Dkt. Joseph Msukuma anastahili PhD kwa kuongeza makusanyo sekta ya madini Tanzania

GUSSIE

JF-Expert Member
Dec 2, 2014
3,866
11,100
Huwezi Kuongelea mabadiliko ya makusanyo ya madini Tanzania bila kutaja jina la Dkt Joseph kasheku Msukuma

Dkt Joseph Msukuma ndio mtu wa kwanza awamu ya tano kumgomea Waziri wa Fedha wakati huo Philip Mpango kuwa hatakubali bajeti ipite mpaka pale sheria ndogo za madini hasa vipengele vinavyohusu wachimbaji wadogo zitafanyiwa marekebisho.

Marekebisho ya Dkt Msukuma yameiwezesha serikali kukusanya pesa toka shilingi Milioni 87 za kitanzania kwa mwaka mpaka Shilingi bilioni 500 kwa mwaka toka kwa wachimbaji wadogo wa madini.

Ni PhD holder gani ameiwezesha serikali kufanya mambo haya makubwa.

PhD holders wengi na hasa Maprofesa wengi mnajua matokeo yake.

Tuna PhD holder Lipumba amefanya nini Tanzania.
Tuna PhD holder Kabudi amefanya nini Tanzania.
Tuna PhD holder Mkenda, Juzi ameambiwa ni mawazo nosense kuzuia sukari ya uganda.

Dkt Msukuma ni mtu anayesimamia anachokiamini kwa uwazi na ukweli.

Dkt Msukuma ni mfano wa matajiri toka jamii inayoitwa ya darasa la saba kwa Kumiliki migodi, Magari ya usafiri, Maduka ya kutosha kariakoo.

Dkt Msukuma na Kibajaji ni watu wenye mawazo ya kufikiri nje ya box kuliko watanzania wengi.

Hongera Dkt Joseph Msukuma umeingia kwenye list ya Wasomi Tanzania, Sasa Bungeni utaitwa Dkt na hata Mimi Gussie nakuita Dkt kwani unastahili heshima.

Katika haya maisha kuna watu wana bahati zao, Wengine wanatafuta kazi lakini Dkt Joseph Msukuma anawatengenezea watu kazi na ajira kwenye biashara zake.

Ni Dkt Joseph Msukuma anaewapa changamoto Wasomi ambao hawayajui mambo.
 
Back
Top Bottom