Dkt. Mwinyi asema azma ya kuifungua Pemba kiuchumi inakwenda vizuri

Ojuolegbha

JF-Expert Member
Sep 6, 2020
741
479
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mhe. Dk. Hussein Ali Mwinyi amesema wakati wa kuadhimisha miaka 3 ya uongozi wake azma yake ya kuifungua Pemba kiuchumi inakwenda vizuri.

Dk. Mwinyi aliahidi kuifungua Pemba kibiashara na uwekezaji kupitia maeneo makuu manne ikiwemo mkakati wa kuboresha bandari za Pemba ambao unaendelea, ujenzi wa barabara, kuvutia uwekezaji wa viwanda eneo la Chamanangwe yote yatatimia kabla ya uchaguzi mkuu 2025.

Rais Dk. Mwinyi amesema hayo akindua boti mpya ya Zanzibar 3 ya Kampuni ya Zan Fast Ferries itakayofanya safari zake Pemba hadi Unguja kwa muda wa saa mbili, Tanga na Dar es Salaam bandari ya Mkoani Mkoa wa Kusini Pemba leo tarehe 01 Novemba, 2023.

Rais Dk. Mwinyi amesema alizungumza na wawekezaji mbalimbali kuhusu changamoto ya usafiri Pemba wa anga na bahari hatimaye wawekezaji hao wameitikia wito ikiwemo Kampuni ya Azam Marine, na leo Zan Fast Ferries kuileta boti mpya ya Zanzibar 3 kwa safari za Pemba. Pia kampuni za Flight link na Assalam Air kuongeza ndege kwa safari za Pemba .

01 Novemba, 2023.

Mkoa wa Kusini Pemba.

IMG-20231101-WA0034.jpg
IMG-20231101-WA0045.jpg
IMG-20231101-WA0046.jpg
IMG-20231101-WA0047.jpg
IMG-20231101-WA0036.jpg
IMG-20231101-WA0043.jpg
IMG-20231101-WA0037.jpg
IMG-20231101-WA0044.jpg
IMG-20231101-WA0032.jpg
IMG-20231101-WA0033.jpg
IMG-20231101-WA0035.jpg
 

Attachments

  • IMG-20231101-WA0034.jpg
    IMG-20231101-WA0034.jpg
    70.3 KB · Views: 2
Na uzuri wa wapemba huwa hawatishiki na vitu, hata mkutano hawakuudhuria. Walienda na ccm wao na kurudi nao.
 
Back
Top Bottom