Dola yaidhibiti Chadema | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Dola yaidhibiti Chadema

Discussion in 'Habari na Hoja mchanganyiko' started by kilimasera, Dec 23, 2010.

 1. kilimasera

  kilimasera JF-Expert Member

  #1
  Dec 23, 2010
  Joined: Dec 2, 2009
  Messages: 3,073
  Likes Received: 17
  Trophy Points: 135
  Polisi wavunja mkutano wake Arusha
  Mbowe, vigogo waenda kuokoa jahazi
  Naye John Tendwa ajitosa kusuluhisha

  Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema)
  Zaidi ya magari 40 ya Jeshi la Polisi na idadi kubwa ya pikipiki, jana zilitumika kusambaratisha wafuasi wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema) na kuuvunja mkutano wa hadhara uliopangwa kuhutubiwa na Mbunge wa chama hicho Jimbo la Arusha, Godbless Lema.
  Lema alitarajia kutoa ufafanuzi kuhusiana na utata wa uchaguzi wa nafasi ya Umeya na Naibu Meya katika Manispaa ya Jiji la Arusha uliofanyika Jumamosi na kukishirikisha Chama Cha Mapinduzi (CCM) pekee.
  Katika tukio la jana majira ya saa 5:00 asubuhi, magari ya polisi yakiwa na askari waliovalia mavazi rasmi na wakiwa na mabomu, walitanda kila mahali, huku wakipiga king’ora.
  Pia askari hao walikuwa na gari la maji ya kuwasha kwa lengo la kuwatisha wananchi wasihudhurie mkutano huo.
  Hali ilizidi kuwa tete pale Mbunge Lema alipolazimika kutinga katika viwanja vya mkutano eneo la NMC akiwa amejifunika bendera na kushangiliwa na umati wa watu waliokuwa wameanza kukusanyika.
  Hata hivyo, kabla ya Mbunge huyo kuzungumza chochote, magari ya polisi yalivamia eneo la mkutano na kuwatimua wananchi kwa maelezo kuwa Jeshi la Polisi halikutoa kibali cha mkutano huo. Akizungumzia kitendo hicho, Lema alisema ameshangazwa na hatua ya Jeshi la Polisi kuwazuia kufanya mkutano wao wakati chama kilishaandika barua ya taarifa ya mkutano huo na kuomba kupatiwa ulinzi siku moja kabla.
  Alisema barua hiyo ilipokelewa na ofisi ya Mkuu wa Polisi wa Wilaya (OCD) Wilaya ya Arusha, lakini jana walishangaa kuwakuta polisi wametanda kila kona ya Jiji la Arusha.
  “Hii ni ajabu kwani Arusha kuna nini hasa kwenye umeya wa Manispaa hii. Kila nikitaka kufanya mkutano nazuiwa mpaka vitisho ndipo niruhusiwe. Je, ingekuwa CCM wangezuiwa?,” Alihoji na kuongeza: ”Huu ni uonevu.”
  Lema alisema baada ya kuzuiwa, alilazimika kwenda kwenye ofisi ya Kamanda wa Polisi Mkoa wa Arusha, Thobias Andengenye, ili kujua sababu ya kuzuia mkutano huo.
  “Sababu aliyotupa Andengenye ni kuwa hawana polisi wa kutosha kulinda mkutano, ila cha ajabu wanao polisi wa kutosha kutanda kona zote za Arusha leo na kusababisha hofu kwa wananchi na kuacha kufanya kazi zao, huku barabara zikifungwa,” alisema.
  Lema alisema anashangaa kuona wanasema hakuna polisi wa kutosha lakini jana kundi la askari lilikuwa likimfuatilia kila kona alikokuwa akielekea.
  Wakazi kadhaa wa Manispaa ya Arusha, walihoji sababu za polisi kuvunja mkutano huo wakati mbunge ana haki ya kusikilizwa na wananchi ili kujua kero zao.
  Mkazi mmoja alisema mbunge ana haki ya kufanya mkutano na wameshuhudia wabunge wa CCM wakifanya mikutano mingi isiyotangazwa na ya ghafla na wanaruhusiwa lakini Chadema ni dhambi kufanya mkutano licha ya kuutangaza na kuwaandikia barua polisi ya kutoa taarifa.
  Halima Hamisi, alisema inashangaza CCM wanafanya mikutano bila kudhibitiwa na polisi.
  Akizungumza na waandishi wa habari, Kamanda Andengenye alithibitisha kupokea kwa barua kutoka kwa viongozi wa Chadema kupitia ofisi ya OCD na kwamba OCD alipoipata aliisoma na kuona kuna mapungufu mengi, kama vile kutoeleza madhumuni ya mkutano huo.
  Pia makosa mengine makubwa mawili ambayo OCD aliyosema aligundua ni kutotimiza masharti ya kuipeleka barua hiyo ndani ya saa 48 na wakati Chadema waliipeleka ndani ya saa 29.
  Alisema sababu nyingine iliyosababisha kuzuiwa kwa mkutano huo ni kwamba Polisi ilipata taarifa kuwa kama mkutano huo ungefanyika, kuna vijana waliokuwa wamejiandaa kuvunja maduka, hivyo wakaamua kuchukua hatua hiyo. “OCD anayo mamlaka ya kuzuia mkutano iwapo anaona kuna utata wa mkutano huo kufanyika na kuna dalili ya ukosefu wa amani,” alisema na kuongeza kuwa kama Chadema wanataka kufanya mkutano, wasubiri Mwaka Mpya Krismas zipite, ili kusubiri wananchi watulize jazba.

  MBOWE aenda Arusha
  Muda mfupi baada ya kuvunjwa kwa mkutano huo, Mwenyekiti wa Taifa wa Chadema, Freeman Mbowe, aliwasili jijini Arusha na kukutana na madiwani wa chama hicho na kuwaomba viongozi wenye busara kuingilia kati sakata la Arusha, ili kuweka sawa hali ya usalama.
  Mbowe pia aliitaka serikali kumchukulia hatua OCD wa Arusha, Zuberi Mwombeji na Mkurugenzi wa Manispaa ya Arusha, Estomy Chang’ah, kwa kukiuka sheria na kanuni za uchaguzi.
  Mbowe alitoa kauli hiyo wakati akizungumza na waandishi wa habari, huku akiwa ameongozana na wabunge wa majimbo mbalimbali ya mikoa jirani na Arusha.
  Alisema Chadema kimeheshimu kuvunjwa kwa mkutano huo kutokana na busara na heshima za Inspekta wa Jeshi la Polisi (IGP) Said Mwema, na siyo Polisi Arusha kwa sababu wamekuwa wakitumia madaraka yao vibaya kunyanyasa nguvu ya umma na kumdhalilisha Mbunge.
  “Chadema Taifa tunatoa tamko kwamba, tunaomba jitihada za makusudi zichukuliwe na viongozi wa Taifa ambao hawajaweka akili pembeni, kumhamisha huyu OCD na mkurugenzi kama siyo kuwafukuza kazi, kwani hawajui nini umuhimu wa kutumikia wananchi,” alisema Mbowe.
  Alisema kutokana na CCM kufanya uchaguzi kinyemela Desemba 18, mwaka huu na kumchagua Gaudence Lyimo kuwa Meya na Naibu Meya, Michael Kivuyo wa TLP, Chadema hawawatambui wote kwani walichaguliwa kwa kukiuka sheria.
  “Mkurugenzi amekiuka sheria kwa makusudi siyo kama hazijui ila aliamua kuweka akili pembeni, hivyo tayari nimeongea na Msajili wa Vyama vya Siasa, John Tendwa, na yeye anawasiliana na Waziri wa Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (Tamisemi), George Mkuchika, ili tufanye mazungumzo kufikia mwafaka,” alisema.
  Mbowe alisema wakati Mkurugenzi anakiuka kanuni na sheria, OCD naye anashirikiana na kikosi chake cha Kuzuia Ghasia (FFU) kunyanyasa nguvu ya umma na kumpiga mbunge wa Chadema, hivyo lazima naye achukuliwe hatua za kisheria.
  Alisema yanayotokea Arusha yanafanana na yanayotokea halmashauri nyingine kama Hai, Mwanza na Kigoma.
  Alisema Mbunge anayo mamlaka ya kuitisha mkutano ili kuzungumza na wananchi wake na polisi hawana mamlaka ya kuwafukuza, bali wajibu wao ni kulinda amani.
  Mbowe alisema Chadema Taifa wametoa nafasi hadi Januari 4, mwakani, ili viongozi wenye busara wakae pamoja kuweka mambo sawa na iwapo itafika Januari 5, mwakani, watalazimika kutangazia umma kuandamana kudai haki yao ya msingi.
  Hata hivyo, alisema kama chama chao kimetoa tamko kutoingia katika vikao vya halmashauri mpaka mwafaka upatikane na kwamba watakuwa tayari kukaa kwenye vikao hivyo kushirikiana na viongozi walioingia kwa kuchaguliwa kisheria.
  Lakini alisema hatua yao ya mwisho baada ya kushindikana kwa mazungumzo, watakwenda mahakamani kushtaki kwa sababu ya kuvunja sheria za nchi kwa makusudi kulikofanywa na viongozi wachache kwa manufaa yao binafsi.
  CHANZO: NIPASHE
   
 2. G

  Gad ONEYA JF-Expert Member

  #2
  Dec 23, 2010
  Joined: Oct 26, 2010
  Messages: 2,641
  Likes Received: 4
  Trophy Points: 135
  Wenzenu wamegundua hawezi kuishi kwa kutenda ukweli! Lazima ku-fluke ndo watafaidi! Ndo nchi yetu imefika huko. You try to live a decent/straight life, you die a poor man!
   
 3. d

  dotto JF-Expert Member

  #3
  Dec 23, 2010
  Joined: Sep 29, 2010
  Messages: 1,720
  Likes Received: 18
  Trophy Points: 135

  Huyu ni Mwanamke au !!! Atakuwa alishakuwa Jambazi! Halafu atakuwa hana Dini! Halafu atakuwa alishaua Albino!Halafu ni Uchochoro upstairs!
   
 4. Kobe

  Kobe JF-Expert Member

  #4
  Dec 23, 2010
  Joined: Jun 17, 2009
  Messages: 1,756
  Likes Received: 361
  Trophy Points: 180
  No hali kama hii sio nzuri kwa siku za usoni. ingependeza kila jambo lifanyiwe utaratibu mzuri pasiwepo manung'uniko nalawama za aina yeyote ile.
   
Loading...