Uchaguzi 2020 Dkt Bashiru kutua Tabora

Mpekuzi Tanzania

JF-Expert Member
Mar 11, 2018
586
908
TAARIFA YA UJIO WA KATIBU MKUU WA CHAMA CHA MAPINDUZI DR BASHIRU ALLY KAKURWA MKOANI TABORA

Ndugu zangu wanaCCM tarehe 7 na 8 Disemba 2019 tutakua na ugeni wa katibu mkuu wa CCM katika mkoa wetu wa Tabora. Atakua na shughuli maalumu katika wilaya ya Nzega Jimbo la Nzega mjini.

Amealikwa kuwa mgeni Rasmi katika mkutano mkuu wa Jimbo la Nzega mjini.

Mapokezi ya kimkoa yatafanyika Wilaya ya IGUNGA saa 2:40 asubuhi tarehe 07.12.19 Jumamosi. Katibu mkuu atatembelea miradi na kuona utekelezaji wa ILANI ya CCM ulivyotekelezwa katika jimbo la Nzega mjini siku hiyohiyo ya Jumamosi .

Pia tarehe 07.12.19 Dr Bashiru atakutana na wafanyabiashara mbalimbali na ataendesha Harambee ilioandaliwa na mh BASHE kwa ajili ya kumalizia ujenzi wa Ukumbi wa kisasa wa CCM

Tarehe 08.12.19 atashiriki mkutano mkuu wa Jimbo akiwa ni mgeni Rasmi kusikiliza taarifa ya utekelezaji wa ILANI itakayowasilishwa na Mh HUSSEIN M. BASHE mbunge na Naibu Waziri wa Kilimo na Ushirika.

Katibu bora kabisa na mzalendo wa kweli wa CCM DR BASHIRU ALLY KAKURWA, Karibu sana mkoani Tabora

KIDUMU CHAMA CHA MAPINDUZI

Imetolewa na
Majaliwa Bilali
Katibu siasa na uenezi CCM Mkoa wa Tabora
 
Vipi tathimini yake kuhusu mafanikio ya ziara yake ya Tanzania Visiwani hasa kule Pemba. Aliweza kukijenga chama na kukifunika chama cha ACT Wazalendo?
 
Awe
Vipi tathimini yake kuhusu mafanikio ya ziara yake ya Tanzania Visiwani hasa kule Pemba. Aliweza kukijenga chama na kukifunika chama cha ACT Wazalendo?
Ameweka mitambo, subiri matokeo 2020 muhimu ACT wasijitowe tuu na kuweka mpira kwapani
 
Mahakamani kwa kujitakia,mikutano ya ndani ruksa,ruzuku na michango ya wabunge kila mwezi inalipia pango hili,upumbavu sana
Mikutano kwa CCM ruksa Wapinzani wao Mahakamani
tapatalk_1573313066845.jpeg
 
Back
Top Bottom