“Sasa hivi tunaoishi katika Dunia hii tunatakiwa kuwa waangalifu wa kila jambo.”
Ni kauli ya Dkt. Khalid Salumu Mohamed, Waziri wa Ujenzi, Mawasiliano na Uchukuzi, Serikali ya Mapindizi Zanzibar (SMZ) aliyoitoa wakati akifungua rasmi mafunzo ya Dhana ya Ulinzi wa Taarifa Binafsi kwa Maafisa Habari na Wanachama wa Chama cha Waandishi wa Habari Zanzibar, ambapo amewataka wanahabari hao kulinda taarifa kwakuwa zinathamani kubwa.
==================================
Your browser is not able to display this video.
“Sheria ya Ulinzi wa Taarifa Binafsi inalenga kuhakikisha tunalinda Utu na Faragha na ni Sheria ambayo inazingatia katiba yetu”
Haya ni maneno ya Dkt. Emmanuel Mkilia, Mkurugenzi Mkuu wa Tume ya Ulinzi wa Taarifa Binafsi wakati akizungumza na Maafisa Habari wa Serikali ya Mapinduzi Zanzibar (SMZ) na Wanachama wa Chama cha Waandishi wa Habari Zanzibar kwenye hafla ya Uzinduzi wa Mafunzo ya siku moja ya Dhana ya Ulinzi wa Taarifa Binafsi kwa wanataaluma hao.