HATUA ya kupungua kwa mizigo
inayotoka nje ya nchi kwenye
Bandari ya Salama haitokani na
ongezeko la kodi, anaadika
Regina Mkonde.
Dk. Phillip Mpango, Waziri
wa Fedha na Mipango
amesema kuwa, pamoja
na kuwepo kwa madai
kwamba, mizigo kutoka
nje ya nchi imepungua
kutokana na ongezeko la
kodi “kauli hii si ya kweli.”
Dk Mpango ametoa kauli hiyo leo
katika mkutano wa
uorodheshwaji wa hisa kwenye
Soko la Hisa la Dar es Salaam
(DSE) uliofanyika jijini Dar es
Salaam.
Mpango amefafanua kuwa,
kuyumba kwa soko la China
ndiyo sababu ya mizigo hiyo
kupungua kwa kuwa, Tanzania
inashirikiana na nchi hiyo katika
masuala ya kiuchumi.
“Muangalie uchumi wa China
unavyokwenda, soko lake
limepungua ulimwenguni,
kutokana na sababu ya nchi
kuwa na ushirikiano wa
kiuchumi na china kumeathiri.
Kodi haiathiri chochote kile, na
kelele zote zinazoendelea
zinafanywa na wale wakwepa
kulipa kodi.
“Waambie waache porojo,
waende kwenye takwimu, hata
kwa nchi jirani ya Kenya mizigo
inayoingia imepungua kwenye
Bandari ya Mombasa. Waende
wakapate ripoti.”
Amesema kuwa, serikali ipo
makini na wafanyabishara
ambao hawataki kulipa kodi.
“Walipe kodi tu ili serikali iweze
kuwahudumia, haiwezekani
bandari itoe huduma kwa
wafanyabiashara pasi na wao
kulipa kodi, hapana.”