Nguruvi3
Platinum Member
- Jun 21, 2010
- 15,407
- 31,391
Kwanza, ningeomba mtu anionyeshe wapi Dr Slaa hakubaliani na Magufuli?
Kujenga std gauge na electrification ni kitu kimoja katika hatua tofauti, si tofauti ya suala zima
Pili,aliyeoeleza Dr, sioni ambalo Watanzania wanakataa. Ufisadi, ufujaji, ubadhirifu , vitu hewa n.k.
Watanzania hawakubaliani na kutumia mambo hayo 'kinafiki' kwasababu za kisiasa
i) Mikutano ya hadhara iliyopo kikatiba inaingilia vipi na ufisadi, ubadhirifu na vitu hewa?
ii) Kuondoa bunge live kuna mahusiano gani na mambo maovu yanayopigwa vita?
iii) Kuminya vyombo vya habari kunamsaidiaje kujua hali ya nchi na yatokanyo?
vi)Kufuatilia watoa habari katika mitandao kunaendaje sambamba na vita ya maovu?
v) Dr anakubaliana na ukiukwaji wa haki tunaouona nchini?
vi) Kufutwa mchakato wa katiba kunatusaidiaje kutengeneza mfumo wa kujiendesha?
Kwa miaka kadhaa tumekuwa na Dr Slaa jamvini.
Akiwa mwanasiasa tulimwambia hatuhitaji mtu wa kutenda yote kama mtu binafsi.
Tunahitaji mtu wa kusimamia urekebishaji wa mifumo yetu inayotukwamisha
Hatua za mtu mmoja siyo sustainable.
Yote aliyosimamia Rais kama usafi wa maeneo hayakuwa sustainable na leo ni historia.
Ndivyo ilivyokuwa safari za magari ambazo zimeisha na sasa ni uwanja wa ndege
Sherehe tulizoambiwa zinagharimu sasa ni mapambo makubwa yakinogeshwa zaidi
Haya hayatokei kwa bahati mbaya , yanatokea kwasababu nchi ni ya watu na jitihada za pamoja zinatakiwa. Ingalikuwa si hivyo leo tusingerudi kule tulikotoka
Ningemwelewa Dr Slaa kama angezungumzia kufutwa kwa mchakato wa katiba.
Hili ni jambo alilosimamia kwa nguvu zake ingawa leo haoni umhimu wake