Dola/Mataifa yaliyotikisa dunia na kuwa wababe wa dunia katika historia.Ya Marekani na China hivi sasa Historia inajirudia?

N'yadikwa

JF-Expert Member
Joined
Aug 10, 2014
Messages
4,676
Points
2,000

N'yadikwa

JF-Expert Member
Joined Aug 10, 2014
4,676 2,000
Wengi hawafahamu kwamba Misri ni miongoni mwa Mataifa ya dunia yaliyowahi kuwa na nguvu kubwa ya uchumi na maarifa ukiachilia mbali dola zinazosifika na kufahamika zaidi kwenye historia ikiwemo BABELI,UMEDI NA UAJEMI,ROMA,UGIRIKI,DOLA YA OTTOMAN nk nk

HAPA CHINI NI ORODHA YA MATAIFA YALIYOSHIKA UCHUMI WA DUNIA KWA NYAKATI TOFAUTI HUKU MISRI IKING'ARA KAMA ILIVYO KWA MAREKANI HIVI LEO:

Kadiri ya mwaka 4000 Kabla ya Kristo: Maisha ya kuishi mjini ndio yanaanza kuibuka huku mji wa kwanza ukiyumkinika kuwa ni Sumer. Uruk unaaminika kuwa ndio mji mkongwe kabisa na wa awali kwa mujibu wa historia ghafi.

Mwaka 3000 Kabla ya Kristo: Misri Upper na Lower zinaungana,na kuifanya Misri kuwa Taifa lenye nguvu zaidi duniani(hapa ndio unakutana na storia za wana wa Canaan kutumikishwa huko misri)...Mafirauni walikuwa na mpunga hatari kwao ilifika wakti dhahabu ilikuwa kama chuma hivi leo.

Mwaka 2300 BCE: Dola ya Akkadian ilizaliwa na kuwa ndio dola ya kwanza katika historia kwa mujibu wa historia ghafi.

Mwaka 1500 BCE: Misri inaibuka tena na kuwa Taifa lenye nguvu zaidi duniani.

Mwaka 1200 BCE: Bado Misri ipo kileleni.

Mwaka 1000 BCE: Wakati Mashariki ya Kati ikiwa katika Mchafukoge(Machafuko),Dola ya Zhou Magharibi huko Uchina inaibuka na kuwa dola yenye nguvu zaidi duniani.

Mwaka 700 BCE: Dola Mpya ya Ashuru (Syria),ikiwa na makao yake Mesopotamia,iliibuka na kuwa ndio dola yenye nguvu zaidi duniani. Zinagatia dola hii ya Ashuru ilikuwa kati ya Iran, Syria na Uturuki...wengine wanasema ni eneo la Mashariki mwa Mediterania.

Mwaka 500 BCE: Dola ya Achaemenid iliibuka kuwa mwamba wa dunia,ikiwa imechipuka kwenye Taifa la Iran ya leo, kwa ufupi unaweza kusema hii ni dola ya Uajemi. Umedi na Uajemi zilifahamika sana zikiongozwa na Koreshi Mkuu ambae hivi leo nadhani ndio muendelezo wa hawa viongozi wakuu wa huko Iran kina Ayatollah.

Mwaka 200 BCE: Dola za Han, Mauryan, Seleucid, na Jamhuri ya Rumi zilikuwa zikichuana vikali kutwaa ubabe wa dunia. Sasa kwa kuzingatia India ilikuwa na uchumi mkubwa na idadi kubwa ya watu basi wengi waliipa turufu dola ya Han(India) kwamba nayo wakati huu ilishika usukani na kuwa mbabe.

Mwaka 50 BCE: Dola ya Han Uhindi iliendelea kushika hatamu.

Mwaka 100: kukatokea mvutano mkali baina ya dola hii ya Uhindi na dola ya Rumi cha kufurahisha ni kwamba hawa wote wawili wakafanikiwa kujitwalia eneo(milki) ya ukubwa wa skwea kilomita Milioni 6.5.wote wawili walikuwa wakikaribiana sana kwa idadi ya watu takribani milioni 100 chini ya udhibiti wao...na wote wawili walikaa hapo kileleni kwa zaidi ya karne Nne...baadae wote wakadondoka.

Mwaka 300: Dola ya Jin,Rumi,na Sassanid ziliendelea kuchuana vikali kutwaa udhibiti wa dunia,lakini dola ya Sassanid haikuwa kubwa kama zilivyo hizo dola mbili. kwa hiyo mchuano ukaachwa kwa Rumi na Jin hata hivyo Rumi akaibuka kidedea na kuendelea kuongoza dunia tena. ZINGATIA: zama hizo kuongoza dunia ilikuwa ni pamoja na nguvu yako ya kuwa na milki kubwa,watumwa wengi na wafuasi wa kutosha bila kusahau jeshi lenye nguvu na watu wenye maarifa makubwa hasa ya sayansi ya vita.


Mwaka 450: Ikaibuka dola ya Gupta (Ustaajabu ya akina Gupta wale wa sauzi wametoka mbali) na Dola ya Rumi ya Mashariki dola hizi zikachuana vikali. Wakati huu dola ya Gupta ilishinda.

Mwaka 600: Dola ya Sui (Uchina) ikashika hatamu baada ya mchuano mkali baina yake na dola za Rumi Mashariki na Sassanid(Hii Sassanid isikuchanganye ni IRAN).

Mwaka 800: Dola ya Kiislamu ya The Abbasid ilishindana na dola ya Tang ya Uchina na hatimae kunyanyuka kidedea.

Mwaka 1000: Ushindani mkubwa ni kati ya dola ya Rumi, Song Dynasty,dola ya Ghaznavid (hii ilikuwa Iran), dola ya Chola (Kusini mwa India) na dola ya kidini ya Fatimid (ikiwa Misri). Wakati huu Ulaya Magharibi ilikuwa nyuma sana kiteknolojia na ilikuwa na idadi ndogo mno ya watu kuliko dola nyingine zote hasa za upande wa kule Asia. Kipindi hiki iliibuka dola ya Song kutawala dunia ikiwa na nguvu ya uchumi wa dhahabu(Hii ni dola ya Uchina). ZINGATIA Uchina ilikuwa na dola kadhaa zilizotawala kwa nyakati tofauti...kwa hiyo baadae unapotoa maksi zihesabu hizo kwamba ni uchina katika ujumla wake.

Mwaka 1250: Dola ya Mongol ilichipuka na kusumbua dunia....Hii ni dola gani....Hii ni dola iliyoibuka kutokea Mongolia,Dola hii ilijitanua na kutwaa milki hadi upande wa Ulaya Mashariki na baadhi ya Maeneo ya Ulaya ya Kati ikienda hadi upande wa Asia katika Bahari ya Japan huku ikisambaa hadiupande wa Kaskazini ikifikia hadi Siberia,huku upande wa Mashariki na Kusini ikienda hadi India,na eneo lililoitwa Indochina na upande wa safu za mwambao wa Iran; hadi Levant na milima ya Carpathian huko Ulaya pia. Dola hii inafikirika ndiyo hasa ilianza kuipa Ulaya tambo tunazoziona leo maana ilijitanua kwa fujho.


DOLA HII NDIO IKAWA KUBWA SANA KATIKA HISTORIA NA NDIYO WATU WENGI WANAYOIFAHAMU.

1500: Dola ya Ottoman, ambayo ilipambana vikali na himaya ya Ming...na kwa wakati wake ikawa dola kubwa kabisa iliyotikisa dunia.


Ufaransa 1700: Chini ya Louis XIV katika kipindi hiki lilikuwa ndio Taifa lenye nguvu kabisa Ulaya...lakini uongozi mbovu haukuifikisha mbali Ufaransa kwenye mabavu..Ni katika kipindi hiki nchi kadhaa za Ulaya zikaanza kuibuka ikiwemo Hispania ambayo ilikuwa na himaya kubwa tena ya Kikoloni lakini ilishindwa kufurukuta kwa sababu ya uongozi mbovu....Uingereza nayo ikawa inajitutumua kwa kumiliki tuvijisiwa kadhaa huko Ulaya kwa hiyo hapo Ulaya kukawa na tunchi kadhaa twenye ushawishi na ndio wakati huu Atlantic trade,inachipuka...Hata hivyo haikuwa wazi saana kwamba Ulaya ilikuwa ndiyo dola yenye nguvu duniani kwa sababu zile dola za Asia bado zilikubwa mbabe!

Mfano dola ya Ottoman ambayo ilitawala ukanda mpana sana Asia Ulaya hadi Afrika ilikuwa imekazana pia wakati huo...Huku dola ya Qing huko uChina sambamba na dola ya Mughal huko India zilikuwa ngangari pia....katika kipindi hiki inayumkinika kwamba dola ya Qing ya Uchina ndiyo ilikuwa yenye nguvu zaidi duniani kwa kigezo cha idadi kubwa ya watu na uchumi mnono wa dhahabu na biashara kubwa kubwa.


1815: Vita ya Napoleonic inafikia tamati. Wakati huo huo Mapinduzi ya Viwanda (Industrial Revolution) ndiyo yalianza kuibua nguvu isiyodhibitika ya zile dola za Ulaya na hatimae kuwa juu ya hawa wote wa Asia waliokuwa wanategemea watumwa,upinde na mshale kujenga dola zao... Ni katika kipindi hiki Ufaransa ambayo pamoja uongozi mbovu bado ilikuwa ndiyo yenye miguvu kwa zile dola za Ulaya...ambapo baada ya Vita ya Napoleon walipaswa kuendeleza ukanda wa Ulaya...

Wakati huu huu Austria-Hungary na Urusi hawa wote walikuwa na dola kadhaa kubwa sana,kama ilivyo kwa dola ya Qing ya Uchina. Lakini kwa kipindi hiki pamoja na ushawishi wa Ufaransa hapo Ulaya, ukubwa wa hizi dola mbili za Urusi na mwenzio Hungary, ukubwa na nguvu ya Mchina na dola yake pale Asia...Uingereza akiwa sasa ndio KITOVU cha Mapinduzi ya Viwanda huku akiwa na jeshi la kisasa kwa wakati huo linalojua makombora akawa ndie mbabe sasa wa dunia.(si ana viwanda?, si ana teknolojia?) Hapa ndio nguvu ya akili dhidi ya miguvu ikaanza kuonekana)

Karne ya 19

1914: Ulaya ina kila unaloweza kulitaja kwenye Teknolojia kuanzia ile ya vita,nyumbani,miundombinu,usafiri nk....Urusi Ufaransa, Austria-Hungary, na Italia ni Mataifa yenye nguvu pia wakati huu lakini hawamfikii Uingereza.....na pia hao usingewafananisha na Ujerumani,na Wamarekani,ambao wakati huo walikuwa ndio wababe watatu wakubwa muhimu wa dunia wakiongozwa na mwingereza.

Pamoja na kwamba Marekani alikuwa na Uchumi na ni mbabe kiasi lakini hakuwa nalo jeshi lolote la kumtisha Uingereza au Ujerumani kwa wakati huu.

Ujerumani kwa mfano kwa wakti huu alikuwa na watu wa kutosha na Jeshi bora...lakini Uingereza kwa wakati huu anayo Himaya kuubwa mno na jeshi bora na lililojitosheleza kila eneo kuanzia majini hadi ardhini huku akiwa na kiburi cha teknolojia...
Uingereza kwa wakati huu alikuwa pia anajivunia uwezo wake wa kumudu diplomasia na hatimae kufanikiwa kuwashawishi Marekani Italia na Japan kuwa upande wake wakati wa vita ya kwanza ya Dunia...kwa hiyo Uingereza hapa ndo mbabe wa dunia.

1919: Baada ya Vita ya Kwanza ya Dunia kumalizika,mataifa mengi ya Ulaya yamepata hasara kubwa kutokana na madhira ya vita....huku watu wake wengi wakifariki kwenye mapambano....wakati huohuo pamoja na Marekani kuwa mshirika wa Uingereza kwenye vita hiyo ya kwanza yeye hakuweka miguvu miingi kumsaidia kivita ila kijamii kwa kupeleka mahitaji ya vita zikiwemo silaha,maakuli na magwanda nk....Bado pamoja na kubafuliwa katika kipindi hiki Uingereza inakuwa sawa na Marekani kiuchumi...alietangulia katangulia tu.


1939: Marekani Uingerza na Ujerumani hapa wanaibuka na kuwa washindani wakubwa...huku kila mmoja kwa wakati huu akiwa na nguvu za kumtosha kabisa yaani sema hakuna wa kumtisha mwenzake kihiivyo kwamba umenizidi nini!....Wakati huu Marekani akawapiku wenzake( yeye muda huu alikuwa na ndege njema si inatakiwa aendelee kuwapa msaada na kuwakkopesha ili warekebishe uchumi na kujenga tena miji yao iliyoharibiwa vibaya kwenye vita ya kwanza ya dunia?...na vita yenyewe ilikuwa inapiganwa town.

1942: Ujerumani wakati huu ilikuwa inadhibiti karibia nusu ya bara la Ulaya....wakati huu kina Hitler na NAZI movement ilikuwa ndo inashika hatamu.....katika kipindi hiki wabashiri wanasema kama NAZI wangefanikiwa kumwangusha mwingereza au Mrusi basi Ujerumani ingetwaa kikombe na kuwa mbabe wa dunia...lakini walishindwa,....Marekani akaendelea kuwa mbabe...

1945: Marekani,Muungano wa Sovieti,na Uingereza wanachuana vikali....lakini bado Marekani ndie mbabe.

2009: Ni Marekani bado.Hakuna jeshi wala uchumi unaoweza kulinganishwa nao.

2017-2019: Marekani na Uchina:Vita ya uchumi kila mmoja akimtunishia misuli mwenzake NANI ATAIBUKA KIDEDEA?.....Je, ni dalili kwamba China inakaribia kurudisha heshima yake ya karne na karne kwamba ndie mbabe wa dunia?....ukisoma hapo historia unaona China ndie katawala dunia kwa muda mrefu zaidi.
 

Dripboy

JF-Expert Member
Joined
Mar 22, 2019
Messages
3,206
Points
2,000

Dripboy

JF-Expert Member
Joined Mar 22, 2019
3,206 2,000
Porojo nyiiiiiingi ila hazina uhalisia na yanayoendelea sasa, hii ni karne ya 21 na si karne ya 6 wala ya 1 mzee.

Watu wako more advanced kwenye kila kitu Misri na Roma zitabaki kama nguzo tu ya historia ni makumbusho ya dunia
 

Fiati

JF-Expert Member
Joined
Oct 9, 2013
Messages
1,176
Points
2,000

Fiati

JF-Expert Member
Joined Oct 9, 2013
1,176 2,000
Porojo nyiiiiiingi ila hazina uhalisia na yanayoendelea sasa, hii ni karne ya 21 na si karne ya 6 wala ya 1 mzee.

Watu wako more advanced kwenye kila kitu Misri na Roma zitabaki kama nguzo tu ya historia ni makumbusho ya dunia
Mkuu umeonyesha kuwa wewe ni mwepesi mnoo.Lengo la mtoa mada ni kuonyesha kuwa unayoyaona Leo kumbe yalikuwako Jana na juzi Hakuna jipya.
 

N'yadikwa

JF-Expert Member
Joined
Aug 10, 2014
Messages
4,676
Points
2,000

N'yadikwa

JF-Expert Member
Joined Aug 10, 2014
4,676 2,000
Porojo nyiiiiiingi ila hazina uhalisia na yanayoendelea sasa, hii ni karne ya 21 na si karne ya 6 wala ya 1 mzee.

Watu wako more advanced kwenye kila kitu Misri na Roma zitabaki kama nguzo tu ya historia ni makumbusho ya dunia
Dripboy kunywa maji urudi,hakuna porojo kwenye historia.Tujadili nimechokoza mada kutoka kwenye kwa historians na hiyo relevant extract.Karibu
 

N'yadikwa

JF-Expert Member
Joined
Aug 10, 2014
Messages
4,676
Points
2,000

N'yadikwa

JF-Expert Member
Joined Aug 10, 2014
4,676 2,000
Unaandikaje uzi kama huu bila kumtag Malcolm. Subiri nikuitie.
CC Malcom Lumumba njoo huku nawe udadavue story hii.
Huwa najiepusha kuwatag individuals sababu huwa inasababisha wanabodi wengine kuona kwamba hawajatiliwa maanani...ukizingatia hii public forum. Namkaribisha Malcom kwa mchango wake
 

Dripboy

JF-Expert Member
Joined
Mar 22, 2019
Messages
3,206
Points
2,000

Dripboy

JF-Expert Member
Joined Mar 22, 2019
3,206 2,000
Dripboy kunywa maji urudi,hakuna porojo kwenye historia.Tujadili nimechokoza mada kutoka kwenye kwa historians na hiyo relevant extract.Karibu
Historia hizo kamwe hazitowahi kujirudia niamini.

Ni sawa na muingereza au mjerumani aje kututawala tena NEVER watatutawala kwa namna nyingine na si ile ya awali
 

Forum statistics

Threads 1,382,315
Members 526,332
Posts 33,824,100
Top