Waufukweni
JF-Expert Member
- May 16, 2024
- 4,393
- 14,500
Katibu Mkuu wa Chama cha Mapinduzi (CCM), Balozi Dkt. Emmanuel Nchimbi, amewataka watendaji wa chama hicho kuhakikisha wanatekeleza mambo yanayojibu changamoto za wananchi, akisisitiza kuwa CCM si chama cha viongozi bali ni cha wanachama wa kawaida.
Dkt. Nchimbi ametoa maagizo hayo akiwa wilayani Mbinga, alikosimama kusalimiana na wananchi waliokusanyika kwa wingi kumpokea wakati akiwa safarini kuelekea Mbamba Bay, wilayani Nyasa.
Amesema kuwa tangu nchi ilipopata uhuru, ajenda za CCM zimekuwa zikilenga kutatua changamoto za wananchi, jambo ambalo limechangia maendeleo yanayoonekana nchini hadi sasa.
Aidha, Dkt. Nchimbi amesisitiza kuwa chama hicho kitaendelea kupeleka maendeleo kwa wananchi huku kikilinda amani na utulivu wa Taifa.