Smart Finance
Member
- Apr 10, 2025
- 35
- 114
Hii ni aina ya Fixed Income Security, yaani Serikali inakukopa pesa yako leo na Inakuahidi malipo ya riba ya kudumu (fixed 14% kwa mwaka), Na baada ya miaka 10, inakurudishia mtaji wako wote.
Riba ya 14% inabaki ile ile kwa miaka yote 10 bila kujali kama hali ya uchumi itabadilika — iwe mfumuko wa bei (inflation) au viwango vya riba mabenki vikibadilika.
Kwa hatifungani hii:-
📚 Riba hulipwa kila miezi sita (semi-annually), si kusubiri miaka 10.
📚 Kila malipo ni 7% ya thamani ya hatifungani yako.
Kwa mfano:
Kama ulinunua hatifungani ya thamani ya TSH 5,000,000, basi kila miezi sita unapokea TSH 350,000 (ambayo ni 7% ya TSH 5M).
Kwa mwaka mzima unapokea TSH 700,000 (yaani 14% ya mtaji wako).
Hivyo, unaweza kupanga matumizi yako kwa kutumia malipo haya ya mara mbili kwa mwaka.
Hatifungani hizi huuzwa kupitia mnada (auction) unaoratibiwa na Benki Kuu ya Tanzania (BoT). Watu na taasisi huwasilisha zabuni (bids) wakisema bei wanayotaka kununua. Bei inaweza kuwa ya punguzo au juu ya thamani halisi (Face Value).
Ukijua kuweka zabuni vizuri, unaweza kupata hatifungani kwa bei chini ya 100%, na hivyo riba yako halisi (yield) ikawa kubwa zaidi ya 14%.
Kwa mfano: Kama unapata kwa 95% ya thamani, riba yako halisi inaweza kufika hata 15% au zaidi.
Hatifungani za Serikali ni salama, lakini:-
🟥 Hatari ya Mfumuko wa Bei (Inflation Risk): Kama mfumuko wa bei nchini utaongezeka sana kupita 14%, mapato yako halisi yanaweza kupungua thamani.
🟥 Hatari ya ukwasi (Liquidity Risk): Kama ukihitaji kuuza kabla ya miaka 10, unaweza kulazimika kuuza kwa hasara kama soko litakuwa chini.
🟥 Hatari ya Riba (Interest Rate Risk): Kama viwango vya riba sokoni vitapanda baadaye (tuseme benki zianze kulipa 20%), thamani ya hatifungani yako inaweza kushuka kwenye soko la sekondari.
Faida za hizi Hatifungani Kwa mwekezaji wa kudumu
✅ Mapato ya kudumu: Kila miezi sita bila kukosa.
✅ Hakikisho la Mtaji: Unarudishiwa mtaji wote mwisho wa muda.
✅ Mauzo kwenye Soko la upili: Unaweza kuziuza kwenye Soko la Hisa la Dar es Salaam (DSE) kama ukihitaji pesa kabla ya miaka 10.
✅ Mapato ya hatifungani za Serikali ya Tanzania hayatozwi kodi ya mapato (withholding tax). Yaani:
Riba yote unayopata ni yako bila makato.
Kwa kifupi kabisa:
Hii ni fursa nzuri sana kwa mtu anayetaka: Kulinda fedha zake dhidi ya mabadiliko makubwa ya uchumi. Kupata mapato ya uhakika kila baada ya miezi 6. Kuwekeza kwa usalama mkubwa.
Kujua mengi kuhusu hisa na Hatifungani click hii linki kujiunga na darasa la bure
Follow the Smart Finance - SW channel on WhatsApp: Smart Finance - SW | WhatsApp Channel