GE2025 Dodoma: Watumishi Magereza 1611 wapewa majiko ya gesi

GE2025 Dodoma: Watumishi Magereza 1611 wapewa majiko ya gesi

Matukio, Taarifa, Habari na Mijadala ya Wananchi WAKATI wa Mchakato wa Uchaguzi Mkuu 2025

Mkalukungone Mwamba

JF-Expert Member
Joined
Aug 29, 2022
Posts
2,437
Reaction score
5,235
Katika utekelezaji wa Mkakati wa Taifa wa Matumizi ya Nishati Safi ya Kupikia, Wakala wa Nishati Vijijini (REA) umegawa majiko na mitungi ya gesi kwa Maofisa na Askari wa Jeshi la Magereza katika mikoa 14 nchini ili kulinda afya zao kwa kuwaondoa kwenye matumizi ya kuni na mkaa.

Akizungumza Agosti 6, 2025 kwenye hafla ya uzinduzi wa ugawaji wa jumla ya majiko na mitungi 1,611 katika magereza sita ya Mkoa wa Dodoma, iliyofanyika Gereza la Isanga, Mjumbe wa Bodi ya Nishati Vijijini (REB), Mhandisi Sophia Mgonja amesema hatua hiyo ni sehemu ya juhudi za serikali ya awamu ya sita chini ya Rais Samia Suluhu Hassan katika kusambaza nishati safi kwa Watanzania wote.

"Ni matarajio yetu kwamba Maofisa na Askari mtaendelea kutumia nishati hii safi na kuwa mabalozi kwa jamii nyingine. Tusiwaruhusu kurudi nyuma kwa kutumia tena kuni au mkaa. Hii ni hatua ya kulinda maisha, afya na mazingira,” amesema Mhandisi Mgonja.

Kwa upande wake, Mkuu wa Magereza Mkoa wa Dodoma, Kamishna Msaidizi wa Jeshi Magereza (ACP) George Wambura, amesema kupokea majiko na mitungi hiyo ni uthibitisho kuwa serikali inajali afya na ustawi wa Maofisa na Askari wake.

“Niwahimize Maofisa na Askari wote, baada ya mitungi hii kuisha gesi, hakikisheni mnaijaza na kuendelea kutumia gesi. Tuchukue hatua madhubuti za kuachana kabisa na matumizi ya kuni na mkaa,” amesema ACP Wambura.

Amebainisha kuwa tangu Desemba mwaka 2024, magereza yote nchini yameanza kutumia nishati safi, na kusisitiza kuwa nishati zisizo safi ni hatari kwa afya, zikiwemo kusababisha magonjwa ya mfumo wa hewa na saratani.

Naye, Mwakilishi wa Mkurugenzi Mkuu wa REA, Godfrey Chibulunje, amesema Wakala huo uliingia mkataba na Jeshi la Magereza Septemba 2024 wenye thamani ya Shilingi bilioni 35.23 kwa ajili ya kusambaza na kufunga miundombinu ya nishati safi ya kupikia kwenye magereza yote nchini.

“Kwa Mkoa wa Dodoma jumla ya majiko na mitungi 1,611 itatolewa kwa watumishi wa Jeshi la Magereza, ambapo Gereza la Isanga pekee limepokea seti 350 kwa ajili ya Maofisa na Askari wake,” amesema Chibulunje.

snapins-ai_3693999719500409408.jpeg
 
Pongezi baada ya kumshughulikia Lissu juzi mahakamani, Kidogo wamvunje kwa mara ya pili mzee wa watu.
 
Wanageuzwa wateja wa kudumu wa makampuni husika.
 
Back
Top Bottom