Dkt. Magufuli aibomoa ngome ya Lowassa

Nyoka wa Makengeza anaweza kuwasaidia CCM maana ndio mpiga dili mwenzao nayekubalika mpaka akatunga katiba.
 
ccm mkilogwa mkampendekeza lowassa achukue fomu ya urais mmeumia.
 
Naomba kuuliza kwanini lowassa anatumia mabilioni kuutaka urais?je atarudishaje fedha zake?
 
Bora wameanza kubomoana wenyewe kwa wenyewe kabla hawajakumbwa na mafuriko ya UKAWA.
 
Wewe mwenyewe mleta mada upo kundi lipi, na je tukusaidieje ili mambo yakunyokee?
 

Na wale walioikosa ambao ndio walikusudiwa je haki ipo wapi?hapa tunazungumzia haki ,hakuna aliyebora au na afadhali pamoja na huyo Magufuli wote ni mafisadi tu,hana cha afadhali hata chembe wote ni ndege wa aina moja,halafu watu mnavyochekesha nikuwa kwa mfano kwa kumsema Magufuli basi mtu yupo kambi ya Lowasa au kwa kumsema Lowasa basi mtu yupo kambi ya Membe au Muhongo,kueni bana haya mambo ya kambi sio kila mtu anahusika,mumeanza ujinga wa kuwasema watu ambao wako against na watu mnaowataka kuwa wapo kambi fulani au chama fulani,wengine hatuna vyama wala kambi tunachosema ni kile tunachokiona,nadhani ndugu wewe ni mgeni humu JF,jaribu kupitia nyuzi zangu ndio utajua mimi ni mtu wa sampuli gani.
 
CCM ikisimamisha rais mwingine ya JP Magufuli au S. Sitta, basi ikae tayari kukabidhi mikoba ya Administration kwa Upinzani
 

Magufuli ana akili sana alifupisha njia ya kutoka mwanza hadi bukoba kiasi leo mtu unaweza kwenda bukoba na kurudi mwanza kabla jua halijatua,mpeni nafasi awatumikie watz.
 
Naona wanapingana na ile dhana yao ya kusimamisha mgombea Wa kike
 
ccm mkilogwa mkampendekeza lowassa achukue fomu ya urais mmeumia.

Sisiem walimtosa Lowassa, CDM wamempokea na kumpatia fursa ya kugombea urais kwa mwamvuli wa UKAWA, je, CDM na UKAWA nao wameumia? Naomba jibu lako fasta!
 
CHANGAMOTO ni gazeti linalochapwa wapi?
 
Magufuli kuibomomoa ngome ya aliyewahi kuwa bosi wake ni ngumu sana. Kitendo cha kusalitiana ndani ya ccm kitawamaliza kabla ya october kwani watahama wengi au kuendesha uasi wakiwa ndani ya chama. Kumbukeni kuwa hakuna dhambi na adui mbaya kama unafiki. Ni wachache sana walio ndani ya ccm wenye dhamira na mapenzi ya kweli na chama hicho kwani walio wengi walimpenda na kumwamini Lowasa kama rais wao na atakayeweza kuya-balance makundi yanayoasimiana ccm. Wengi watamfuata UKAWA na au watampigia kampeni za chinichini ili ashinde. Ccm ijiandae kushindwa kwani hata mwenyekiti wao alishawatabiria hilo badiliko.
Suala la ufisadi halina mashiko kwa sasa kwani kiukweli liliasisiwa na kulelewa ccm na moja ya nguzo kuu za ccm ya leo kuwa kama wewe siyo fisadi basi ni mpinzani wao. Ccm bomokeni mkajiumbe upya!
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…