Dkt Mwinyi ‘awaangukia’ wauguzi nchini

Dkt Mwinyi ‘awaangukia’ wauguzi nchini

ndiyomkuusana

JF-Expert Member
Joined
Aug 2, 2012
Posts
668
Reaction score
426
WAZIRI wa Afya na Ustawi wa Jamii, Dk. Husein Mwinyi amewasihi wauguzi nchini kutofanya mgomo kama ule wa madaktari, kwa vile serikali imeanza kushughulika na madai yao mbalimbali ikiwa ni pamoja na upandishwaji wa posho zao ambazo zilikuwa zikilipwa kwa viwango vya chini.

Akizungumza jana wakati wa ufunguzi wa mkutano wa tano wa Chama cha Wauguzi Tanzania (TANNA), Mwinyi alisema migomo siyo njia bora ya kutatua migogoro bali mazungumzo na kuwaomba kuwasiliana na ofisi yake kila wanapokuwa na madai mbalimbali.

“Ninawasii kutulia wakati Serikali ikishughulikia madai yenu mbalimbali, lakini pia niwapongeze kwa kutogoma wakati ule wa mgomo wa madaktari walipogoma. Majadiliano ni njia bora ya kutatua matatizo na siyo migomo,” alieleza Mwinyi.

Alisema ajira za wauguzi katika sekta ya Afya ni asilimia 60 ya watumishi wote na kubainisha kamba hili ndilo jeshi kubwa ambalo limekuwa likifanikisha utoaji huduma za afya.

Kuthibitisha ushughulikiaji wa madai yao alisema wizara yake imepeleka maombi idara ya utumishi maboresho ya posho za ada sare kutoka Sh120,000 hadi Sh300,000 kwa mwaka, huku akiangalia uwezekano wa kuboresha pia posho za wito kazini (On Call allowance) ili waweze kuzipata bila ya kikwazo.

Awali akitoa maelezo ya mkutano wao,Rais wa chama cha wauguzi Tanzania, Paul Magesa alisema wakati wa mgomo wa

madaktari walipokutana na Waziri Mkuu, Mizengo Pinza pia walitoa malalamiko yao wakiitaka Serikali kuyafanyia kazi lakini mpaka leo hayajashughulika.

“katika mgomo huo tulionyesha uungwana tulitoa mapendekezo

kwa kamati, lakini inatuuma sana kwani mpaka leo madai yetu hayajashughulikiwa, ila hatupendi hali iendelee…,” alieleza.

source: mwananchi
 
hivi madaktari na watumishi wengine wa afya hawahitaji uniform allowance?
 
WAZIRI wa Afya na Ustawi wa Jamii, Dk. Husein Mwinyi amewasihi wauguzi nchini kutofanya mgomo kama ule wa madaktari, kwa vile serikali imeanza kushughulika na madai yao mbalimbali ikiwa ni pamoja na upandishwaji wa posho zao ambazo zilikuwa zikilipwa kwa viwango vya chini.

Akizungumza jana wakati wa ufunguzi wa mkutano wa tano wa Chama cha Wauguzi Tanzania (TANNA), Mwinyi alisema migomo siyo njia bora ya kutatua migogoro bali mazungumzo na kuwaomba kuwasiliana na ofisi yake kila wanapokuwa na madai mbalimbali.

"Ninawasii kutulia wakati Serikali ikishughulikia madai yenu mbalimbali, lakini pia niwapongeze kwa kutogoma wakati ule wa mgomo wa madaktari walipogoma. Majadiliano ni njia bora ya kutatua matatizo na siyo migomo," alieleza Mwinyi.

Alisema ajira za wauguzi katika sekta ya Afya ni asilimia 60 ya watumishi wote na kubainisha kamba hili ndilo jeshi kubwa ambalo limekuwa likifanikisha utoaji huduma za afya.

Kuthibitisha ushughulikiaji wa madai yao alisema wizara yake imepeleka maombi idara ya utumishi maboresho ya posho za ada sare kutoka Sh120,000 hadi Sh300,000 kwa mwaka, huku akiangalia uwezekano wa kuboresha pia posho za wito kazini (On Call allowance) ili waweze kuzipata bila ya kikwazo.

Awali akitoa maelezo ya mkutano wao,Rais wa chama cha wauguzi Tanzania, Paul Magesa alisema wakati wa mgomo wa

madaktari walipokutana na Waziri Mkuu, Mizengo Pinza pia walitoa malalamiko yao wakiitaka Serikali kuyafanyia kazi lakini mpaka leo hayajashughulika.

"katika mgomo huo tulionyesha uungwana tulitoa mapendekezo

kwa kamati, lakini inatuuma sana kwani mpaka leo madai yetu hayajashughulikiwa, ila hatupendi hali iendelee…," alieleza.

source: mwananchi

si mliamua kumtumikia KAFIRI endeleeni tu.
 
Back
Top Bottom