaaaaaaa!!!!!!!!!!!!! uwiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiii!!!!! heheeeeeeeeeeeeeeeeeeee!!!!!!!! yaani nimecheka hadi basi, akya nani duh.....................
 
hii ieleweke kwamba jamaa katumwa akapige debe huko mbagala charambe Ilakapoteya njiya mwelekeze wakuu
 
Kwani amepona magonjwa yake ya matumbo huyu Dovutwa???
 
Kwa nini mtu ukimbilie Ikulu after all those problems you have gone through? Mwalimu Nyerere bado ni taa yetu whatever the mistakes he did kama binadamu. He said no to Mr. Lowasa! Alikuwa na maana yake Mzee Nyerere! I dont think if there is any need for Tanzanians to give chance to him to prove Mzee Nyerere wrong as I am 100% sure that he will prove Mzee Nyere to be right.
 
Mjini hapa watu kweli wanaishi kwa mbinu. EL kila mara kutafuta kutokea front pages asisahaulike. Na huyu Dovutwa nae anaamua kudandia mgongono kwa EL nae apate airtime. Anyway, na mimi kwa kumnukuu Mwalimu Nyerere huyo huyo, alishasema EL hatufai kwa kuwa ni fisadi. Haya ngoma droo.
 
JUMATANO, AGOSTI 22, 2012 06:04 NA KHAMIS MKOTYA

lowasa.jpg

Mbunge wa Monduli, Edward Lowassa

MWENYEKITI wa Chama cha United Peoples Democratic (UPDP), Fahmi Dovutwa, amemfananisha Mbunge wa Monduli, Edward Lowassa na Waziri Mkuu Mstaafu, marehemu Rashid Kawawa.

Katika taarifa yake kwa vyombo vya habari jana, Dovutwa alisema Lowassa hana tofauti na Kawawa, ambaye katika uhai wake akiwa waziri mkuu alibeba lawama za Serikali katika utawala wa awamu ya kwanza.

Dovutwa ambaye mwaka 2010 aligombea urais, alisema Lowassa hakuhusika katika kashfa ya rushwa iliyotokana na mkataba tata wa Richmond na kwamba alijiuzulu uwaziri mkuu ili kulinda heshima ya Serikali na si vinginevyo.

"Mwalimu Nyerere alipata kutoa hotuba siku moja akisema kwamba: ‘Namshukuru sana mzee Rashidi Mfaume Kawawa, amenisaidia sana.

‘Mambo yote ambayo amekuwa akilaumiwa Kawawa niliyafanya mimi na yeye (Kawawa) alibeba tuhuma hizo kwa ajili yangu', haya ni maneno ya Baba wa Taifa na hotuba zake hizi zipo," alisema Dovutwa akimnukuu Mwalimu.

Dovutwa aliongeza: "Kwa kauli hiyo ya Baba wa Taifa ni wazi Lowassa hakuhusika na kashfa ya Richmond. Kwa sababu maamuzi ya kiutendaji wa Serikali yako mikononi mwa Baraza la Mawaziri ambalo mwenyekiti wake ni Rais.

"Waziri yeyote hana uwezo wala mamlaka ya kuamua jambo bila ridhaa ya Rais. Lowassa aliwajibika ili kuilinda Serikali ya CCM chini ya Rais Kikwete isianguke na kupisha uchaguzi mwingine," alisema.

"Mwalimu Nyerere alielewa vizuri dhana ya uwajibikaji na Watanzania wengi hawakumwelewa Mwalimu Nyerere alipokuwa akiwarudisha baadhi ya watumishi ambao awali waliwajibika kwa tuhuma za kiutumishi.

"Kimsingi tuhuma alizokuwa amelaumiwa kiongozi mwandamizi wa Serikali zilikuwa ni tuhuma za kiongozi mkuu wa Serikali ambaye ndiye mwenye mamlaka ya kuamua kufanya jambo au kulikataa.

"Ili kuilinda Serikali na kiongozi mkuu wa Serikali ndipo hutokea mtumishi mmoja wa Serikali kubeba lawama na tuhuma za wizara yake kwa manufaa ya Serikali yenyewe.

Hivyo dhana ya kuwajibika ilieleweka vizuri kwa Mwalimu Nyerere kuliko wasomi walio wengi wa ndani na nje ya CCM," alisema Dovutwa.

Dovutwa alisema Lowassa ni kiongozi makini mwenye ujasiri ambaye aliweza kufanya mambo akiwa waziri mkuu, huku akiwatahadharisha wananchi kuwa makini na baadhi ya viongozi.

"Watanzania tusikumbuke kufanya mabadiliko ambayo huenda tukaondoa wala rushwa wadogo na kuingiza wala rushwa wakubwa zaidi," alisema.

Dovutwa aliwataka Watanzania kutafakari juu ya mwenendo wa vyama vilivyoko bungeni, hasa kutokana na Bunge kuchafuka kutokana na kashfa ya rushwa inayowahusisha wabunge.

Sasa ni Kwanini PRINCE anasema ataandika KITABU jinsi LOWASSA alivyomgeuka Baba yake JK KIKWETE?

huu uzi ulishakuwepo tatizo la viroba!
 
Kwani Mzee Kawawa akiwahi kujizulu Uwaziri Mkuu kwa tuhuma kama za Lowassa? RIP Mzee R. M. Kawawa
 
DOVUTWA njaa inamsumbua mzee huyu na lile kofia lake.
 
Back
Top Bottom