Domayo mbioni kurudi Uwanjani

Domayo mbioni kurudi Uwanjani

Rugby Union

JF-Expert Member
Joined
Nov 21, 2012
Posts
402
Reaction score
257
cde70c980f0af7bcffa2bc539a6c433f.jpg


​
Kiungo mpya wa Azam FC,Frank Domayo ameanza kujifua na mazoezi ya Gym,kwa ajili ya kujiandaa kuingia uwanjani Januari mosi,baada ya kukaa nje ya uwanja kwa muda mrefu kutokana na kuuguza majeruhi ya nyama za paja.


Domayo amesajiliwa Azam msimu huu kama mchezaji huru baada ya kumaliza mkataba wake na Yanga lakini alipojiunga na timu hiyo alipelekwa nchini Afrika Kusini,kufanyiwa upasuaji wa mguu uliokuwa na majeruhi aliyoyapata akiwa Yanga.


Mchezaji huyo alianza mazoezi ya Gym,Jumatano ya wiki hii na Azam,ambapo alisema maendeleo ya mguu wake yapo vizuri tofauti na awali.


Wachezaji wa Azam huwa wanatumia Gym yao ya kisasa iliyopo kwenye uwanja wao wa Azam Complex,Chamanzi nje kidogo ya Dar es Salaam.


“Nikijaliwa uzima nitahakikisha nafanya kile kilichowavutia viongozi kunisajili,hivyo najituma kwa bidii ili niweze kuwa fiti,lakini naamini nitafanya mambo makubwa nikishirikiana na wenzangu.”


Domayo ni kati ya wachezaji ambao usajili wao ulitikisa na kugusa hisia za wadau wa soka nchini,jambo alilosema hatakubali heshima yake ishuke kipindi atakaporudi uwanjani kucheza soka.

KandandaGalacha
 
Back
Top Bottom