mtapa wilson
Member
- Jan 2, 2014
- 10
- 13
Uchungu wa mwana aujuaye mzazi. Hivi mnapata hisia za maumivu na uchungu kama wanazopata hawa kina mama?
Hivi mmeona ile picha ya Bi Theresia Ngowi (Mama mzazi wa Mbunge wa Kawe, Halima Mdee) akiwa amesimama pembezoni mwa kitanda alicholala mwanae pale hospitalini Aga Khan huku akibubujikwa na machozi?
Bi Theresia analia. Anahisi maumivu makali anayoyapata mwanae baada ya kuvunjwa mkono na askari.
Vipi kwa mama yake Ester Bulaya (Mbunge wa Bunda Mjini), ambaye anaugulia maumivu ya mgongo baada ya kupigwa, kukanyagwa kifuani na askari wanaoishi kwa kodi za Watanzania?
Ester amesema, "askari magereza alisema ametupania sana hasa mimi na Halima....kwanini tuliwahi kutolewa gerezani maana walikuwa wamepania kututesa gerezani...askari aliendelea kusema nipo kwenye himaya yangu naweza kuwafanya chochote," Je, hiyo ni kauli sahihi kutolewa na askari?
Fikiri pia, vipi kuhusu mama mzazi wa Henry Kilewo (Katibu mkuu chadema mkoa wa Dar es Salaam) akiona jeraha la mpasuko kichwani kwa mwanae?
Kosa lao nini? Je, kosa lao ni kwenda viunga vya gereza la Segerea kumpokea kiongozi wao wa chama ambaye ni Mwenyekiti wao, Freeman Mbowe, baada ya wananchi kumlipia faini yake?
Hivi mliona ule msafara wa Katibu wa Itikadi na Uenezi wa Chama cha Mapinduzi (CCM) Taifa, Humphrey Polepole alipokwenda kumpokea kada wao mpya Vincent Mashinji? Mliona msafara wa magari na idadi ya makada aliokuwa ameambatana nao?
Hivi mliona kuna askari aliyemsukuma hata singi mtu mmoja aliyekuwepo katika msafara wa Polepole? Hivi mlisikia hata mlio wa baruti siku hiyo?
Ukisikia wapinzani wanasema hii nchi inaendeshwa kwa 'double standard' basi muelewe ndio hivyo. Yaani suala lilelile moja akilifanya mtu mmoja ni sawa lakini akilifanya mtu mwingine kavunja sheria. Waswahili wanasema. Ashakum si matusi. Kunya anye kuku akinya bata kaharisha.
Sasa mtambue kuwa ile kauli ya Katibu mkuu CCM Taifa, Dk. Bashiru Ally haikuwa ya bahati mbaya. Si mlimsikia wenyewe akisema kuwa chama kilichoshika dola kinatakiwa kutumia dola kama nafuu yake kusalia kwenye dola.
Au mmesahau niwakumbushe? Dk. Bashiru alifafanua akiwa mkavu kweli usoni akasema kwa mifano kabisa kuwa, vyama vyote tawala vilitoka madarakani baada ya kushindwa kutumia vizuri dola.
Jeshi la polisi ni chombo cha dola. Haya yanayofanywa na chombo hiki cha dola kwa maana nyingine, tunaweza kusema ndio matumizi mazuri ya dola ya walioshika dola nchini Tanzania kama alivyosema Dk. Bashiru.
Ni furaha kwa walioko kwenye dola wakiona vyombo hivi vinatumika kunyanyasa wakosoaji wao ili mradi tu wabakie kwenye dola.
Kiongozi wa chama kilichoshika dola aliwapamba wanawake wa Tanzania kwenye siku yao (Machi 08, 2020) kuwa serikali yake inawathamini. Vyombo vyake vya dola leo vinapiga wanawake nae yuko kimya. Sishangai si alishasema angeweza kupiga hata mashangazi wa mtendaji wake mkuu kama wangeandamana kule kwao.
Si mmeona hata ile picha ya mionzi inayosambaa mitandaoni ikionyesha jinsi Mbunge Halima Mdee alivyovunjwa mkono wake?
Hata enzi za utawala wa kibaguzi nchini Afrika Kusini wapo waafrika weusi waliokuwa wakiimba mapambio dhidi ya utawala wa makaburu. Walisifu na kuwadhihaki waafrika wenzao waliokumbana na mkono wa chuma.
Serikali ya Misri chini ya utawala wa Rais Hosni Mubarak ilioondolewa madarakani mwaka 2011 licha ya kuwa na jeshi zuri lililojiimarisha kimbinu pamoja na kuwa na silaha bora za kijeshi. Hayakuwa mapambano mepesi lakini nguvu ya umma ilishinda nguvu ya dola.
Wananchi wanajenga chuki na visasi dhidi ya vyombo vya dola kwakuwa wanaona vinatumika vibaya na dola dhidi yao wakati wakipigania haki yao.
Si mnakumbuka lile tukio la kuuwawa kwa askari kule mkoa wa Pwani wilaya Kibiti? Si mliona watu walivyokuwa wanashangilia huko mitandaoni? Tusiwalaumu na kuwaona sio wazalendo. Ile ni chuki iliyojengwa na walioshika dola kwa manufaa yao.
Mwalimu Nyerere amewahi kusema kuwa mawazo hayapigwi rungu. Mawazo yanapingwa na mawazo yaliyo bora zaidi.
Hoja za wapinzani zisipingwe rungu. Vyombo vya dola visitumike kunyanyasa na kunyamazisha sauti za wapinzani.
Maumivu ya wapinzani yanajenga chuki na mgawanyiko kwenye taifa. Si mnaona zile faini zilivyokusanywa. Waliochanga ni wananchi wa taifa hili? Sio kila mtu anafurahishwa ama kuchukizwa na yale wanayofanyiwa wapinzani wa nchi hii.
Yote ya yote, chuki, ghiriba na mitafaruku haijawahi kuwa na hatma nzuri katika taifa. Ukianza kuona dola inaonea wananchi, hiyo ni hatma mbaya kwa watawala. Hivyo ndivyo ilivyokuwa kwa Blaise Compaore wa Burkina Faso, Hosni Mubarak wa Misri, Yahya Jammeh wa Gambia na watawala wengine wakiimla barani Afrika na ulimwenguni kote.
Sent using Jamii Forums mobile app