VUTA-NKUVUTE
JF-Expert Member
- Nov 25, 2010
- 6,136
- 17,871
Kesho, mnamo tarehe 31/1/2017, wabunge watatu wa kuteuliwa na Rais: Prof. Palamagamba Kabudi, Abdallah Bulembo na Anne Kilango Malecela wataapishwa kuwa Wabunge wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.
Kati ya hao, Prof. Kabudi anatabiriwa kuchomoza kwenye Baraza la Mawaziri linalotarajiwa kufanyiwa mabadiliko hivi karibuni. Nguli huyo wa Sheria za Katiba anatajwa kupewa Wizara ya Maliasili na Utalii au Uchukuzi au Katiba na Sheria.
Maandalizi yote ya kuapishwa kwa Wabunge hao na kuanza kwa vikao vya Bunge yamekamilika. Inasubiriwa kesho na anasubiriwa Rais Magufuli arudi kutoka Adis Ababa, Ethiopia kwenye mkutano wa Umoja wa Afrika (UA). Mabadiliko yamekaribia mno,kaeni chonjo.
Mwafaaa!
Mzee Tupatupa wa Lumumba (kwasasa Dodoma)