Infantry Soldier
JF-Expert Member
- Feb 18, 2012
- 17,306
- 19,880
Kwanini kaka mkubwa?Ninaweza kusema NDIO na HAPANA kwa wakati mmoja.
Kwa sababu Tanzania ndio nchi yenye demokrasia bora afrika nzima.Kwanini kaka mkubwa?
Hii ya Tanzania haina ubishi kwamba sisi ndio the best Afrika. Sasa vp kuhusu nchi zingine kama Rwanda, Uganda, Cameroon, Libya ya Gadaffi, etcKwa sababu Tanzania ndio nchi yenye demokrasia bora afrika nzima.
Mkuu, kwa hiyo una maanisha "Africa doesn't has its own (unique) definition of democracy" but follows the generally-accepted one? Au sio?Tafsiri ya Demokrasia ni MOJA TU mahali kokote kule ama popote pale na wakati wote.
Tofauti na hapo, ni kitu kingine kabisa.
Ndio, kwa maana ya kwamba, uwepo wa Demokrasia barani Afrika unatokana ama utatokana na hiyo tafsiri MOJA TU iliyopo mahali kokote kule ama popote pale na wakati wote ambayo kwa hiyo ama kwayo tunaweza kuihakikisha kuwa ipo.Mkuu, kwa hiyo una maanisha "Africa doesn't has its own (unique) definition of democracy" but follows the generally-accepted one? Au sio?
Kama nimekosea ninaomba unisahihishe. How was I supposed to put it?Kwamba does Africa has.....?!
Dunia ya sasa imeisha- prove wrong dhana hiyo mkuu. Hivyo unavyo itasfiri wewe, yule au mimi si lazima iwe sawa. Kwani tafsili Ile haikuwa ' law' bali ilikuwa 'principal' tu.Tafsiri ya Demokrasia ni MOJA TU mahali kokote kule ama popote pale na wakati wote.
Tofauti na hapo, ni kitu kingine kabisa.
Hatuwezi kuwa definition yetu ya democracy kwa kuwa hili neno lenyewe tumeletewa na hao wazungu wakaleta na definition yaoShikamooni wakubwa zangu wote wa hapa jamiiforums. Mimi mdogo wenu (Last Born) Infantry Soldier nipo mzima kabisa wa afya. Thanks to God the Almighty.
Eti ndugu zangu watanzania;
Does Africa has its own (unique) definition of democracy?
View attachment 1516346
Nimeamua kuuliza hivi kwa maana kwamba, nimepokea ujumbe huu kutokwa kwa mtoto wa ndugu yangu analiyezaliwa na kuishi huko huko Ulaya (Uholanzi) na hajawaji kukanyaga huku Tanzania (Africa). Huyu dogo ana miaka 15, kama angekuwa huku Tanzania let's say labda angekuwa form II?
Just imagine wewe ndio Infantry Soldier, ungewezaje kumjibu huyu mtoto wa ndugu yako?
PUMZIKA KWA AMANI MZEE MKAPA. VITA UMEIPIGANA NA MWENDO UMEUMALIZA BABA YETU. MUNGU AKUPE PEPO ILIYO NJEMA MZALENDO MWENZANGU.
View attachment 1516337
OUR MOTTO: ENDELEA KUWA MZALENDO IPENDE TANZANIA. USICHAFUE TASWIRA NJEMA YA TAIFA LAKO. USTAWI WA NCHI YETU UNAANZA NA WEWE. TIMIZA WAJIBU WAKO IPASAVYO.
Huo utofauti wa kuitafsiri Demokrasia ni makosa yanayofanywa na watu kwa kujua ama kwa kutokujua.Du
Dunia ya sasa imeisha- prove wrong dhana hiyo mkuu. Hivyo unavyo itasfiri wewe, yule au mimi si lazima iwe sawa. Kwani tafsili Ile haikuwa ' law' bali ilikuwa 'principal' tu.
Suala linalohitaji mjadala mpana unalijibu kiurahisi rahisi na unahitimisha unachokijua ndiyo jibu.Huo utofauti wa kuitafsiri Demokrasia ni makosa yanayofanywa na watu kwa kujua ama kwa kutokujua.
Si sahihi kabisa kwa kitu chenye tafsiri MOJA inayoeleweka kutafsiriwa tofauti na tafsiri yake inayopaswa kuwa.
Iweje utengeneze kitu kingine tofauti na ukipe tafsiri ya 'Demokrasia'? Kwanini usikipe kitu hicho tafsiri ya kuendana na jinsi kitu hicho kilivyo?
Hebu nawe ndugu lijibu suala hilo 'kiugumu ugumu' kupitia huo "mjadala mpana" kisha hitimisha kile unachokijua.Suala linalohitaji mjadala mpana unalijibu kiurahisi rahisi na unahitimisha unachokijua ndiyo jibu.
Siwezi kufanya hivyo maana najua ninachochangia.Hebu nawe ndugu lijibu suala hilo 'kiugumu ugumu' kupitia huo "mjadala mpana" kisha hitimisha kile unachokijua.
Asante.
sawa@Siwezi kufanya hivyo maana najua ninachochangia.
Nitakachoweza ni kutoa maoni tu. Sio kuhitimisha mjadala.
Ninaona umeamua kuandika kitabu kizima. hakika wewe ni noma.Bwana Infantry Soldier,
Demokrasia kama nadharia na kanuni ya kiutawala husisitiza kwamba uhalali wa utawala wowote ule duniani ni lazima utoke kwa wananchi na siyo vinginevyo, pia uhalali wa utawala ni lazima ulenge katika kuwafanya hawa wananchi wapate maendeleo. Hapa unaweza ukawa na mfumo wa aina yoyote ile, aidha Ufalme (A Monarchy), Udini (A Theocracy) au Jamhuri (A Republic) muhimu kabisa ni kwamba lazima nguvu itoke kwa wananchi na siyo vinginevyo.
Watawala lazima watawale kwa matakwa ya wananchi kwa kufuata sheria, kanuni na taratibu zilizowekwa baina ya watawala na watawaliwa. Watawala hawatakiwi kufanya jambo lolote lile ambalo litaathiri mustakabali wa wananchi bila wananchi kuhusishwa. Wakijiamulia tu mambo, tena ambayo yanaumiza watawaliwa basi uhalali wao wa kutawala unapotea.
Wanafalsafa wa kale kama John Locke, Thomas Hobbes na Jean-Jacques Rousseau walizungumzia kitu kiitwacho The Social Contract ambapo walisema mataifa hutengenezwa kwa makubaliano baina ya watawala na watawaliwa. Pindi watawala wanavunja hayo makubaliano na kujiamulia kufanya jambo ambalo litawadhuru wananchi wao basi wanapoteza uhalali.
Nakubaliana na Mzee Nyerere kwamba kila sehemu ina Demokrasia yake, japo lazima tukubali kwamba tunaweza kutoa tafsiri mbalimbali za demokrasia na tusiwe na tafsiri moja kuhusu demokrasia. Lakini nachelea kusema kwamba lengo la demokrasia ni moja tu duniani kote, kwenye mifumo yote ya utawala nalo ni "KUHAKIKISHA NCHI INAWALIWA KWA KUFUATA MATAKWA YA WATAWALIWA"
Hivyo basi naweza kumaliza kwa lugha ya kiingereza kwa kusema haya yafuatayo "Democracy as a value does not have a single accepted Universal definition. We can only define Democracy well through a Purposive Approach of what democracy aims to achieve within a particular society. And that is Ensuring the power to rule is derived from the people for their benefit: Suffice to say it, such benefit should always be just, moral and equitable"
NB: Tusijitie moyo, katika hili wenzetu wazungu pamoja na Ubepari wao wametushinda mbali sana. Kitendo cha kutawala kwa kufuata miiko ya kisheria kwa manufaa ya wananchi ndicho kimewafanya wafike hapa walipo leo: Sisi Afrika hata Katiba kuheshimu ni shida, utasemaje kwamba tuna demokrasia yetu ???