Dkt Mlundwa: Zitto atofautishe Uchumi na Uhasibu

Anayetamka mambo ya hirizi kuhusu zitto hana ufahamu hata robo ya ufahamu wa zitto kuhusu uchumi na fedha. zitto ni wa kiwango cha juu sana kuliko hao wanaomkosoa. Fikiri mara 100 unapotaka kumkosoa zitto kabwe.
Kusoma darasani ni kitu kimoja, Lengo la elimu ni kutoa facts, kuchambua na kuweza kupambana na mazingira yanayobadilika

Uhasibu sio makaratasi au kusoma darasani

Kuna kipindi zito alipeleka kipengele cha Transfer pricing pale makampuni ya gesi yanapobadili gia angani na kuuziana share kinyemela kuwa yanapaswa kutoa gawio kwa serikali alipingwa na hao wachumi mpaka hao maprofesa uchwara

Ishu baada ya kuzaa matunda kelele kimya

Hoja hazijibiwi kwa notes za darasani bali kwa uchunguzi na kusoma taarifa mbalimbali za eneo husika

Huyo Johaness anazijua BoT reports ?
 
Tukiuliza maswali magumu wanakuja na majibu rahisi sasa sie tuwaulize maswali rahisi kabisa. Hivi Bodi ya wakurugenzi ya BOT ndio imepitisha mwaka huu walipe gawiyo la faida kwa kutumia mchanganyiko wa faida ya biashara ya mwaka huu na malimbikizo ya mapato ya miaka iliopita?

Kufanya hivi ndio uvumbuzi wa kiuhasibu tena ndani ya BOT? Kama ndio ni ujinga wa kiwango cha lami. Huwezi kutumia malimbikizo ya fedha zilizohifadhiwa kwa muda mwingi kwa kugawiya shareholders.
 
Nimeona mjadala leo katika page yake ya facebook akihoji inakuwaje BoT imepata faida ya Bilioni 200 halafu ikatoa gawio la Bilioni 300!

Ukiisoma hoja ya Zito utashangazwa na matusi aliyopewa ikiwemo msomaji mmoja aliyehoji utazisomaje taarifa za kihasibu ukiwa na hirizi kiunoni?Kejeli gani hizi!

Ukiacha kejeli hiyo isiyo na msingi kilichopo hapa ni kwamba Zito anahoja ila kihoja cha hoja yake ni kwamba ametumia taaluma yake ya uchumi kwa kiwango cha darasa la nne!

Kwa kiwango hicho utaona haiwezekani kugawa gawio la Bilioni 300 kwa faida ya Bilioni 200.

Lakini kwa nini leo nataka kumsaidia mchumi Zitto ajue tofauti ya uchumi na uhasibu ni kwamba katika taaluma ya ubasibu na uandaaji wa mahesabu kuna kitu kinaitwa "notes" hizi zinakusaidia kupata ufafanuzi wa masuala kadhaa katika taarifa za fedha.

Lakini la pili ambalo ndugu yangu Zitto limempitia mbali katika taaluma ya uhasibu ni ukweli kwamba kuna faida iliyopatikana mwaka huo (bilioni 200) lakini kuna mapato mengine kitaalamu yanaitwa "retained earnings" ambazo zimeainishwa katika taarifa za BoT ambavyo vyote kwa pamoja vina mchango tofauti katika kuamua gawio (vikisomwa kwa pamoja na masahihisho ya BoT kuhusu kama gawio ni mil. 300 au Bilioni 300).

Gawio kwa mujibu wa kifungu cha 18 cha BoT Act ni mchanganyiko wa faida na mapato mengine ya taasisi hiyo hasa hizo "retained earnings" ambazo hupatikana baada ya zoezi la kukokotoa "losses and gains" na hizi huwa zinakuwa carried forward katika hesabu za mwaka mwingine.

Sasa ukitumia uchumi hutaliona hili bali ukizisoma tarakimu kihasibu zaidi utajua kuwa gawio la asilimia 10 katika faida ya 200b ukijumlisha na "retained earnings" baada ya kubalansi "losses and gains" BoT ilikuwa na uwezo wa kugawa gawio la zaidi hata ya Bilioni 350 kwa Serikali. Na haya yote yapo katika taarifa ya hesabu za BoT ya yameainishwa vyema katika taarifa ya hesabu zake.

Nimshauri tu Zitto Kabwe katika zama hizi ni vyema kujipa muda kutafiti zaidi mambo ya uchumi na kihasibu kuliko anavyoaibika katika hili na mengine kadhaa niliyomsoma kabla ya hili.

Nafahamu kama mwanasiasa anahamu sana ya kuikosoa Serikalianapohisi mahali fulani kuna kasoro lakini ushauri wa bure ni atafiti na kutathmini kabla ya kuandika maana anaangusha taaluma aliyoisomea ambayo pia ni taaluma ya wengi: *think before you ink*

_Dkt Johannes Mlundwa (MA Finance London, CPA T)_
Naomba nikukosoe mkuu "retained earnings" sio mapato mengine... bali ni faida inayorudishwa kwenye kampuni kwa ajili ya kuinvest na shuguli zingine, .. baada ya kutoa portion ya gawio .... Unapoongelea mapato mengine "other income" ni faida inayopatikana kwenye vyanzo vingine vya mapato ambavyo ni tofauti na normal operations za kampuni husika haina uhusiano na retained earnings.
 
Hoja mtambuka ni je ni lini last time BOT imetoa gawiwo kwa serikali?. Kama imekuwa ikitoa ktk miaka iliyopita bila kukosa, then itakuwa inafikirisha Kuwa hilo gawiwo la 300B zimetoka wapi wakati profit mwaka huu ni just 200 B
 
Kwa kawaida retained earnings hazitolewi kiholela,jamani.Ukisha lipa dividend zinazobaki mara nyingi zinafidia losses hivyo si rahisi kulipa gawia nje ya profit ni hatari hata kwa taasisi.Tusidanganyane kwa sababu ya kutaka vyeo.

Pigeni zumari sana lakini effect ya zumari tutakuja kuliona baadaye.Ukiangalia kwanini taasisi/mashirika yetu yamekufa ni kwa sababu yakuingilia taaluma za watu wengine.

Haya ya kuingilia kupiga data za Bank kuu yatatugharimu kama Taifa,tusipige makofi tu bila kufikiri sababu tu kuenzi uchama badala ya taaluma

Kaka aliyeandika hapo juu ni CPA (T) Kwa maana ya kuwa ni authority
 
Hoja mtambuka ni je ni lini last time BOT imetoa gawiwo kwa serikali?. Kama imekuwa ikitoa ktk miaka iliyopita bila kukosa, then itakuwa inafikirisha Kuwa hilo gawiwo la 300B zimetoka wapi wakati profit mwaka huu ni just 200 B
 
Acha kujifurahisha penye stahili tusilete siasa ,Lipumba ni mbombezi wa uchumi,wewe hata usome vipi humfikia Lipumba hata robo,Chadema nzima mtu ambaye anaweza kujilinganisha na Lipumba ni Baregu ,hata huyo mwenyekiti wenu kwa Lipumba ni kama kichunguu tu cha mtwa
Usomi wake umesaidiaje kuinua uchumi wa Nchi yake au kwako ww msomi niyule anaemiliki mabulungutu ya Vyeti?
 
In short wote Dr na Zitto hakuna mwenye fact ...Financial Statement ndio msemakweli. Ingawa Zitto nae alipaswa kwenda hatua zaidi ili doubt yake iwe na mashiko. Otherwise ndio dhana ya kukaa mkao wa kupinga tu serikali!
Kunadhambi yoyote ikiwa Serikali itapingwa kwa kufanya blah blah?
 
Naomba nikukosoe mkuu "retained earnings" sio mapato mengine... bali ni faida inayorudishwa kwenye kampuni kwa ajili ya kuinvest na shuguli zingine, .. baada ya kutoa portion ya gawio .... Unapoongelea mapato mengine "other income" ni faida inayopatikana kwenye vyanzo vingine vya mapato ambavyo ni tofauti na normal operations za kampuni husika haina uhusiano na retained earnings.
Bora hata usingekosoa tu ...
 
Baada ya kutoa expenses unabakiwa na profit, hiyo profit unaweza kuibakisha (retained earnings) au kuitoa kama (dividends).
Profit unayoibakisha utaiweka kama capital kwenye shirika, sasa kama serikali walikua wana-retain profit kipindi cha nyuma kwanini sasa hivi wanatoa dividends kubwa kuliko profit ya mwaka husika?
Kwasababu hile profit iliyobaki unai-reinvest tena..
Kama nimekosea naomba mnirekebishe, haya mambo nilisoma zamani.
 
Bora hata usingekosoa tu ...
Kama huu ulikusudiwa kuwa mjadala wa kihasibu, mleta mada amekosea kuiita retained earning kuwa ni other income. Hizo ni dhana mbili tofauti kabisa katika uhasibu.

Kama ni mjadala was level ya darasa la nne, itakuwa "sahihi" kuita "retained earnings" kuwa ni "other income".

Fani zinaingiliwa hapa. CPA ya huyo daktari mkosoaji inatia mashaka.
 
Kunadhambi yoyote ikiwa Serikali itapingwa kwa kufanya blah blah?
Tatizo sometimes mnajifanya hamuelewi. Tatizo kuna watu wamekaa mkao wa kupinga tu! Ndio maana Zitto wakati mwingine anakurupuka kutoa comment ili apinge tu! Tusimame kwa facts ....serikali ikikosea ipingwe na tuone pia mkisifia ikifanya vyema! Itasaidia kutupa attention hata mnapokosoa otherwise kabla hujaongea kila mtu anajua utapinga tu! Huwezi kufikiri positively kama umekaa mkao wa kupinga tu! Hatupaswi kuiga siasa za CCM bali kuwa mfano kwa CCM!
 
Kaka Hakuna sehemu Dr ametukana, ispokua amedadavua barabara
hao madokta uchwala , wachumia tumbo , any way usimuamini kila mtu anayeitwa daktar kumbuka hata rais wako anaitwa dokta ila mambo anayoyafanya hayatofautiani na mganga wa kienyeji , dokta manyaunyau
 
Nimeona mjadala leo katika page yake ya facebook akihoji inakuwaje BoT imepata faida ya Bilioni 200 halafu ikatoa gawio la Bilioni 300!

Ukiisoma hoja ya Zito utashangazwa na matusi aliyopewa ikiwemo msomaji mmoja aliyehoji utazisomaje taarifa za kihasibu ukiwa na hirizi kiunoni?Kejeli gani hizi!

Ukiacha kejeli hiyo isiyo na msingi kilichopo hapa ni kwamba Zito anahoja ila kihoja cha hoja yake ni kwamba ametumia taaluma yake ya uchumi kwa kiwango cha darasa la nne!

Kwa kiwango hicho utaona haiwezekani kugawa gawio la Bilioni 300 kwa faida ya Bilioni 200.

Lakini kwa nini leo nataka kumsaidia mchumi Zitto ajue tofauti ya uchumi na uhasibu ni kwamba katika taaluma ya ubasibu na uandaaji wa mahesabu kuna kitu kinaitwa "notes" hizi zinakusaidia kupata ufafanuzi wa masuala kadhaa katika taarifa za fedha.

Lakini la pili ambalo ndugu yangu Zitto limempitia mbali katika taaluma ya uhasibu ni ukweli kwamba kuna faida iliyopatikana mwaka huo (bilioni 200) lakini kuna mapato mengine kitaalamu yanaitwa "retained earnings" ambazo zimeainishwa katika taarifa za BoT ambavyo vyote kwa pamoja vina mchango tofauti katika kuamua gawio (vikisomwa kwa pamoja na masahihisho ya BoT kuhusu kama gawio ni mil. 300 au Bilioni 300).

Gawio kwa mujibu wa kifungu cha 18 cha BoT Act ni mchanganyiko wa faida na mapato mengine ya taasisi hiyo hasa hizo "retained earnings" ambazo hupatikana baada ya zoezi la kukokotoa "losses and gains" na hizi huwa zinakuwa carried forward katika hesabu za mwaka mwingine.

Sasa ukitumia uchumi hutaliona hili bali ukizisoma tarakimu kihasibu zaidi utajua kuwa gawio la asilimia 10 katika faida ya 200b ukijumlisha na "retained earnings" baada ya kubalansi "losses and gains" BoT ilikuwa na uwezo wa kugawa gawio la zaidi hata ya Bilioni 350 kwa Serikali. Na haya yote yapo katika taarifa ya hesabu za BoT ya yameainishwa vyema katika taarifa ya hesabu zake.

Nimshauri tu Zitto Kabwe katika zama hizi ni vyema kujipa muda kutafiti zaidi mambo ya uchumi na kihasibu kuliko anavyoaibika katika hili na mengine kadhaa niliyomsoma kabla ya hili.

Nafahamu kama mwanasiasa anahamu sana ya kuikosoa Serikalianapohisi mahali fulani kuna kasoro lakini ushauri wa bure ni atafiti na kutathmini kabla ya kuandika maana anaangusha taaluma aliyoisomea ambayo pia ni taaluma ya wengi: *think before you ink*

_Dkt Johannes Mlundwa (MA Finance London, CPA T)_
Labda kwa farida ya wanajamvi ni BOT kwa muda mrefu hawajatoa hilo gawio kwa serikali hivyo wakaamua kutoa na malimbikizo ya faida ya miaka ya nyuma. Ndio maana taarifa ya Mapato huwa kwa mwaka husika. Naungana na maada kuna tofauti kubwa kati ya fani ya uhasibu na uchumi katika utoaji wa taarifa hivyo hapo bw. Zito Kabwe kakurupuka has.
 
Tatizo sometimes mnajifanya hamuelewi. Tatizo kuna watu wamekaa mkao wa kupinga tu! Ndio maana Zitto wakati mwingine anakurupuka kutoa comment ili apinge tu! Tusimame kwa facts ....serikali ikikosea ipingwe na tuone pia mkisifia ikifanya vyema! Itasaidia kutupa attention hata mnapokosoa otherwise kabla hujaongea kila mtu anajua utapinga tu! Huwezi kufikiri positively kama umekaa mkao wa kupinga tu! Hatupaswi kuiga siasa za CCM bali kuwa mfano kwa CCM!
Mkuu kwanini unatamani watu wote wawe na mawazo yanayofanana? kama nikupongeza mbona wapo watu hata Media zinalazimishwa kupongeza hata mambo yakijinga.... huamini kwamba hawatoshi mpaka mpongezwe Nchi nzima?
Huoni kwamb kupinga kwa Zitto kumetuletea huu Mjadala hata sisi wengine tusioajua mambo ya Uchumi tunapata Shule hapa? Inawezekana zitto
anajua kila kitu ila kwavile anajua kuna baadhi ya mambo hayaeleweki kwa wananchi wengi na kwakujua Serikali ikishatoa Startment inasubiri kupigiwa makofi hata Mahali pasipoeleweka na wananchi ndio kachokoza hiyo ili wengi tujue... huamini kama hii ni Faida? au mnataka muwe mnelewa nyinyi tu
 
Labda kwa farida ya wanajamvi ni BOT kwa muda mrefu hawajatoa hilo gawio kwa serikali hivyo wakaamua kutoa na malimbikizo ya faida ya miaka ya nyuma. Ndio maana taarifa ya Mapato huwa kwa mwaka husika. Naungana na maada kuna tofauti kubwa kati ya fani ya uhasibu na uchumi katika utoaji wa taarifa hivyo hapo bw. Zito Kabwe kakurupuka has.
...unaFACTS
yakuthibitisha hii utuwekee hapa nasisi tuone?
 
Back
Top Bottom