Dodoma: Msanii Chidi Benz akamatwa akiwa na dawa za kulevya. Hii ni mara ya tatu kukamatwa

mwanamwana

JF-Expert Member
Aug 1, 2011
1,076
4,113
Msanii wa Hip Hop nchini Rashid Makwiro 'Chid Benz anashikiliwa tena na jeshi la polisi mkoani Dodoma kwa tuhuma za kukutwa na dawa za kulevya na hii inakuwa mara ya tatu kwa msanii huyu kukumbwa na sakata hili.

Akithibitisha taarifa hizo Kamanda wa Polisi wa Mkoa wa Dodoma, SACP, Giless Muroto amesema kwamba ni kweli msanii huyo alikamatwa na taarifa kamili zitatolewa hapo kesho.

Kamanda Muroto amesema "Ni kweli Chidi Benz mnamo tar 30/12/2017, tulimkamata akiwa yeye na mke wake na vijana wawili. Tumemkamata akiwa na dawa za kulevya zidhaniwayo kuwa ni Heroine. jalada lake lipo tayari kwa Mwanasheria wa wa serikali linafanyiwa uchunguzi na muda wowote watapelekwa mahakamani"

Aidha ameongza kuwa watuhumiwa wote bado wako mahabusu.

Ucha Uchuro kijana Jana tu nilikuanae Chid beenz chuma sehemu Fulani tunapata Mvinyo.
 
Kama alikuwa anayauza ni sawa kumshikilia na kumpeleka mahabusu

Nje ya hapo ni kiki tu polisi wa Dodoma wanatafuta
 
Msanii wa Hip Hop nchini Rashid Makwiro 'Chid Benz anashikiliwa tena na jeshi la polisi mkoani Dodoma kwa tuhuma za kukutwa na dawa za kulevya na hii inakuwa mara ya tatu kwa msanii huyu kukumbwa na sakata hili.

Akithibitisha taarifa hizo Kamanda wa Polisi wa Mkoa wa Dodoma, SACP, Giless Muroto amesema kwamba ni kweli msanii huyo alikamatwa na taarifa kamili zitatolewa hapo kesho.

Kamanda Muroto amesema "Ni kweli Chidi Benz mnamo tar 30/12/2017, tulimkamata akiwa yeye na mke wake na vijana wawili. Tumemkamata akiwa na dawa za kulevya zidhaniwayo kuwa ni Heroine. jalada lake lipo tayari kwa Mwanasheria wa wa serikali linafanyiwa uchunguzi na muda wowote watapelekwa mahakamani"

Aidha ameongza kuwa watuhumiwa wote bado wako mahabusu.

Msikilize hapa chini Kamanda Muroto akifafanua zaidi

RPC-DODOMA.jpg

Chanzo: EATV
 
Duuuh, namkubal sana chidi Benz lkn ameshindwa kuachana na madawa ya kulevya.Naomba Mungu amjalie aachane nayo maana bado anahitajika kutoa track kali zaidi za hip hop ! King"""" kongggggg""" ......
 
Madawa ukishaonja kutoka ni bahati sana, wengi hawatoki hadi wanakufa. Huyu jamaa juzijuzi alikuja na kiki za kuacha kwenye media leo karudi tena. Tatizo ana company mbaya, hata huyo sijui mke wake na watu wanaomzunguka, akitaka kuacha inabidi akae nao mbali kabisa akae na watu wapya kama miaka kadhaa maana waliomzunguka wanamchekea tu.
 
Dsm bila King kongggg.......

Dsm bila chumaaaa......

anyway kama wanamshika lakini waliompa mzigo hawajulikani raia tufanyaje,?
 
Back
Top Bottom