PreGE2025 Dkt. Nchimbi: Kipaumbele kitabaki kuwa maisha bora kwa Watanzania

Mijadala ya Uchaguzi Mkuu wa Tanzania 2025 (Kabla)

Waufukweni

JF-Expert Member
Joined
May 16, 2024
Posts
4,393
Reaction score
14,500
Katibu Mkuu wa Chama Cha Mapinduzi (CCM), Balozi Dkt. Emmanuel Nchimbi, amesema chini ya uongozi wa Rais Samia Suluhu Hassan, huduma za matibabu zimeimarika kutokana na kuboreshwa kwa hospitali za rufaa za mikoa.

Ameongeza kuwa ajenda kuu ya chama hicho ni kuendelea kuboresha huduma za afya kwa Watanzania.

Dkt. Nchimbi ameyasema hayo mjini Musoma wakati akipokea taarifa ya maendeleo ya mradi wa Hospitali ya Rufaa ya Kumbukumbu ya Mwalimu Julius Nyerere iliyopo Kata ya Kwangwa, ambapo amesema kuwa taarifa kuhusu idadi ya wagonjwa wanaotibiwa kutoka ndani na nje ya nchi zinaonyesha kuimarika kwa huduma za afya.

Kupata matukio na taarifa zote kwa kila mkoa kuelekea Uchaguzi Mkuu 2025 ingia hapa: Special Thread: Mijadala na Matukio ya Uchaguzi Mikoa yote Tanzania Bara na Zanzibar kuelekea Uchaguzi Mkuu 2025

Katika hatua nyingine, amemuelekeza Waziri wa Fedha, Dkt. Mwigulu Nchemba, kuhakikisha ndani ya kipindi cha wiki mbili fedha kwa ajili ya ununuzi wa jenereta zinatolewa ili kuwezesha upatikanaji wa umeme wa uhakika hospitalini hapo wakati wote.

Hospitali ya Rufaa ya Kumbukumbu ya Mwalimu Julius Nyerere ilianza tangu awamu ya kwanza ya serikali.

Maisha Bora Makal*o yake!

Miaka zaidi ya 40 wameshindwa kumaliza tatizo simpo Tu la Maji, umeme au matundu ya vyoo mashuleni kwa asilimia walau 95% .

Hayo maisha Bora watayaleta kwa njia ipi, YAS ?
 
Maisha bora yaanze na kuthamini uhai wa mtanzania na yeyote anayeishi ndani ya JMT.
 
Maisha Bora Makal*o yake!

Miaka zaidi ya 40 wameshindwa kumaliza tatizo simpo Tu la Maji, umeme au matundu ya vyoo mashuleni kwa asilimia walau 95% .

Hayo maisha Bora watayaleta kwa njia ipi, YAS ?
I feel you brother!

acha tu, yaani maCCM wanatuchukulia poa sana

kitu hawajui ni kuwa siku hizi wananchi wameamka,

wao wanadhani bado tupo katika enzi za Zidumu Fikra Shaii za Mwenyekiti wa CCM
 
Katibu Mkuu wa Chama Cha Mapinduzi (CCM), Balozi Dkt. Emmanuel Nchimbi, amesema chini ya uongozi wa Rais Samia Suluhu Hassan, huduma za matibabu zimeimarika kutokana na kuboreshwa kwa hospitali za rufaa za mikoa.

Ameongeza kuwa ajenda kuu ya chama hicho ni kuendelea kuboresha huduma za afya kwa Watanzania.

Dkt. Nchimbi ameyasema hayo mjini Musoma wakati akipokea taarifa ya maendeleo ya mradi wa Hospitali ya Rufaa ya Kumbukumbu ya Mwalimu Julius Nyerere iliyopo Kata ya Kwangwa, ambapo amesema kuwa taarifa kuhusu idadi ya wagonjwa wanaotibiwa kutoka ndani na nje ya nchi zinaonyesha kuimarika kwa huduma za afya.

Katika hatua nyingine, amemuelekeza Waziri wa Fedha, Dkt. Mwigulu Nchemba, kuhakikisha ndani ya kipindi cha wiki mbili fedha kwa ajili ya ununuzi wa jenereta zinatolewa ili kuwezesha upatikanaji wa umeme wa uhakika hospitalini hapo wakati wote.

Hospitali ya Rufaa ya Kumbukumbu ya Mwalimu Julius Nyerere ilianza tangu awamu ya kwanza ya serikali.
View attachment 3325019
Emmanuel Nchimbi tunamfahamu toka akiwa kijana UVCCM.
Maisha yake yote ni katika siasa.
Huyu ni mmoja wa watu watuambie tathmini yake ya yale tunayoyaona sasa, na kama yamekaa katika ushirikishwaji wa wananchi wote wa Tanzania.
Tunajua , kuongoza watu ni kazi kubwa, lakini kitu cha kwanza ni sera shirikishi kwa watu wote nchini.
 
Ccm kuna wenye akili nyingi na uwezo mfano huyu jamaa, tatizo ukishakuwa huko ni kama akili zako zinatoka kichwani zinahamia matakoni
 
Back
Top Bottom