VUTA-NKUVUTE
JF-Expert Member
- Nov 25, 2010
- 6,136
- 17,871
Wanachama na wajumbe wa Baraza la Vijana la CHADEMA (BAVICHA) wanawasili hapa Dodoma tayari kwa Julai 23. Taarifa zilizopo zinaonesha kuwa wanachama wa BAVICHA wanawasili hapa kama wasafiri wa kawaida,huku wengine wakiongozana na vijana wa CCM almaarufu kama UVCCM.
Tarehe 23 mwezi huu,kutafanyika mkutano mkuu wa taifa wa CCM hapa Dodoma kumkabidhi uenyekiti wa CCM Taifa Rais J. P. Magufuli. Kufuatia kuwekwa katazo la mikutano ya kisiasa nchini na uwepo wa mkutano wa CCM,BAVICHA wamedhamiria kuwepo hapa Dodoma 'kulisaidia Jeshi la Polisi kuzuia mkutano huo wa CCM'.
Natoa wito kwa Jeshi la polisi Tanzania kueleza vyema mantiki ya zuio lao ili kuondoa sintofahamu ya kisiasa iliyopo na ile ya Julai 23. Eid Mubarak!
Mzee Tupatupa wa Lumumba (kwasasa Dodoma)