Francis12
JF-Expert Member
- Sep 30, 2016
- 7,533
- 22,278
Mbunge wa Jimbo la Hai Freeman Mbowe anazungumza na waandishi wa habari mjini Dodoma hivi sasa.
Freeman Mbowe amesema hatafika polisi kwa kuitwa na Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Paul Makonda. Amekanusha vikali tuhuma za kuhusika na biashara au kutumia madawa ya kulevya.
Anasema wao kama chama wanaunga mkono jitihada za mapambano dhidi ya dawa za kulevya na serikali imechelewa kuendesha vita hiyo.
Asema CHADEMA na kambi ya upinzani kwa ujumla haiungi mkono mapambano hayo yanayoendeshwa kwa hila.
''Makonda hana mamlaka ya kumpa wito mtu kwenda polisi kwa mujibu wa sheria ya serikali za mitaa. Makonda amenichafulia jina langu, chama, familia na upinzani.”
Anasema RC anachofanya ni kuwaepusha watuhumiwa wa dawa za kulevya na mkono wa sheria. Anasema atamfungulia mashitaka ya kumchafulia jina lake kwa kumhusisha na biashara ya dawa za kulevya.
Anasema yupo tayari kutoa ushirikiano wakati wowote endapo njia sahihi zitatumika.