Samcezar
JF-Expert Member
- May 18, 2014
- 13,095
- 22,705
Habari zenu watanzania
Kwanza napenda kudeclare wazi kuwa sina mashiko na ajenda za raisi wa marekani ndugu trump lakini pia sipo hapa kuzungumzia hii mada kwaajiri ya trump ila sisi watanzania na waafrika kwa ujumla.
Ni karne nyingi zimepita tokea sisi kama waafrika tuanze mahusiano na jamii tofauti na yetu kwa maana ya waarabu, wareno, wahindi, wajerumani, waingereza, wachina, na wamarekani pia. Lakini katika kujitafakari ni wapi hasa haya mahusiano kwetu ni yamekuwa ni ya kiutu nagundua kuwa jibu hapana. Katika miaka ya uhuru kama sisi kizazi cha sasa tungekuwapo ama itokee uvumbuzi wa time machine ya kutuwezesha kurejea tena miaka ile ya nyuma basi mtaungana nami kuwa raia wa bara hili yaani native africans walikuwa hawana haja ya mazoea na raia yeyote wa kigeni na walikuwa tayari kuvunja mazoea yeyote alimradi waafrika tubaki kama tulivyo wenyewe.
Sina kumbukumbu sahihi kuwa ni lini ama ni wapi jamii ilianza kutengeneza mawazo na tamaa ya kutaka kuona nchi za kimagharibi au nchi zingine za kiarabu ni mahala tunaweza kupageuza nyumbani kwetu badala ya afrika especially Tanzania. Leo hii ukitazama nchi kama somalia, nigeria, na kwengineko vijana ambao ndiyo nguvu kazi ya jamii yeyote, wako tayari kufia majini wakikimbilia nchi za ugenini kwenda kutafuta maisha na wakiwa hawana matarajio ya kurejea tena afrika hata kwa kuahidiwa kupewa mgodi. Huu ni walakini wa ajabu sana na ndio umenifanya leo kutoa mada hii ili wajumbe tushee knowledge.
Raisi wa marekani yaani ndugu Trump, siku za karibuni yaani wakati wa kampeni zake, alitoa moja ya ajenda zake amabazo aliahidi kuzifanyia utekelezaji mara atakapo kaimu nafasi ya uraisi toka kwa ndugu obama. Ndugu Trump aliweka wazi kuwa hatopenda tena kuona kasi ya wahamiaji kutoka mataifa mbali mbali kuja kwenye bara la amerika ikiendelea bali anataka kuona ikipungua na hatimaye kukoma kabisa. Na katika kusema hivyo aliweka wazi kuwa mataifa hayo ni ya Mexico, Afrika, na baadhi ya jamii za Uarabuni. Lengo likiwa ni kuwataka kila raia abaki kwao taifa la marekani sio jalala la masikini kwenda kutafutia maisha au shamba la bibi kwenda kuchuma matembele.
Katika ajenda hiyo ambayo imetafsiriwa na jamii mbali mbali za duniani kuwa ni ajenda ya kibaguzi imenifanya ni kae chini na kufanya uchambuzi wa kina sana. Katika uchambuzi wangu nikaamua kufananisha ndugu Trump na ndugu wa damu ama mtu aliyesomeshwa na mzazi wako kipindi anashida kisha miaka ilipokwenda akaja kufanikiwa na kuwa mtu mwenye uwezo kiuchumi sana kutokana na msaada wa 90% kutoka kwa wazazi wako walivyomsaidia kipindi ukiwa mdogo. Sasa umekua kijana mkubwa, umefika muda wa kwenda shule, wazazi wameshatangulia mbele za haki, sasa wewe huna wa kumtegemea ila yule ndugu, ila ulipoamua kuchua maamuzi ya kwenda kulalamikia shida za mahitaji ya shule kwake akaamua kukukatalia na kukwambia hawezi kukusaidia kila mtu ahangaike kwa bidii yake kwa maana wazazi wako wangekuwekea akiba usingetegemea kutoka kwake kisa alisaidia na wazazi wako, hivyo basi fadhila si lazima kulipa.
Katika mfano huo hapo juu najaribu kuangalia sisi kama waafrika namna tunavyojikomba sana katika mataifa ya watu na kusahau kuwa kama ilivyo kwa jamii za wanyama hata binadamu tumetofautiana sana na ni muda sasa wa kuzitambua hizo tofauti na kuamua kujitathimini kuwa na sisi tunasimama wapi. Ukirejea miaka si mingi hapo nyuma, Taifa kama China lilikuwa ni mojawapo kama ya sisi, walikuwa masikini wa kiuchumi, sera za kisiasa hazieleweki, tamaduni zao zilipuuzwa duniani walikuwa ni makabwela kama sisi waafrika. Ulifika muda jamii ya wachina walikaa chini(sijui nani aliwakalisha chini ila nina uhakika hakuwa makonda), wakajitathimini kuwa wao kama jamii katika hii dunia wanaonekana vipi kwa wengineo. Kwa maana back in days, raia wa kichina akikutana na wa uingereza alikuwa anaonekana ni mkazi wa dar akutane na mjia maisha Dar anayetokea kigoma mwisho wa reli na nguo zenye viraka. Hii tafasiri yake ni kuwa wachina hawakuwa chochote mbele ya raia wa uingereza kwa wakati huo. Ila hali ipoje wakati huu, ni kwamba raia wa uingereza anatambua kuwa mchina ni moja ya raia wenye hadhi ya kuitwa binadamu.
Hebu chukua hiyo picha hapo juu halafu jaribu kufananishia sisi waafrika tunaonekanaje katika jamii ya kimataifa. Najua majibu yatatofautiana ila maana itakuwa ni moja kuwa tunaonekana kama jamii ya hadhi ya chini sana. Thamani tuliyonayo na inayotufanya tukutane na mataifa ya nje ni hizi rasilimali zetu za asili ambazo hayo mataifa yanazihitaji kwaajiri ya kufanyia maendeleo yao na si vinginevyo. Ila kama wanajamii katika ulimwengu, waafrika ni watu wa mwisho kabisa na hatuna thamani hata kidogo, si kwa mila wala tamaduni zenu zenye maana, si kwa rangi zetu za asili, si kwa historia yetu, si kwa lugha zetu, sisi si chochote. Usije ukajidanganya na maswala ya imani kuwa kwakua tuna christians, muslims na other adopted rituals kama ufreemason ukahisi sisi na wao ni sawa si kweli, hakuna anayetuthamini, si wazungu, si waarabu si wachina, si wahindi. Ni ukweli mchungu ila kuumeza ni wajibu wetu.
Leo trump anatangaza waafrika ni miongoni mwa jamii ambazo hazitaki pale marekani je umesikia china au uingereza, au russia, au germany imetajwa?! Je hii inakupa picha gani ukiamua kujitathimini kama muafrika na si muhanga wa maneno ya trump na kujiunganisha na waarabu na wamexico.....lahasha....wewe kama muafrika mweusi tiiii kama Baraka de prince au kuntakinte unasimama wapi?!
Jibu ni rahisi sana na sote tunalijua. Trump anahaki ya kusema vile especially kwetu sisi waafrika ambao tumekuwa tukiamini kuwa bila muingereza au marekani au mrusi au mchina hatutaweza pata maendeleo. Katika ulimwengu wa leo wa kiutandawazi ni aibu kwa taifa la kiafrika kama tanzania kuwa na wimbi la vijana wanaokimbilia nje ya nchi za watu huku jamii ya wanafikra wa tanzania wakitizama na kuona ati ni sahihi kwakuwa hali ni ngumu. Nani ka kwambia kuwa kwenu kukiharibika unatakiwa kukimbia na kwenda kwa jirani huku ukiangalia kwa dirishani jinsi kunavyosambaratika. Huu ni ujinga wa karne. Sizungumzi hapa kulenga viongozi, wanawake, wanaume, wazee, ama vijana ila nalenga kuzungumza na waafrika wa tanzania. Sote tunahusika katika hili.
Badala ya kutumia huu muda kutafakari ubaya wa trump, ni muda wa kutafakari ujumbe wa MUNGU uliojificha nyuma ya hiyo ajenda ya trump. katika mfano wetu pale juu ni kuwa ndugu aliyefadhiliwa na wazazi wako si lazima akulipie fadhila wewe anaweza kukataa maana ni juhudi zake zimemfikisha pale na ukitumia zile hasira za kukataliwa vizuri kwa kupambana na maisha yako ili utoke na kuja kumuonyesha kuwa yeye si chochote katika kufaulu kwako kimaisha ndipo hapo utaamini kuwa juhudi binafsi ndizo ambazo humletea mtu maendeleo. Nasema hivi kutokana na jamii ya kiafrika kujisahau wakidhani ni sahihi kwa wao kwenda kwenye mataifa ya watu ikiwamo marekani kutafuta maisha wakikwepa ajenda ya kubaki kwao kurekebisha ili na wao jamii yao isimame. Sina haja ya kuwatetea waarabu kwa kuzuiliwa maana wao si kama mimi kila mtu ajali kwao, mimi ni mwafrika na hii ni kauli mbiu nawapigia waafrika wenzangu popote duniani walipo, rudini nyumbani, kidogo mnachokipata kileteni huku nyumbani kisha mrejee sisi bado tunahangaika na kubadili mifumo ya kizembe inayotufelisha kila uchao na viongozi wasanii ambao ni maigizo tu tumewaachia wamekalia viti na nyadhifa takatifu za kitaifa. Mwafrika mwenzetu martin Luther alishawahi kusema, " I HAVE A DREAM" na "ONE DAY WE SHALL OVERCOME". Watoto wa Afrika msiogope, kaka na wajomba zenu tunaanza sasa kusimama katika kujenga heshima ya mwafrika upya hapa duniani, tudai kiti chetu cha heshima katika meza ya heshima ya kimataifa. Ni muda sasa wa kusahau silaha, vita na fujom kama suluhu ya matatizo. Waafrika tupeni silaha zenu majalalani, chukueni peni, tuanze kuiandika upya historia ya jamii yetu ya mwafrika. Tunavingi vya kuandikia kizazi kijacho muda ni huu wakufanya vya kuandikwa wakati huo ukifika. Tuunde mfumo mpya wa jamii yetu, elimu mpya, falsafa mpya, role models wapya, na ari mpya. Sipo hapa kuhamasisha vyama ila ni jamii ya waafrika isimame kwapa moja. Tupa kule urithi wa tamaduni za kimagharibi na za kiarabu. Dini iwe jambo binafsi ila value zetu za kitaifa na kijamii na sheria za taifa ziwe ni ngao yetu katika jamii ya mwafrika.
TRUMP YOU ARE RIGHT, EVERYBODY SHOULD BUILD THEIR HOMES NOT YOUR HOME.