Nakubali mkuu, nasikia jamaa ana ugonjwa wa kuzimika zimika kama best wake wa zamani, malipo ni hapa hapa duniani. Dunia itatucheka wabongo kama huyu muuaji na mtesaji akiwa rais.
Kuna nyoka anaitwa ndumilakuwili, huyu ni kiumbe aina ya reptilia. Huuma kwa kutumia kichwa cha kwanza na ukimdhibiti anageuka na kutumia kichwa cha pili.
Sote tunajua kua ile ripoti ya richmond bungeni ilificha baadhi ya mambo (sababu sijui).
Baada ya sakata la richmond sote tulishuhudia mfululizo wa vita kali ndani ya serikali miongoni mwa vigogo.
Mwisho tumeshuhudia Mwakyembe akimalizia picha kwa kupatwa na ugonjwa wa ajabu.
Maswali ya kujiuliza:
1. Kwa nini ripoti ya richmond iliyosomwa na Mwakyembe ilificha baadhi ya mambo?
2. Kwa nini ripoti ya ugonjwa unaomsumbua Mwakyembe haiwekwi wazi?
3. Kuna nini kati ya serikali, wananchi na Mwakyembe hadi mambo mazito kama haya yafichwe na yeye Mwakyembe kutulia tuli kama hayamuhusu?
4. Je, Mwakyembe ana siri nzito isiyotakiwa kutolewa hadharani?
5. Mambo haya yote ni kwa faida ya nani, Mwakyembe, Serikali au Wananchi?
Waandishi wa Habari wa Tanzania na Wahariri wao ni wa kuwahurumia. Eti ni waraka wa siri; tena wanoa ndugu zake; tena gazeti linao; Sasa kuna siri tena hapo? Au ni majungu ya kuuzia magazeti?
Mkuu punguza jazba majina ya watu huwa hayatajwi hovyo. Assume unaandika kuwa amewataja fulani na fulani then kesho na keshokutwa Mwakyembe anakanusha kuwa hahusiki na waraka huo sasa haijala kwako?? Unajua pia ipo haja ya kubalance story kabla ya kuitoa kwenye public?? Tuwe na subira Kibanda na wenzake ni watu makini na wanajua wanachokifanya na leo sio mara ya kwanza kufichwa majina....rejea hata issue ya zombe tuliwajua wahusika wote baada ya kufikishwa mahakamani.
kama umeogopa kutaja majina kwa sababu kesho na kesho kutwa Mwakyembe anaweza kusema hahusiki na huo waraka basi umetudanganya kusema huu Waraka ni wa Mwakyembe wakati huna hakika, hujui kitu! Ndo maana nasema nyinyi waandishi ni waongo na vilaza ambao hamjui journalism ikoje na msingeijua hata ingewapiga usoni!
Ungeweka wazi kwamba kuna waraka ulioandikwa unaodai unatoka kwa Mwakyembe unaotaja Edward na Khalfani na Bernard na Saidi na nk nk however this newspaper could not independently confirm the authenticity of its authorship, halafu unapiga simu moja tu ya kizushi kwenye ofisi za naibu Waziri, asipopokea unaandika kwamba simu yake ilikuwa haipatikani au akipokea tarishi unaacha ujumbe Mwakyembe akutafute, asiporudisha simu kabla ya print time, unaenda hewani na habari. Mwisho!
Waraka unao but then ati ''unayahifadhi majina kwa sasa''. Huu si uoga tena bali ni uzezeta. Sijui lini tutapata waandishi wa habari makini. Habari hii ni uzushi na tetesi tu...ili wauze gazeti.
Nakubali mkuu, nasikia jamaa ana ugonjwa wa kuzimika zimika kama best wake wa zamani, malipo ni hapa hapa duniani. Dunia itatucheka wabongo kama huyu muuaji na mtesaji akiwa rais.
Dk. Mwakyembe sasa aandika waraka wa siri
AUSAMBAZA KWA NDUGU, JAMAA NA MARAFIKI ZAKE WA KARIBU
NAIBU Waziri wa Ujenzi anayeugua ugonjwa uliozusha utata mkubwa serikalini, Dk. Harrison Mwakyembe, ameandika waraka mahususi unaoeleza kile anachokiamini kuwa ni chanzo cha ugonjwa wake, Tanzania Daima Jumatano limebaini. Waraka huo ambao gazeti hili limeuona mbali ya kueleza kile ambacho Mwakyembe mwenyewe anaamini kuwa ni chanzo cha ugonjwa wake, unaeleza pia jinsi alivyoanza kuugua, watu anaowashuku kuwa nyuma ya mpango huo, siku na tarehe aliyodhani kuwa ndiyo aliyowekewa sumu hiyo.
Kama hiyo haitoshi, Mwakyembe katika waraka wake huo pasipo kueleza chanzo halisi cha undani wa taarifa zake, anaeleza mbinu iliyotumika kumdhuru na mahala mpango huo wa kumdhuru ulipopangwa. Uchunguzi uliofanywa na gazeti hili umebaini kwamba Dk. Mwakyembe ambaye kwa sasa yuko nchini India ameusambaza waraka huo kwa ndugu, jamaa na marafiki zake wa karibu. Katika waraka huo, Dk. Mwakyembe anaeleza kwamba anaamini alipewa sumu hiyo akiwa ofisini kwake huku akitaja majina ya watu anaowatuhumu kuwa nyuma ya mpango huo ambao gazeti hili kwa sasa linahifadhi majina yao.
Kwa mujibu wa Dk. Mwakyembe, mara tu baada ya kuwekewa sumu hiyo alianza kuwashwa mwili kabla ya hali kuendelea kuzorota na kuwa mbaya. Akionekana kujibu hoja za Mkurugenzi wa Makosa ya Jinai (DCI), Robert Manumba, mwanasiasa huyo katika waraka wake anaeleza kwamba hakuwekewa sumu hiyo kwenye chakula, bali kwenye sabuni na kitaulo cha kujifutia, ambacho huwekwa kwenye chumba maalumu ofisini kwake kwa ajili ya kusafisha mikono na huduma nyingine awapo ofisini.
Vyanzo vyetu vya habari kutoka kwa ndugu na marafiki wa karibu wa Dk. Mwakyembe vilisema kuwa, naibu waziri huyo ambaye pia ni Mbunge wa Kyela, amefikia hatua ya kuandika waraka huo kwa lengo la kutaka kuijulisha familia yake na taifa kile anachoamini anakabiliana nacho endapo atapoteza maisha kabla ya ukweli kamili kubainishwa. Hata hivyo, kutokana na ukweli kwamba suala hilo la afya ya Dk. Mwakyembe liko katika hatua za uchunguzi, Tanzania Daima Jumatano haliwezi kuandika kwa undani kuhusu waraka huo kwa sasa.
Ukiacha hilo, Dk. Mwakyembe katika waraka huo ameelezea historia ya maisha yake kisiasa na mikasa iliyompata kiasi cha kujijengea maadui.Ameeleza jinsi alivyonusurika kuuawa mara kadhaa na kwamba taarifa zote za mikasa yake aliziripoti polisi, lakini hakuna hatua zilizochukuliwa na Jeshi hilo la Polisi.
Baadhi ya mikasa aliyoitaja kwenye waraka huo ni pamoja na tukio la kunusurika kuuawa kwenye ajali ya gari iliyotokea Mei 21, mwaka 2009. Ajali hiyo ilitokea eneo la Ihemi, kilomita 40 kutoka Iringa mjini akiwa safarini kutokea Mbeya kwenda Dar es Salaam. Kwa mujibu wa waraka huo, gari alilokuwa akisafiria aina ya Toyota Land Cruiser T 362 ACH, liliacha njia saa moja asubuhi baada ya kukanyaga shimo na tairi ya upande wa kulia kuchomoka na dereva wake, Joseph Msuya (30), kupoteza mwelekeo kabla ya gari hilo kutoka nje ya barabara upande wa kushoto na kuparamia mti kisha kupinduka.
Ajali hiyo ilitokea wakati dereva wa Dk. Mwakyembe akijaribu kulipita lori kabla ya kukanyaga shimo hilo. Anasema katika ajali hiyo aliokolewa na wasamaria wema pamoja na trafiki wawili waliokuwa kwenye basi dogo waliokuwa wakisafiri kutoka Iringa kwenda Njombe. Anasema katika waraka huo kuwa, baada ya ajali hiyo alilazwa katika Hospitali ya Mkoa wa Iringa kutokana na kuumia taya kisha alihamishiwa Dar es Salaam kwa matibabu zaidi. Kwa mujibu wa waraka huo, Mkuu wa Jeshi la Polisi (IGP), Said Mwema, aliunda tume iliyoongozwa na Mkuu wa Kikosi cha Usalama Barabarani wakati huo, Kamanda James Kombe, kuchunguza chanzo cha ajali hiyo.
2a. Mwakyembe alitoka Kyela jana yake jioni na kulala makambako kwa sababu walikuwa wamechelewa
2b. kwa kulala makambako walichoka na Hivyo mapema asubuhi walipoanza safari; mwakyembe alilala usingizi hadi wanapofika Ihemi (kilomita 120 kutoka Makambao)
2c. Dereva kwa uzembe naye alikuwa amelala (amesinzia) (hapa asitudanganye) kwa uchovu
Jason bourne big up.ulitufumbua macho.sasa wanaumana wao kwa wao.naomba dr mwakyembe apone. Ila ikitokea kifo chake basi ndiyo itakuwa turning point ya mapinduz ya kweli
Saed Kubenea, an investigative journalist in the weekly Mwana Halisi is fighting for his life in hospital after unknown armed men attacked him and a colleague in their office yesterday night in what he believes attempts to terminate his life.
The journalist who sustained severe head injuries is also facing the danger of permanently losing sight after one of the bandits poured him acid on his face before they sped away.
Speaking at his bed at Muhimbili National Hospital (MNH) yesterday, Kubenea said the incident happened at around 9:00 when he and another veteran journalist Ndimara Tigambwage were winding up office duties ready to left for their homes.
"This is the real cost of practicing journalism fearlessly and professionally," courageous and unafraid Kubenea said from his bed flanked by journalists and relatives.
"It is a fight against the truth we uncover and hard-hitting features we publish, nothing else! He said.
The Kinondoni Regional Police Commander, Jamal Rwambow told the Citizen yesterday that investigation on the incident was going on well, promising to release a comprehensive statement today.
Kubenea, news editor with Kiswahili weeklies, Mwana Halisi and Mseto has come out fearlessly last year to expose scandals, office abuse and allegations of embezzlement of public funds involving big shots within and outside the government.
He vowed, however, at his bed not to give up with investigative journalism that has increasingly put his life in jeopardy in recent months.
The writer has received at least 15 text messages from unknown persons from June last year threatening to terminate his life shouldn't he stop following up their life.
"Your death will be of its kind that your body will never be found," one of the SMS he received read.
Another reads:" Take your last breath. We are not far from you. Few hours are left before we send you where you deserve."
"Watch out we are not joking on this. We want your death to be a threat even to mabwana zako.
Doctors treating him are yet to identify the type of acid poured on him and have advised him to seek specialized treatment in India. Kubenea told reporters relatives and friends are making arrangements to secure air ticket and fly him to India, possibly tomorrow.
The opposition Civic United Front (CUF) deputy secretary general (Zanzibar) Juma Haji Duni visited the hospital to comfort Kubenea, describing the act as a failed attempt to suppress the truth.
"This is just a threat to stop you from writing the truth. Do what you good conscious directs you, you don't have to give up,|" Duni said.
Narrating, Kubenea said three men knocked at their office door. Upon opening the door, he found himself surrounded with the men armed with machetes, knives and iron bar, telling him that they needed his soul.
Fight broke out when Ndimara intervened to rescue his colleague. During the fight, he said, one bandit dropped a machete but when he (Kubenea) tried to pick it, acid on his face.
According to Kubenea, the bandits later speed away, probably in belief that Kubenea he already has died.
JamiiForums uses cookies to help personalise content, tailor your experience and to keep you logged in if you register.
By continuing to use this site, you are consenting to our use of cookies.