Donald Trump ashinda majimbo matano muhimu ya mchujo

RUCCI

JF-Expert Member
Oct 6, 2011
1,701
1,714
160427025551_sp_trump_640x360_afp_nocredit.jpg


Donald Trump ameshinda mchujo wa kuteua mgombea urais wa chama cha Republican katika majimbo matano ya Marekani yaliyopiga kura Jumanne.

Mgombea wa chama cha Democratic Hillary Clinton ameshinda majimbo manne kati ya matano yaliyoshiriki mchujo.

Baada ya matokeo kubainika, Bw Trump alijitangaza kuwa “mgombea mteule” wa Republican.

Ushindi wake Connecticut, Delaware, Maryland, Pennsylvania na Rhode Island unamfanya kukaribia sana kutimiza idadi ya wajumbe inayohitajika kumhakikishia ushindi kabla ya kuandaliwa kwa mkutano mkuu wa chama hicho wa kuidhinisha mgombea Julai.

Upande wa Democratic, Bi Clinton amenyimwa ushindi kamili na Bernie Sanders ambaye ameshinda katika jimbo la Rhode Island.

Bw Sanders ameaoa kuendelea na mchujo.

Akiongea katika ukumbi wa mikutano wa Philadelphia baada ya kushinda majimbo hayo manne, Bi Clinton amesema kampeni yake inaweka “malengo jasiri na ya kupiga hatua mbele” katika kuimarisha maisha ya watu Marekani.

“Sisi tunaamini katika wema wa watu wetu na ukuu wa taifa letu,” alisema.
Naye Bw Trump aliwaambia wafuasi wake New York kwamba hatabadilisha sera zake iwapo atachaguliwa kuwa rais.

"Sibadiliki,” alisema. “Mnafahamu kwamba nilisomea shule bora zaidi. Mimi ni mtu mwerevu sana. Nitaiwakilisha nchi hii kwa heshima na vyema sana.

"Lakini sitaki kubadilisha sifa zangu binafsi. Mnajua, ndizo zilizonifikisha hapa.”

Wapinzani wake, Ted Cruz na John Kasich, tayari wameanza kuangazia majimbo yajayo, wakiungana kusaidiana kushinda majimbo ya Indiana, Oregon na New Mexico.

Bw Trump ameshutumu ushirika wao akisema ni ishara ya kukata tamaa.


Chanzo: BBC
 
The problem facing Donald Trump is he is not a politician. He is a realistic person who speaks the actuality of the situation. His running mates are politicians whom speak what people want to hear but which they don't believe in their hearts. Trump is not a politician that is why is not liked by Republican establishment who are supporting the other candidates viz Ted Cruz and John Kasich.
However lay Republicans and even delegates see him as a right Presidential materials. There are some efforts and campaigns against Trump but derailing him it would likely cost the Republicans and their sympathizers whom want to end the era of Democrats. Next phase will portray the actual scenery.
 
Trump ni hatari kwa dunia

Mkuu Trump pamoja lugha yake kali deep down ni binadamu safi sana, ataleta amani Duniani kwa kipindi chake cha Uongozi, watu hawajui tu - binadamu hatari ni Clinton - Mama huyo akifanikiwa kuingia Ikulu ya Marekani Dunia itapita katika kipindi kigumu sana peacewise labda akijirudi.
 
Mm huwa nawashangaa sana watu wanao sema Trump hapendwi Na wamarekani wengi.
Inamaana hao wanao mchagua ni wakina Nani.
mkuu note kuwa trump anaogopeka na wamrekani kwa ujumla na mataifa makubwa ya dunia, yakiwemo uchina na ulaya... hivyo hzo figisu figisu ni za kuwatia hofu wafuas wa trump ili wakate tamaa. but trump analijua hlo na nadhan amejizatiti kivyake kukabiliana na hzo challenges....TRUMP katokea nje ya mfumo ambao unatengeza marais wengi wa marekani na ulaya kitu ambacho kinaongeza HOFU kwa watu wa democratic et al . misimamo yake mikali ndo chanzo kingine cha hzo hofu, pamoja na mikakat yake ya kurudisha biashara marekani ili kuachana na importation za china,canada na mexico.
 
Naamini hakuna bahati mbaya kwa hiyo hata akishinda yeye au mwingine ni kwa kusudi jema tu. Tutafika.
 
Back
Top Bottom