Dodoma kuna matatizo

Manyerere Jackton

JF-Expert Member
Dec 11, 2012
2,436
4,430
Ndugu zangu, niliposhuhudia wale vijana 10,800 walipambana kupita kwenye mchujo wa nafasi 70 za Idara ya Uhamiaji, nilipatwa na simanzi kubwa sana. Ilikuwa simanzi ya ukosefu wa ajira kwa vijana.
Pamoja na ukweli huo, inaelekea, ama halmashauri zetu, au Jeshi letu la Polisi halijatambua kadhia hii ambayo kwa kweli ni bomu linalosubiri kulipuka.
Hapa Dodoma kuna tatizo moja la ajabu sana, na yawezekana lipo katika miji mingi. Vijana wengi wameamua kujiajiri kwa kuuza kuku, mishikaki na vyakula mbalimbali nyakati za jioni. Wanatumia fursa ya wingi wa wageni hapa Dodoma kujipatia riziki kwa njia halali kabisa. Jambo la kusitisha ni kuona Polisi wamegeuza vijana hawa kuwa mradi wao. Wanapita kwenye vibanda kuanzia saa 5 usiku na kuamuru wafunge. Mali za vijana zinaporwa na wengine wanalazimika kutoa pesa ili waachwe.
Hii sheria ya kuamuru watu walale saa 5 katika nchi iliyo huru ina maana gani? Je, hii ndiyo mbinu ya kupambana na majambazi? Iweje ujambazi wa hatari uwe wa usiku, lakini wa mchana mitaani na katika benki usiwe tishio? Je, ni halali kumpangia mtu huru muda wa kufurahi hasa kama kazi zake ni za mchana? Pamoja na hoja yangu ya kupinga ulevi uliopindukia, bado naamini Polisi na Halmashauri wanapaswa kutumia busara kuhakikisha watu huru wanabaki kuwa huru kufurahia uhuru wao, alimradi tu uhuru huo usivuruge taratibu na sheria halali za nchi.

Vijana wa Dodoma na miji mingine nchini waachwe wauze chips, kuku, mishikaki na vyakula vingine kwa muda wanaoona unafaa. Nchi haiwezi kuendelea kwa kuwalazimisha watu kulala saa 5 usiku. Kampala sehemu za vyakula na maduka hazina muda wa kufungwa, kwanini manufaa hayo yasiwe hapa kwetu Tanzania?
 
hebu tuachane na kampala, kwani sheria ya hapa tanzania inasema sehemu kama hizo zinatakiwa zifungwe saa ngapi??

Ni ukweli usiopingika nchi yetu inaendeshwa kwa matukio, maadamu limesikika kwa jirani mara moja nao wanalichukua bila kufanya uchunguzi wa kujua chanzo! Je, wajibu wa majeshi yetu ni nini? Je, ile Intelijensia iliyokuwa inasifika nchini ipo likizo? Je, kweli tupo huru na amani nchini? Je, hilo group la vijana waliokuwa uwanja wa taifa likaamua tofauti kuna atakayelizuia kirahisi? Mungu atusaidie na kuwafunulia viongozi wenye mamlaka maono mema kwa jamii!
 
Nadhani haya mambo hayatakiwi kuwa adressed kwa ujumla wake! !!!!

Badala ya kusema mkoa wa Dodoma ni bora kuuliza mwenye mamlaka yaani mkuu wa mkoa ,mkuu wa wilaya na RPC
kama hiyo sheria ni ya Dodoma pekee!!!!????

Wanasheria hebu mtujuze tafadhali
 
Manyerere huwa unakuwaga na mada nzuri na nzito ila huwa unakosaga wachangiaji kutokana na jinsi unavyo andikaga heading zako. Kwa habari kama hii ungeweza kuandika "Curfew yatangazwa huko Dodoma, hali ni mbaya..!!" japo si kweli exactly ila mtu akiingia si atapata ukweli na atachangia. Kwanza hapo yaan 60% ya watakaoingia watataka kujua hilo neno 'curfew' maana yake nini kwanza.., mpaka hapo ni views tayari..
 
Back
Top Bottom