Dodoma: Rais Magufuli atembelea eneo la ujenzi wa Ikulu Chamwino

figganigga

JF-Expert Member
Oct 17, 2010
25,658
55,485
RAIS DKT.JOHN POMBE MAGUFULI ATEMBELEA ENEO LA UJENZI WA IKULU CHAMWINO MKOANI DODOMA MARCH 16,2017
1-7.jpg

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. John Pombe Magufuli akiwa na Waziri Mkuu Kassim Majaliwa pamoja na Katibu Mkuu Kiongozi Balozi John Kijazi wakimsikiliza Mtendaji Mkuu wa Wakala wa Majengo nchini (TBA) Elius Mwakalinga kuhusu kazi za ufyatuaji wa Matofali yatakayotumika katika ujenzi wa Ikulu Chamwino mkoani Dodoma
2-7.jpg

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. John Pombe Magufuli pamoja na Waziri Mkuu Kassim Majaliwa wakikagua matofali yaliyokatika hatua ya Ukomazaji katika maji.
11-4.jpg

5-5.jpg

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. John Pombe Magufuli pamoja na Waziri Mkuu Kassim Majaliwa wakikagua matofali ambayo yameshakuwa tayari kwa ajili ya ujenzi wa majengo ya Ikulu Chamwino mkoani Dodoma.
7-4.jpg

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. John Pombe Magufuli akibeba moja ya tofali mara baada ya kukagua matofali yatakayotumika katika ujenzi wa Ikulu, Chamwino mkoani Dodoma.
4-5.jpg

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. John Pombe Magufuli akizungumza na vijana wanaoshiriki katika kazi za kubeba matofali katika eneo hilo la ufyatuaji wa matofali, Chamwino mkoani Dodoma.
6-5.jpg

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. John Pombe Magufuli akikagua moja ya matofali yatakayotumika katika ujenzi wa Ikulu, Chamwino mkoani Dodoma, huku Waziri Mkuu Kassim Majaliwa akiangalia March 16,2017
9-2.jpg
12-4.jpg

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. John Pombe Magufuli akiwa pamoja na Waziri Mkuu Kassim Majaliwa wakishiriki katika kazi za ufyatuaji wa Matofali yatakayotumika katika ujenzi wa Ikulu, Chamwino mkoani Dodoma

=======

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. John Pombe Magufuli leo tarehe 16 Machi, 2017 ametembelea eneo la ujenzi wa Ikulu Chamwino Mkoani Dodoma na kuwahakikishia wananchi kuwa atahamia Dodoma hivi karibuni kama alivyoahidi.

Mhe. Rais Magufuli ambaye ameongozana na Waziri Mkuu Mhe. Kassim Majaliwa Majaliwa, Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu Sera, Bunge, Kazi, Vijana, Ajira na Wenye Ulemavu Mhe. Jenister Joakim Mhagama na Katibu Mkuu Kiongozi Balozi John Kijazi amesema pamoja na majengo ya Ikulu Serikali itajenga miundombinu mingine zikiwemo reli na barabara za lami zitakazounganisha maeneo ya vijiji vinavyozunguka Ikulu na mji wa Serikali.

Pia Mhe. Dkt. Magufuli amewahakikishia wananchi kuwa wote watakaoguswa na shughuli za ujenzi wa miundombinu ya Serikali na wanaostahili kulipwa fidia watalipwa, na ametoa wito kwa wananchi hao kutumia fedha za fidia watakazolipwa kujenga makazi bora na kujipanga kufanya shughuli zenye manufaa kwao.

“Hapa sasa watakuja watu wengi, wafanyakazi na wageni maana tayari Mabalozi wa nchi mbalimbali nao watajenga ofisi zao hapa, sasa na nyinyi mjipange kufanya biashara, mtapata soko la kuuza mazao na bidhaa nyingine, mkipata fedha ziwasaidie kwa manufaa na sio kuzichezea” amesisitiza Mhe. Rais Magufuli.

Kwa upande wake Waziri Mkuu Mhe. Kassim Majaliwa Majaliwa amesema utekelezaji wa Serikali kuhamia Dodoma unakwenda vizuri ambapo mpaka sasa viongozi wakuu wa wizara zote na wafanyakazi 2,069 wameshahamia Dodoma na wengine wanaendelea kuhamia Dodoma.

Mhe. Majaliwa ameongeza kuwa atasimamia utekelezaji wa maagizo ya Mhe. Rais Magufuli aliyeagiza kujengwa kwa reli itakayounganisha eneo la Bwigili na Dodoma mjini ili kurahisisha usafiri wa watu pamoja na kuharakisha ujenzi wa barabara za kuzunguka mji wa Dodoma na barabara za kuunganisha mji wa Serikali na Dodoma Mjini.

Wakiwa katika eneo hilo, Mhe. Rais Magufuli na Waziri Mkuu Mhe. Majaliwa wameshiriki ufyatuaji wa matofari yatakayotumia katika ujenzi wa majengo ya Ikulu.

Mapema kabla ya kutembelea eneo hilo, Mhe. Rais Magufuli amepokea taarifa ya mapendekezo ya ujenzi wa Mji wa Serikali wa Makao Makuu Dodoma kutoka kwa Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Ustawishaji Makao Makuu Mhandisi Paskasi Muragili na kuagiza ujenzi wa Mji huo uzingatie maslai ya Taifa.

Gerson Msigwa

Mkurugenzi wa Mawasiliano ya Rais, IKULU

Chamwino

16 Machi, 2017
 
Hili swala la kuhamia Dodoma ni mojawapo ya mambo ambayo huwa nayachukua kwa sura mbili:

Sura ya kwanza ni kumkubali Rais Magufuli kwa ujasiri wa kusimamia jambo na kulitekeleza

Na sura ya pili ni utaratibu wake wa kutoka nje ya vipaumbele vilivyomo katika bajeti iliyondaliwa na serikali yake na kuidhinishwa na bunge letu.

Najua huu mtazamo hautakidhi upande wowote ila ndio la moyo wangu!
 
Kuna sababu tatu zinazofanya Serikali nyingi za Afrika kushindwa kuleta maendeleo
1.kutokuwa na mpango wa maendeleo
2.kuwa na mpango na kisha kuamua kutoutekeleza
3.kufanya kilicho nje ya mipango

Hili swala la kuhamia Dodoma ni mojawapo ya mambo ambayo huwa nayachukua kwa sura mbili:

Sura ya kwanza ni kumkubali Rais Magufuli kwa ujasiri wa kusimamia jambo na kulitekeleza

Na sura ya pili ni utaratibu wake wa kutoka nje ya vipaumbele vilivyomo katika bajeti iliyondaliwa na serikali yake na kuidhinishwa na bunge letu.

Najua huu mtazamo hautakidhi upande wowote ila ndio la moyo wangu!
 
RAIS DKT.JOHN POMBE MAGUFULI ATEMBELEA ENEO LA UJENZI WA IKULU CHAMWINO MKOANI DODOMA MARCH 16,2017
View attachment 481807
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. John Pombe Magufuli akiwa na Waziri Mkuu Kassim Majaliwa pamoja na Katibu Mkuu Kiongozi Balozi John Kijazi wakimsikiliza Mtendaji Mkuu wa Wakala wa Majengo nchini (TBA) Elius Mwakalinga kuhusu kazi za ufyatuaji wa Matofali yatakayotumika katika ujenzi wa Ikulu Chamwino mkoani Dodoma
View attachment 481806
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. John Pombe Magufuli pamoja na Waziri Mkuu Kassim Majaliwa wakikagua matofali yaliyokatika hatua ya Ukomazaji katika maji.
View attachment 481800
View attachment 481805
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. John Pombe Magufuli pamoja na Waziri Mkuu Kassim Majaliwa wakikagua matofali ambayo yameshakuwa tayari kwa ajili ya ujenzi wa majengo ya Ikulu Chamwino mkoani Dodoma.
View attachment 481804
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. John Pombe Magufuli akibeba moja ya tofali mara baada ya kukagua matofali yatakayotumika katika ujenzi wa Ikulu, Chamwino mkoani Dodoma.
View attachment 481803
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. John Pombe Magufuli akizungumza na vijana wanaoshiriki katika kazi za kubeba matofali katika eneo hilo la ufyatuaji wa matofali, Chamwino mkoani Dodoma.
View attachment 481810
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. John Pombe Magufuli akikagua moja ya matofali yatakayotumika katika ujenzi wa Ikulu, Chamwino mkoani Dodoma, huku Waziri Mkuu Kassim Majaliwa akiangalia March 16,2017
View attachment 481802 View attachment 481801
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. John Pombe Magufuli akiwa pamoja na Waziri Mkuu Kassim Majaliwa wakishiriki katika kazi za ufyatuaji wa Matofali yatakayotumika katika ujenzi wa Ikulu, Chamwino mkoani Dodoma

=======

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. John Pombe Magufuli leo tarehe 16 Machi, 2017 ametembelea eneo la ujenzi wa Ikulu Chamwino Mkoani Dodoma na kuwahakikishia wananchi kuwa atahamia Dodoma hivi karibuni kama alivyoahidi.

Mhe. Rais Magufuli ambaye ameongozana na Waziri Mkuu Mhe. Kassim Majaliwa Majaliwa, Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu Sera, Bunge, Kazi, Vijana, Ajira na Wenye Ulemavu Mhe. Jenister Joakim Mhagama na Katibu Mkuu Kiongozi Balozi John Kijazi amesema pamoja na majengo ya Ikulu Serikali itajenga miundombinu mingine zikiwemo reli na barabara za lami zitakazounganisha maeneo ya vijiji vinavyozunguka Ikulu na mji wa Serikali.

Pia Mhe. Dkt. Magufuli amewahakikishia wananchi kuwa wote watakaoguswa na shughuli za ujenzi wa miundombinu ya Serikali na wanaostahili kulipwa fidia watalipwa, na ametoa wito kwa wananchi hao kutumia fedha za fidia watakazolipwa kujenga makazi bora na kujipanga kufanya shughuli zenye manufaa kwao.

“Hapa sasa watakuja watu wengi, wafanyakazi na wageni maana tayari Mabalozi wa nchi mbalimbali nao watajenga ofisi zao hapa, sasa na nyinyi mjipange kufanya biashara, mtapata soko la kuuza mazao na bidhaa nyingine, mkipata fedha ziwasaidie kwa manufaa na sio kuzichezea” amesisitiza Mhe. Rais Magufuli.

Kwa upande wake Waziri Mkuu Mhe. Kassim Majaliwa Majaliwa amesema utekelezaji wa Serikali kuhamia Dodoma unakwenda vizuri ambapo mpaka sasa viongozi wakuu wa wizara zote na wafanyakazi 2,069 wameshahamia Dodoma na wengine wanaendelea kuhamia Dodoma.

Mhe. Majaliwa ameongeza kuwa atasimamia utekelezaji wa maagizo ya Mhe. Rais Magufuli aliyeagiza kujengwa kwa reli itakayounganisha eneo la Bwigili na Dodoma mjini ili kurahisisha usafiri wa watu pamoja na kuharakisha ujenzi wa barabara za kuzunguka mji wa Dodoma na barabara za kuunganisha mji wa Serikali na Dodoma Mjini.

Wakiwa katika eneo hilo, Mhe. Rais Magufuli na Waziri Mkuu Mhe. Majaliwa wameshiriki ufyatuaji wa matofari yatakayotumia katika ujenzi wa majengo ya Ikulu.

Mapema kabla ya kutembelea eneo hilo, Mhe. Rais Magufuli amepokea taarifa ya mapendekezo ya ujenzi wa Mji wa Serikali wa Makao Makuu Dodoma kutoka kwa Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Ustawishaji Makao Makuu Mhandisi Paskasi Muragili na kuagiza ujenzi wa Mji huo uzingatie maslai ya Taifa.

Gerson Msigwa

Mkurugenzi wa Mawasiliano ya Rais, IKULU

Chamwino

16 Machi, 2017
Loading......
 
Huyu kila siku ni majengo tu!!Anaona ni bora kugharamia majengo kuliko kuongeza mishahara ya watumishi,kutoa mikopo kwa wanafunzi,n.k.

Huyu mtu hajali mateso ya wananchi anachojali ni yeye akumbukwe kwa kusimamisha majengo kila mahali anapoamua hata kama sio ya lazima kwa sasa!!
 
Hili swala la kuhamia Dodoma ni mojawapo ya mambo ambayo huwa nayachukua kwa sura mbili:

Sura ya kwanza ni kumkubali Rais Magufuli kwa ujasiri wa kusimamia jambo na kulitekeleza

Na sura ya pili ni utaratibu wake wa kutoka nje ya vipaumbele vilivyomo katika bajeti iliyondaliwa na serikali yake na kuidhinishwa na bunge letu.

Najua huu mtazamo hautakidhi upande wowote ila ndio la moyo wangu!

Ni nadharia yako tu, hata kama ingekuwa kwenye budget, bado vipaumbele vingi tu vingebaki pending, scarceness haiepukikagi, hata wewe, nahisi umepanga nyumba ukaaamua kujenga ya kwako, kuna vitu utajinyima tu, hata kama ussubiri aje, labda uamue kufa bila kuwa na kwako, sasa tatizo la nchi kama Tz haina kifo, tutakufa tutaiacha, wakija viongozi wengine wenye mindset kama yako tutajikuta hadi vitukuu vya vitukuu wetu bado hawajaamia dodoma na bado vipaumbele vitaendelea kuwepo. So we need bold minds like our president's. Ili hizi hatua ngumu zipigwe mbele.

Therefore sura ya kwanza ilitoka rohoni mwako, ulikuwa sawa kabisa, sura ya pili ikakujia kutokea akilini, that's doubting, kama inavyokuwa kwa binadamu wengi wetu, HOFU, ni kitu mbaya sana.

Henceforth, heko kwako raisi Magufuli, sane people can see through.
 
Back
Top Bottom