Jambazi
JF-Expert Member
- Jan 18, 2014
- 16,644
- 18,707
Rais wa Marekani Donald Trump amesema angependa kukutana na kiongozi wa Korea Kaskazini Kim Jong-un, iwapo kungekuwa na mazingira mahsusi. Amesema ingekuwa "heshima kuu kwake". "Kungelikuwa na hali mahsusi kwangu kukutana naye, ninge kutana naye - bila shaka. Ingekuwa heshima kuu kwangu kufanya hivyo," Bw Trump aliambia shirika la habari la
Bloomberg Jumatano. Jumapili, alikuwa amemweleza Bw
Kim kama "kijana mwerevu". Tamko la Bw Trump limetokea huku wasi wasi uki endelea kuongezeka kuhusu mpango wa nyuklia wa Korea
Kaskazini. Ikulu ya White House baadaye ilitoa taarifa kufafanua matamshi ya Bw Trump na kusema Korea Kaskazini
ingehitaji kutimisha masharti mengi kabla ya mkutano kati ya viongozi hao wawili kufanyika. Msemaji wa ikulu hiyo Sean Spicer alisema Washington inataka kuona tabia ya uchokozi ya Korea Kaskazini ikikoma mara moja. "Ni wazi kwamba kwa sasa, hakuna mazingira mahsusi (ya kufanikisha mkutano kama huo)," aliongeza.
Source: bbc