PostGE2025 Dkt. Rioba wa TBC: Niko tayari kuomba silaha kulinda Taifa langu dhidi ya tishio lolote la usalama na amani ya Tanzania

Conversations and stories after Tanzania's 2025 General Elections

Just Pray

JF-Expert Member
Joined
Nov 7, 2023
Posts
2,142
Reaction score
4,777
Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Utangazaji Tanzania (TBC) Dkt. Ayub Rioba Chacha kupitia ukurasa wake kwenye mtandao wa Facebook amesema yupo tayari kuomba silaha kwaajili ya kuilinda Tanzania dhidi ya tishio lolote la usalama na amani kwani aliwahi kufanya hivyo mwaka 1990.

"Mwaka 1990 nikiwa JKT, Chimala, Mbeya, nilikaa miezi 3 nikiwa na bunduki kulinda madaraja ya reli na barabara pale dhidi ya tishio la makaburu wa Afrika Kusini. Leo hii niko tayari kuomba silaha kulinda Taifa langu dhidi ya tishio lolote la usalama na amani ya Tanzania kutoka kwa maadui wa sasa, ambao sisi wengine tunawajua!"


 
MANENO YA MWANAMABADILIKO YALIYO TOFAUTI NA CHAWA RIOBA WA TBC

Nukuu:
"Maneno matupu ya kumkera mkoloni (mweusi) bila ushiriki katika harakati za mapambano kwa vitendo hayaweze kutokomeza Ukoloni mkongwe na ubeberu (imperialism) wa chama dola kongwe haramu " - Amilcar Cabral

"We are not going to eliminate imperialism by shouting insults at it." ~ Amilcar Cabral

Picha : Amilcar Cabral akiongoza mapambano Guine Bissau dhidi ya ukoloni mkongwe wa Kireno.
Image and article courtesy of Mshana Jr : Africa history made (Marejeo)

 
Tanzania kutoka kwa maadui wa sasa, ambao sisi wengine tunawajua!"

Rioba GenZ hawana chama wala kiongozi, bali ni movement yaani vuguvugu

TOKA MAKTABA:

Mkuu wa Idara ya Habari CHADEMA akiwa uhamishoni azungumza mazito


View: https://m.youtube.com/watch?v=tkHzeukGufk
Katika mahojiano haya exclusive ya kipekee, mwanahabari mpekuzi Francis Ontomwa anaongea na kada wa CHADEMA kamanda Gerva Lyenda, Mkuu wa Idara ya Habari wa CHADEMA, ambaye anakanusha madai kwamba chama hicho kinafadhili maandamano ya Desemba 9,2025 na kuieleza dunia hali halisi ya kisiasa, kiusalama na kijamii ilivyo chini ya utawala wa Samia Suluhu Hassan..
 
Kwa hiyo Makaburu walikuwa wanatoka South Kuja Kuiba Vyuma chakavu Mbeya?
 
Kwani Kuna vita? Maandamano ni ya amani
 
Akalinde tbc,kwa sababu hatutaki ulinzi wake wakinafiki.
 
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…