Donald Trump will never ever be POTUS!

Nyani Ngabu

Platinum Member
May 15, 2006
86,641
2,000
Chini hapo ni video za mkusanyiko wa watu waliokuwa wanaapia kuwa Donald Trump kamwe hatoweza kuja kuwa rais wa Marekani.

Nami nakiri kuwa nilikuwa mmoja wa hao watu licha ya kwamba uchaguzi wa mwaka huu ulikuwa ni uchaguzi wa mabadiliko [change election] ambao hutokea mara nyingi kila baada ya miaka 8 ambapo rais wa chama kimoja anakuwepo madarakani kwa muda wote huo wa mihula miwili.

Hivyo, kwa kufuata utamaduni huo wa chaguzi za kisiasa, mwaka huu ulipaswa kuwa ni mwaka wa chama cha Republican kushinda uchaguzi mkuu. Lakini kwa vile ambavyo mgombea wa chama hicho alivyokuwa akijinadi, maoni ya watu wengi yalikuwa kwamba hawezi kabisa kushinda.

Ila uzuri wa mambo ni kwamba kura na maoni ya watu yanayojalisha na kuhesabika ni ya wale ya watu waendao kupiga kura siku ya uchaguzi.

Kura za maoni na maoni ya wataalamu [mimi nawaita wajuaji] hayajalishi na wala hayahesabiki kabisa.

Na ndicho haswa kilichotokea siku ya tarehe 8 mwezi Novemba, mwaka 2016 ambapo Bw. Trump, licha ya watu wengi kuona kuwa hawezi kumshinda Bi. Clinton, alijishangaza hata yeye mwenyewe kwa kuibuka kidedea katika uchaguzi mkuu huo wa taifa bora kabisa kuwa kutokea katika uhai wa mwanadamu.

Ingawa sikuwa namuunga mkono, lakini nilifurahi sana. Kilichonifurahisha kuhusu huo ushindi wake ni kitendo chake cha kuwatia kidole cha kati wale wote waliokuwa wanamdharau, kumkebehi, kumkejeli, na hata kumzushia mambo lukuki.

Nilifurahi mno kwa sababu karibu dunia nzima, vyombo karibu vyote vya habari, hususan vile vya ndani vya Marekani, vilionyesha upendeleo wa wazi kabisa dhidi yake. Yaani viliamua kuitupilia mbali kabisa miiko yote ya uandishi wa habari na kuamua kumuunga mkono yule bibi na kumpinga Trump.

Ila licha ya vigingi vyote hivyo, jamaa akaibuka juu.

Shikamoo Bw. Donald J. Trump.

Nguruvi3 El Jefe The Boss
 

fyddell

JF-Expert Member
Dec 19, 2011
5,771
2,000
According to your own word kuwa hukutaka ashinde that means hata wewe pia kakupiga kidole cha kati.
You're engulfed by your own word haha.
 

Bavaria

JF-Expert Member
Jun 14, 2011
48,272
2,000
Uchaguzi wa Marekani ni sawa na kura zilizopigwa Brexit.
Waliomchagua Trump ni wazungu ambao wengi waliamini katika sera yake kuhusu uhamiaji.
 

Nyani Ngabu

Platinum Member
May 15, 2006
86,641
2,000
Uchaguzi wa Marekani ni sawa na kura zilizopigwa Brexit.
Waliomchagua Trump ni wazungu ambao wengi waliamini katika sera yake kuhusu uhamiaji.
Unajua Trump alipata asilimia ngapi ya kura za African-Americans na Latinos ukimlinganisha na John McCain na Mitt Romney?
 

Jindal Singh

JF-Expert Member
Sep 9, 2015
1,856
2,000
Trumph alitakiwa ashinde tu! kulingana na system ya US na mahitajio yao ya ushawishi katika dunia, US kuna tabaka ambalo linaitwa The Establishment hawa watu miaka yote lazima wawepo katika kuendesha maslahi ya America, na system ya US haimes katika kipande hiki. Kama ilivyokuwa Tz vile na The Establishment yao, na system ya Tz haichezi katika kipande hichi, ndio maana...
 

JipuKubwa

JF-Expert Member
Jun 1, 2013
2,222
2,000
Nilianiamini Trump anashinda, kwasababu opponents wake walikuwa wanamshambulia binafsi zaidi.
 

Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom