Dkt. Kigwangalla: Kuna Mawaziri wamehongwa na mwekezaji wa Ngorongoro

Etwege

JF-Expert Member
Jul 4, 2018
5,738
15,208
Aliyekuwa Waziri wa Maliasili na Utalii wa awamu ya tano Dkt. Hamis Kigwangala alishawahi kunukuliwa akisema mwekezaji wa kitalu cha uwindaji Ngorongoro amekuwa na tabia ya kuhonga viongozi mbalimbali ikiwemo Mawaziri tangu alipopewa kitalu hicho mwaka 1992.

Kwenye video hiyo amesema kuna Waziri wa Utalii wa awamu ya nne alihongwa dola laki mbili ili aweze kumwachia mwekezaji huyo atekeleze masilahi yake .

 
Bila kuweka ushahidi wa kile anachoongea, itakuwa ni sawa na debe tupu. Aibu kwa mtu kama yeye kufanywa puppet na wamasai wa Kenya kwa ajili ya masilahi ya Kenya. Inakuaje waziri mstaafu mzima kufanywa zuzu na hawa watu wasiokuwa na elimu? Tanzania haiwezi kuendelea kufanywa shamba la bibi na manyang'au kamwe.
 
Bila kuweka ushahidi wa kile anachoongea, itakuwa ni sawa na debe tupu. Aibu kwa mtu kama yeye kufanywa puppet na wamasai wa Kenya kwa ajili ya masilahi ya wakenya. Tanzania haiwezi kuendelea kufanywa shamba la bibi na manyang'au kamwe.
Alafu wewe jamaa unakuwa na kiherehere...Pesa za muharabu zishakuchanganya?
 
Na yeye hamisi alipokuwa anaongoza hiyo wizara alihongwa dola laki ngapi? Maana amekiri mwenyewe kuwa tangu 1992 mwekezaji anahonga.
Ni muhimu kumpongeza Kigwangala kwa ujasiri huo.
Kuna rushwa nyingine ni kubwa na ngumu kupambana nazo kwa sababu ya ushawishi, madaraka ya wahusika na mtandao wao.
Tatizo kubwa kuliko yote katika taifa letu ni umasikini wa fikra kwa asilimia kubwa ya watu na hili hujidhihirisha kwenye mijadala kama hii.
 
Nadhani kingwangwala njaa imekaba fursa ya pesa ya mwarabu ingemfikia asingepiga kelele. Hana usafi gani wa kunyooshea wengine vidole?
 
Kila nikikumbuka kile kinyago chake cha mwalimu nyerere hata aongee nn namuona kama mzushi tu🥲
Hivi kigwangala QNET yeye walimhonga sh. Ngapi?
Screenshot_20220626-151536.jpg
 
Alafu wewe jamaa unakuwa na kiherehere...Pesa za muharabu zishakuchanganya?
Pesa ya muarabu inayopatikana kwa njia ya uwekezaji, na mavi ya ng'ombe yanayopatikana kwa njia ya shamba la bibi kipi bora? Muarabu anawekeza na faida inapatikana kwa taifa, mkenya anatujazia mavi ya ng'ombe na faida inapatikana kwa wakenya kuanzia nyama, maziwa, kodi nk. Yani mtu aje alishe mifugo yake kwenye shamba la bibi afu mifugo ikishanenepa kwa lishe bora, nyama na maziwa akauze kwao Kenya. Hii hai make sense kwa sisi tusioshikiwa akili.
 
Bila kuweka ushahidi wa kile anachoongea, itakuwa ni sawa na debe tupu. Aibu kwa mtu kama yeye kufanywa puppet na wamasai wa Kenya kwa ajili ya masilahi ya Kenya. Inakuaje waziri mstaafu mzima kufanywa zuzu na hawa watu wasiokuwa na elimu? Tanzania haiwezi kuendelea kufanywa shamba la bibi na manyang'au kamwe.
Njaa imemlazimisha awe chawa wa wachunga ng'ombe wa Kenya ndugu yangu.
 
Back
Top Bottom