Dodoma: Sakata la Bosi wa UN kufukuzwa nchini latua bungeni

Ghazwat

JF-Expert Member
Oct 4, 2015
23,718
66,266
Sakata la kufukuzwa nchini kwa bosi wa Shirika la Maendeleo la Umoja wa Mataifa(UNDP) Tanzania, Awa Dabo, limetua bungeni

Mbunge wa Mbozi, Pascal Haonga wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) akizungumza bungeni leo, aliitaka Serikali kufafanua sababu za kumfukuza nchini Mkurugenzi Mkazi huyo wa UNDP Tanzania kwa kumpa saa 24

Hata hivyo, Mwenyekiti wa Bunge, Andrew Chenga aliliiambia Bunge kuwa Serikali ina mamlaka yote katika masuala ya Kidiplomasia na hivyo bunge haliwezi kuhoji sababu za mkurugenzi huyo kufukuzwa.
027b4e7f560cc12add21ab8b8c2fac51.jpg

Chanzo: Mwananchi
 
Kwa wanaojua makubaliano ya Vienna ( Vienna conversion) wala hawahitaji kuuliza swali la kijinga kama hili, sema tu ni kwa sababu ktk Taifa letu kila kitu kimegeuzwa siasa, watu tena Wabunge aidha hawajui nini maana ya Maslahi ya Taifa au wanajua lkn wanatumika na watu( Parliament capture). so sad yaani ila kwa wenye mapenzi mema na Taifa letu pamoja na hali kuwa mbaya tuendelee kuliombea...Mungu Ibariki Tanzania
 
Unatutusi wajinga ilhali mnaojua kiini cha ndani ni wachache ila mkatumia vyombo vya habari kutangaza kufukuzwa kwake,,,,, kwa nini mambo mengine msifanye kimya kimya? Very disgusting kind of administration!!!!!
 
Yaani wabunge wetu wanapenda vitu vya umbea umbea na maneno ya mtaani!wabadilike kwa kweli
Kutwa wanaongelea mambo ya dar es salaa.Ukiangalia sehemu kubwa za wanaojadili hasa wabunge wa UKAWA sehemu kubwa ni matukio ya kudakia dakia yanayojitokeza dar esalaam .Huu ni ushahidi kuwa huwa wanaenda bungeni wakiwa hawajajiandaa kabisa.Wanasubiri mtani wangu Mange kimambi aandike kWENYE ukurasa wake ndio wadakie na kufanya hoja bungeni.Mkuu INAUMA SANA wabunge wa upinzani wanaishi kwa hoja za kuokoteza mitandaoni na matukio yanayojitokeza tu hapa na pale hawaendi bungeni wakiwa wamejiandaa kwa hoja walizotoka nazo majimboni kwao wwalizokabidhiwa na wananchi wao.Mbunge makini hawezi simama na kuanza kuongelea mambo ya umoja wa mataifa wakati kwake wananchi wake wako hoi bin taabani.Ubunge wa upinzani ni sifuri,Hakuna wapinzani nchi hii.Shame on them.
 
Back
Top Bottom