Dkt. Tulia tunakutakia heri, kinyang'anyiro cha Uspika

masopakyindi

Platinum Member
Jul 5, 2011
17,002
11,687
Kwanza nakishukuru chama changu, CCM kwa kumteua kijana wetu, Dr Tulia katika kinyang'anyiro cha Uspika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.

Nina sababu kuu mbili:
Sababu ya kwanza ni kwamba Dr Tulia ana uzoefu sasa wa kuliendesha vyema bunge kwa manufaa ya maendeleo ya nchi.

Sababu ya pili, kuipongeza CCM kwa kuona mbali ambapo ililipoteza jimbo la Mbeya kimakusudi kabisa miaka ya 2005-2010.

Sina haja ya kurudia mchafuko ndani ya CCM, na hasa CCM mkoani Mbeya wakati huo uliosababisha vijana wengi kukimbilia upinzani.

Kutoka kipindi hicho maendeleo ya Mbeya yalisuasua sana na kwa kipindi kirefu. Ni matumaini ya wana Mbeya kuwa uteuzi wa Dkt. Tulia hatimaye ikiwa atashinda kiti cha Uspika,utaleta focus kwa mambo mengi yaliyo achwa na kudorora.

Cha muhimu zaidi nampongeza Dkt. Tulia kwa kuteuliwa kugombea kiti cha Uspika, sisi wana Mbeya tuna imani naye kuendesha vyema majukumu yake.
 

MKANDAHARI

JF-Expert Member
Apr 7, 2011
4,940
5,460
Kwani anashindana na nani kwenye hicho kinyang'anyiro unachosema hapa? Hivi mataga nani aliewaloga?
 

Behaviourist

JF-Expert Member
Apr 8, 2016
38,833
92,452
Naibu Speaker ambae alikuwa anazuia masuala ya ufisadi kujadiliwa Bungeni hafai kuwa Speaker wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.
 

Lutifya

JF-Expert Member
Jan 6, 2011
1,962
2,953
Tuna Bunge Tanzania?. Letu siyo Bunge bali Rubber stamp ya kupitisha matakwa ya Serikali ya CCM
 
2 Reactions
Reply
Top Bottom