Dodoma yakumbwa na uhaba mkubwa wa sukari

Dibo10

JF-Expert Member
Apr 2, 2012
1,307
1,583
Habari wakuu, moja kwa moja niende kwenye mada, hali mjini Dodoma si shwari kuna uhaba wa sukari ambao haujawahi kutokea, wakati vyombo vya habari vikiwa bize na kuripoti yanayotokea mjengoni mjini hapa, huku mtaani hali ni mbaya sana, sukari imeadimika kabisa na ukibahatika kuikuta inauzwa kwa sh 6000.

Sukari sasa imekuwa ni bidhaa ya anasa, walalahoi wameacha kunywa chai rasmi, haya wadau wadau naomba kuwasilisha, acha niwahi usafiri wa kwenda Dodoma niwapelekee ndugu zangu sukari.
 
Habari wakuu, moja kwa moja niende kwenye mada,hali mjini dodoma si shwari kuna uhaba wa sukari ambao haujawahi kutokea,wakati vyombo vya habari vikiwa bize na kutipoti yanayotea mjengoni mjini hapa,huku mtaani hali ni mbaya sana,sukari imeadimika kabisa na ukibahatika kuikuta inauzwa kwa sh 6000. Sukari sasa imekuwa ni bidhaa ya anasa,walalahoi wameacha kunywa chai rasmi,haya wadau wadau naomba kuwasilisha, acha niwahi usafir wa kwenda dodoma niwapelekee ndugu zangu sukari.
c dodoma2 mkuu ni nchi nzima
 
kweli awamu ya tano ni awamu ya hapa kazi tuu..
-njaa
-uchinjaji wa binaadamu
-mfumuko wa bei
-wananchi kubaguana
-mivutano na wafanyabiashara hadi bidhaa zinaadimika
-uvunjaji wa nyumba
-timuatimua wakati mwengine kwa kukurupuka
-wanafunzi wasio hatia kutimuliwa kwa nguvu za vyombo vya dola
-kuwaziba midomo wanaotaka bunge lioneshwe live
-kufutwa kwa posho mbalimbali za kujikimu wakati walizungumzia kuboresha maslahi ya wafanyakazi..
KWELI HAPA KAZI TU..
 
Nilikuwepo huko kwa wiki mbili mfululizo, hali imebadilika sana kuanzia mwanzoni mwa wiki hii,tukajua hali itaimarika bahati hali inazidi kuwa tete mkuu,nimerejea toka huko juzi tuu,
Hukupita pale pembeni ya Makao makuu ya chama chetu opposite na NMB kuna duka pale la mama mmoja alikuwa anauza 3500 official price hapepesi macho mchana kweupe tena anakwambia ndiyo amepata sukari ya kata.
 
Back
Top Bottom