Dkt. Kigwangalla azifungia hospitali mbili za kigeni

Informer

JF-Expert Member
Jul 29, 2006
1,599
6,669
a47feb534b8587cc9dd9a9f0791884f6.jpg

Naibu Waziri wa Afya, Dkt. Hamis Kigwangalla amezifungia hospital mbili tofauti zinazomilikiwa na Raia wa kigeni wakiwemo kutoka Korea kwa kile walichoeleza kuendesha huduma bila vibali maalum ikiwemo usajiri wa msajili wa hospital binafsi pamoja na ule wa msajili wa tiba mbadala.

8cfa2e3a0f89fa1bc84f84fa8600dcdd.jpg

Miongoni mwa vifaa vilivyokutwa ni pamoja na vile vinavyotumika mahospitalini na vingine vile ambavyo hawakuruhusiwa.

Hospitali hizo zilizovamiwa na kukaguliwa ni pamoja na Korea Medical Clinic ya Kariakoo Mtaa wa Mahiwa na nyingine ni Oriental Traditional medicine clinic... Ambazo zote zinazomilikiwa na Mabong.

Dk. Kigwangalla ameeleza kuwa watu hao wamekuwa wakitoa huduma bila vibali halali huku pia wakiendesha huduma pasipo kufahamu lugha za kiswahili na Kiingereza.

75f455918e3ba5af9c5d795291d9cb56.jpg
 
a47feb534b8587cc9dd9a9f0791884f6.jpg

Naibu Waziri wa Afya, Dkt. Hamis Kigwangalla amezifungia hospital mbili tofauti zinazomilikiwa na Raia wa kigeni wakiwemo kutoka Korea kwa kile walichoeleza kuendesha huduma bila vibali maalum ikiwemo usajiri wa msajiri wa hospital binafsi pamoja na ule wa msajiri wa tiba mbadala.

8cfa2e3a0f89fa1bc84f84fa8600dcdd.jpg

Miongoni mwa vifaa vilivyokutwa ni pamoja na vile vinavyotumika mahospitalini na vingine vile ambavyo hawakuruhusiwa.

Hospitali hizo zilizovamiwa na kukaguliwa ni pamoja na Korea Medical Clinic ya Kariakoo Mtaa wa Mahiwa na nyingine ni Oriental Traditional medicine clinic... Ambazo zote zinazomilikiwa na Mabong.

Dk. Kigwangalla ameeleza kuwa watu hao wamekuwa wakitoa huduma bila vibali halali huku pia wakiendesha huduma pasipo kufahamu lugha za kiswahili na Kiingereza.

75f455918e3ba5af9c5d795291d9cb56.jpg
kwanini awamu iliyopita iliwalinda , ni nani aliwaleta ? tuanzie hapa kwanza.
 
wakorea na wachina wameifanya nchi hii kama jalala au kichwa cha mwehu , sitaisamehe kamwe ccm kwa kugawa nchi yetu kama zawadi .
Halafu hawa wageni wanatudharau sana na mbaya zaidi wanadharau mpaka viongozi wetu.

Jana nilikuwa naangalia ITV jinsi mchina anavyowavimbia viongozi huko Wilaya ya Morogoro
 
Na hawa wachina ndio wanajifanya marafiki wema kwa nchi yetu, huko wanatumaliza kwa bidhaa feki na matibabu feki, ccm sijui nani kawapofua ufahamu?!
 
Na hawa wachina ndio wanajifanya marafiki wema kwa nchi yetu, huko wanatumaliza kwa bidhaa feki na matibabu feki, ccm sijui nani kawapofua ufahamu?!
Na mbugani vipusa vyote hasa tembo na faru ndio wamehamia china
 
hizo za kariakoo nilitamani sana apatikane mtu asaidie watanzania. Mheshimiwa Kigwangala hongera kwa hilo maana hata bei wanazotoza kwa siku ni kubwa mno na mgonjwa anatakiwa ahudhurie clinic miezi kama sita hivi. Kwa siku ilikuwa 40000 nadhani
 
  • Thanks
Reactions: 911
Na hawa wachina ndio wanajifanya marafiki wema kwa nchi yetu, huko wanatumaliza kwa bidhaa feki na matibabu feki, ccm sijui nani kawapofua ufahamu?!
mkuu ni ss ndo tunajipendekeza kwao,yote haya kwakuwa tunaogopa kukosolewa kunakofanywa na wale wa upande wa pli wa dunia pindi tunapofanya vibovu ila ukiangalia kati ya wageni wenye biashara za ajabu ajabu na waleta bidhaa feki na wachina sasa sijui wanatusaida au ndo wanatuua kabisa
 
aje na hapa ifakara ipo moja ya wachina hawana mswahili hata 1, lakin wanatibu watu, halafu hawajui kiswahili wala kiingereza, kunawakati najiuliza hivi huwa hakuna namna ya kuwalazimisha hawa jamaa wawe na watu wanaojua kiswahili?

pitien na huku ifakara N/w mtaona maajab mengi,
 
Ya Mwaka yaliishaje? Maana matangazo na vipindi vya upotoshaji kwenye TV na redio kama kawa. Jana nilikuwa nasikiliza redio moja nikakuta jamaa katinga humo akiwaelimisha wadanganyika kuwa anatibu kwa mitishamba/ dawa mbadala: hydrosalpinx, uterine fibroids, cancers, renal failures, congenital heart diseases, male impotence etc etc!
 
wakorea na wachina wameifanya nchi hii kama jalala au kichwa cha mwehu , sitaisamehe kamwe ccm kwa kugawa nchi yetu kama zawadi .

Pia ilinisikitisha sana jana kwenye taarifa ya habari huko morogoro kuna mchina alikuwa anachimba mawe yenye madini ya kutengeneza tile na viroba kadhaa vyenye mchanga wa dhahabu kinyume cha sheria.

Hii ni aibu sana hawa watu wanakuja nchini kwetu kama wanaingia chooni .
 
mkuu ni ss ndo tunajipendekeza kwao,yote haya kwakuwa tunaogopa kukosolewa kunakofanywa na wale wa upande wa pli wa dunia pindi tunapofanya vibovu ila ukiangalia kati ya wageni wenye biashara za ajabu ajabu na waleta bidhaa feki na wachina sasa sijui wanatusaida au ndo wanatuua kabisa

Usisahau kwamba Magufuli safari yake ya pili nje ya nchi itakuwa China.
Mbona tutakoma na hawa wachina.
 
shamba la bibi Tanzania, wachina, wakorea wamevuna sana, bado geraji bubu mitaani, kuna air polution, sound polution.
 
..naona vita yake na anayejiita Dr. Mwaka imeisha...maana siku hizi namwona Chanel 10 jioni akijinasibu kuwatibu wanawake kijanja....tofauti na zamani siku hizi anajiita tabibu Mwaka....huku akifanya kile kile alichokuwa akifanya zamani....nchi hii ina vioja sana....
 
Back
Top Bottom