PostGE2025 Dkt. Biteko akabidhi rasmi ofisi kwa Waziri Ndejembi

PostGE2025 Dkt. Biteko akabidhi rasmi ofisi kwa Waziri Ndejembi

Conversations and stories after Tanzania's 2025 General Elections

Bawabu wa pili

Senior Member
Joined
Nov 14, 2025
Posts
147
Reaction score
432
Waziri wa Nishati, Mhe. Deogratius Ndejembi leo 20 Novemba, 2025 amekabidhiwa rasmi ofisi na aliyekuwa Naibu Waziri Mkuu na Waziri wa Nishati, Mhe. Dkt. Doto Mashaka Biteko kwenye ofisi za wizara zilizoko mtumba mkoani Dodoma, na kumshukuru Mhe. Biteko kwa utendaji wake wa kazi katika kipindi chote cha uongozi wake.

Waziri Ndejembi amesema katika kipindi cha uongozi wake, utendaji kwenye sekta ya nishati umekuwa kwa kiasi kikubwa na huduma za utendaji zimeboreshwa na tija kuonekana katika harakati za kukuza sekta ya nishati.

1763648202741.png

Waziri Ndejembi ameahidi atayaendeleza yote pale alipoishia Mhe.Biteko, ili kuhakikisha azma ya serikali na maono iliyonayo kufanikisha miradi ifikapo 2030 yanafikiwa.

Kwa upande wake, Mhe. Dkt. Biteko amempongeza Mhe. Deogratius Ndejembi kwa kuteuliwa kuwa Waziri wa Nishati na kumhakikishia kumpa ushirikiano wakati wowote katika kufanikisha maono makubwa ya Mheshimiwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan katika Sekta ya Nishati.

“Mengi niliyojifunza kipindi nikiwa Wizara ya Nishati lakini jambo kubwa zaidi ni sala zangu kwenu katika utekelezaji wa kazi zenu za kila siku“ amesema Biteko.

Halfla ya Makabidhiano hayo imehudhuriwa na Naibu Waziri wa Nishati, Mhe. Salome Makamba, Katibu Mkuu wa Wizara ya Nishati, Mha. Felchesmi Mramba, pamoja na viongozi waandamizi wa Wizara hiyo.
 
Kwanini amechelewa kukabidhi ofisi Kwa wakati,

Siku 3 tokea uwapisho,ofisi anakabidhi Leo

wakati Raisi Samia alisema , baada TU ya uwapisho ni kwenda kwenye kufanya majukumu ya kazi (ofisi).

Ay yeye alikuwa Bado hajatoa matunguli yake ofisini
KAZI (siasa), hizi. Zina Mambo
 
Back
Top Bottom