Dkt. Slaa: Ninapokubaliana na kutofautiana na Magufuli

KATIKA kitabu 'Tujisahihishe' kilichoandikwa na Baba wa Taifa, Mwalimu Julius Nyerere mwaka 1962 ukurasa wa pili, anaeleza dhana nzima kuhusu ukweli.

Anasema, “Ukweli una tabia moja nzuri sana. Haujali mkubwa wala mdogo, haujali adui au rafiki wote kwake ni sawa. Pia ukweli una tabia ya kujilipiza kisasi kama ukipuuzwa.

“Ukiona nataka kulipiga teke jiwe kwa kuwa nafikiri kuwa ni dongo au mpira, natumaini utanionya.

“Lakini nikilipuuza onyo lako kwa sababu eti wewe ni mdogo au kwa sababu sikupendi, nikalipiga teke, basi litanivunja dole, japo ningekuwa nani.

“Ukweli haupendi kupuuzwa puuzwa! Wakati mwingine mtu tunayempinga huwa ana makosa kweli, lakini hoja tunazozitoa ni za kinafsi na hazihusiani kabisa na hoja zake.

“Nikisema mbili na tatu ni sita nakosa. Lakini ni bora kunionyesha kwamba pengine nafikiri tunazidisha kumbe tunajumlisha.

“Ni kweli mbili mara tatu ni sita, lakini mbili na tatu ni tano, siyo sita.

“Lakini ukijaribu kuwashawishi wenzetu wakatae mawazo yangu na kukubali yako kwa kusema meno yangu ni machafu, au natoa kamasi daima, utakuwa unatumia hoja ambazo hazina maana.

“Huu ni mfano wa upuuzi, lakini mara nyingi hoja tunazotumia kuwashawishi watu wakatae mawazo ya wale tusiowapenda, au kukubali mawazo yetu, huwa hazihusiana kabisa na mambo tunayojadili,” anasema Mwalimu katika kitabu chake hicho.

Kwa kutumia angalizo la Mwl. Nyerere, baadhi ya watu badala ya kumpinga Mzee Slaa kwa kutumia nguvu za hoja, watakachofanya ni kuandika kejeli na matusi.
Dude DR Silaa,ni mwana siasa,anaongea mawazo yake,kwakuwa saahizi hata angekuja nani aseme yanayotendeka
nchini tanzania,hakutaleta mabadiliko yoyote,kwani wameanza leo kutoa hoja zao nzito na nuri,linapokuja swala
la siasa inabaki siasa,hakuna mabadiliko,nimesema Dr Silaa,ni mwanaa siasa,kwasababu niliwahi kumshauri mimi kama personlity akiwa highly elevated in the political platiform,2010,nikamwambia wajitahidi wapiganie mabadiliko ya tume huru ya uchaguzi ndipo angeshinda urais,akapuuza,katika uchaguzi ule upinzani ukashindwa,KWA SASA NCHI
hii itakuwa kama wakati wa SUELEMANI katika israeli,watu walitaka wapunguziwe kongwa zito alilowabebesha Daudi babake ,lakini yeye alisema ,mimi nitaongeza zaidi kongwa,baba yangu aliwapiga kwa mijeredi,LAKINI MIMI NITAWAPIGA KWA NGE,KWA MAANA IMEANDIKWA KIUNO CHA BABA YANGU NI KINENE KULIKO KIDOLE CHANGU CHA MWISHO,
soma ripoti hii KATIKA 2NYAKATI 10:11-12,MAANA YAKE kwa siasa nzuri za kina DR Silaa,zi sizo za kivitendo,kwamba watu mnaowaamini kuongoza mapambano YA MABADILIKO unakuta nao ni wapiga dili kwa rangi nyingine,
Wapo waliojaliwa kuongea na kutetea wasio weza kuongea ingawa wanaumia,lakini wapo kimya(awesome muted)
soma ripoti hii katika provebs 31:8-9 wenye uwezo wa kufungua kinywa kuongea kwajili ya bubu(wasio na uwezo kuzungumza)hukumu kwa Mungu itakuwa kali sana,
nao kumbe ni wapiga dili,hakuna
 
Huyu Dr pamoja nawakina Shigogo wakatutesa sanna during campaign period ....mwezio Shigogo ameokoka akabaki kidogo tu huyu padre atubu.
Nyie makada wa chadema na ccm ndio cancer ya maendeleo TZ


Mpo kwa interests zenu

Slaa
 
An
Mkuu barafu
Huwa ninakukubali kutokana na hoja zako kuwa balanced pamoja na kwamba kuna hoja zingine huwa tunapingana.

Umemuelezea Dkt. Slaa kwa jicho la mtazamo wangu.

Pamoja na mapungufu ya kibinadamu lakini Mzee Slaa aliendesha siasa za kujenga taifa.

Taifa limekosa mchango wake kisiasa lakini hatuwezi kumsahau kwa kile alikifanya kitaifa na hasa wakati akiwa mbunge. Ikumbukwe kuwa Kanuni za bunge zinazotumika kwa sasa ambazo zinatoa nguvu na uhuru mpana kwa wabunge ni matunda ya mchango wa Mzee Slaa.
Anayepingana na Dr Slaa ana yake....binafsi naona kama hyo mtu sio mzalendooo
 
Hii article itakuwa haijaandikwa na Dr. Slaa tunayemfahamu, maana imekaa kinafiki mno.
 
Kwa miaka yote niliyomfatilia huyu mzee nimegundua ili umuuelewe unahitaji akili fulani hivi ya ziada. Ukiikosa hiyo si ajabu sana kwa maamuzi yake yale ya kuiacha CDM/UKAWA kipindi kile ukamwita kila aina ya majina mabaya ila ki uhalisia huyu jamaa ni kichwa sana. Kwa namna ambavyo alimtaka Lowassa kwenye UKAWA ingekuwa kweli kaja kwa namna ile mi naamini leo tungekuwa tunaandika mengine. Tatizo hata wenzake kwenye uongozi CDM hawakumuelewa na ndio maana wakamchukua Lowassa ki juha namna ile
 
Pengo la Slaa ni pengo kuu lisilozibika,kila siku inajidhihirisha hivyo,huyu jamaa alifanya niamini there is light at the end of the tunnel katika upinzani,tofauti na ilivyo sasa.
Kwa sasa tuna Dkt. Mashinji mwenye mikakati ya kisiasa zaidi ya Dkt. Slaa!

Dkt. Slaa is from bygone era!(in CHADEMA fanatics voice)
 
Kwanini asianzishe chama chake au akatwe mkia?
Kitu gani kinakufanya mkapa udhani ni muhimu kuanzisha chama chake au akatwe mkia?

Kwa hiyo wale wote wanaoandika makala za kisiasa ni lazima waanzishe vyama vyao vya siasa.
 
Dundo_Boy,

Mzee Slaa alifanya aliyoweza na sasa ni zamu ya wengine kuendeleza alipoachia. Kumbuka idadi ya watu wakati Mzee Slaa anaondoka ubunge ilikuwa ni kidogo kulinganisha na sasa.

Hata mahitaji ya maji yameongezeka.
Leo lumumba ni watetezi wa Slaa!Mmeshasahau upadre wake!
 
Tatizo mnatoa Hoja na hamtaki mtazamo tofauti, watu hawapingi utendaji wanataka Raisi hawe msikivu na ajifunze kauli nzuri. Dr. Slaa anaandika kutoka wapi? Isijekuwa Canada na kama kunyosha nchi ni kuua biashara Zetu, kutumia polisi kutupiga faini za hovyo haki ya mungu na sie tutamnyoosha kwenye sanduku la kura. Hatuungi mkono kuwatolea maneno makali watu wa bukoba. Raisi Mwenye kiburi, visasi hatufai hata kama nia yake nzuri.
 
Soma article yote utafamu ni eneo gani hakubaliani na serikali.

Nimeirudia bado msimamo upo pale pale. Reli ni views zake.

Namjua Slaa ni mpigania haki na hapendi ufisadi na dhuluma yoyote. Msimamo huu amebaki nao katika maisha yake yote japo ulimgharimu sana siyo tu kwenye siasa bali hata alipokuwa kanisani.

Kama mwana falsafa ameeleza anayokubaliana na Magufuli kwa mtazamo chanya katika mtazamo hasi wa wengi na ninaamini wengi pia wamekubaliana na mawazo yake. Lakini pia Magufuli na raisi wa watanzania, wanaomkubali na wasiomkubali na anamapungufu yake ambayo ni ya kwake ya kuzaliwa, ya kiutamaduni, ya kujifunza na hata yale ya kisisiem. Dr Slaa aje tena aandike makala ya asiyo kubaliana na Magufuli kwa vile kwa kufanya hivyo tunashiriki moja kwa moja kwa uongozi wa nchi yetu.

Ninatamani niandike mengi lakini naomba ni reserve kwa sasa
 
Hizi ni hekaya wajinga tuliaminishwa na kuamini ili kuhalalisha maamuzi ya hovyo kupata kutokea ktk siasa za upinzani tz.

Rudia kuangalia alichoenda kukifanya Hotelini akiwa na Mwakyembe UTAJUA nini nasema.
 
Sehemu kubwa ya hoja ya Dr Slaa ni Propaganda zaidi.

Kwanza kuna tofauti ya yeye Slaa alipokuwa Mbunge Karatu, na raisi mtu ambaye Hazina iko chini yake!. Ukiwa Mbunge wewe kazi yako ni kupiga kelele serikali ikusikilize ifanye, lakini ukiwa Raisi wewe ndo una maamuzi ya mwisho pesa iende wapi na ifanye nini na lini!, kwa hiyo mfano wa Dr Slaa kuhusu Maji kule Karatu hauna mashiko!

Pili sijaona popote Slaa akizungumza kwa kina pale anapotofautiana na Magufuli, zaidi ya kamfano kamoja mfu kuhusu Reli Standarg Gauge, ambayo kimsingi mchakato ulianza katika serikali ya Kikwete. Najua Dr Slaa amekatupia haka ka mfano ili kubalance story yake asionekane mnazi!.

Kiufupi Slaa anatwambia anakubaliana na uminyaji wa Demokrasia nchini.

Slaa anatwambia anakubaliana na Ukamatwaji wa watu na kuwa harrassed kwa sheria kandamizi za mitandao.

Slaa anatwambia anakubaliana na matamko controversial, Uminywaji wa haki za Wazanzibari

Laiti Slaa kama hakubaliani nayo mbona hajasema kuwa hakubaliani nayo?
Nakuunga mkono. His analysis is biased. How about Zanzibar? Demokrasia nchini ikoje? Muingiliano wa kimajukumu ambao ni hatari sana ukoje? Au anafurahia "anaodhani ni maadui wake" kunyimwa uwanja sawa wa kisiasa? Naona uchambuzi wake umekosa uhalisia. Anamuunga mkono Ili kuwaumiza waliomweka pembeni. Labda baada ya Muda atapatiwa kazi
 
SLAA NI MZALENDO , ANAONGEA UKWELI TUPU ,WATANZANIA WANACHEZEA RAIS AMBAYE NI ZAWAI KUBWA TOKA KWA MUNGU BAADA YA KUTUONA TUMETESEKA MIAKA MINGI ,NI JAMBO LA MUDA TU BAADAYE MAMBO YATAKAA SAWA

Hizi sifa ulizomwaga hapa usithubutu kwenda kusema mbele ya wana Bukoba. Ni lini hiyo hali ya muda itatengamaa kwa hiyo watu wasubiri? Hivi mawaziri, wabunge, pamoja na rais mishahara yao na upendeleo mwingi umeshushushwa ili tuamini wote tuna hali mbaya ya muda? Wenzako wanakuimbisha ni suala la muda wao wanazidi kunawiri.
 
Haya MZEE, mbona pale tatizo la maji ni sugu au lilikuwa zaidi?. Pale Endallah kale kashule ka secondary pale juu mbona watoto wa kike wanashinda kule chini kuchimba masalia ya maji ya mvua?

Na kule Nina taarifa nyingi sana kwamba wanabakwa sana maana kuna siku pia napitaga hata saa mbili nakuta watoto wamevaa uniform wameinama kule!!!!!!!......inamaana maji hayakufika kwao?

Na mbona sisikiagi kesi ya ubakaji? Au nao watoto wanafurahia mahaba maana matukio ni mengi naishia kusikia kuwa wamemalizana! Na haijulikani wamemalizanaje?......maji pale hata PM juzijuzi amekiri pana tatizo na atasaidia kulitatua maana wageni toka nje ni wengi wanapenda kuzunguka zunguka vijijini humo. Maji KARATU bado ni Shida, tatueni kwa hawa watoto wa shule.

Maelezo hayo nitatafuta gazeti ili nisome vizuri maana hapa wala hata robo sijafika
Endalah wamechimbiwa maji ya magadi haijulikani hata kiwango cha fluoride na bado wanafurahia kama tunu! Karatu huko vijijini maji ni shida.
 
FB_IMG_1483627906216.jpg
 
Back
Top Bottom