Dk. Wanyancha M/kiti Mfuko wa Barabara | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Dk. Wanyancha M/kiti Mfuko wa Barabara

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by lifeofmshaba, Jun 26, 2011.

 1. lifeofmshaba

  lifeofmshaba JF-Expert Member

  #1
  Jun 26, 2011
  Joined: Feb 19, 2011
  Messages: 868
  Likes Received: 7
  Trophy Points: 35
  RAIS Jakaya Kikwete amemteua Dk. James Wanyancha kuwa Mwenyekiti wa Bodi ya Mfuko wa Barabara (RFB) kwa kipindi cha miaka mitatu kuanzia Juni 3 mwaka huu.

  Kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa na Wizara ya Ujenzi iliyosainiwa na Katibu Mkuu wa Wizara hiyo, Balozi Herbert Mrango, uteuzi huo ni kwa mujibu wa kifungu namba 5-(1) (a) cha Sheria ya Bodi ya Mfuko wa Barabara namba 1 ya mwaka 1998.

  Katika taarifa yake, Balozi Mrango amemwelezea Dk. Wanyancha kuwa ana uzoefu mkubwa katika masuala ya utawala na uongozi, kwani amewahi kushika wadhifa wa Naibu Waziri katika Wizara ya Mifugo na Uvuvi hadi mwishoni mwa mwaka jana, wakati huo akiwa Mbunge wa Jimbo la Serengeti.

  Aidha, Dk. Wanyancha amewahi kuiwakilisha Tanzania katika Bunge la Afrika na kuitumikia
  Jumuiya ya Maendeleo ya Nchi za Kusini mwa Afrika (SADC) akiwa mtaalamu mshauri.
   
Loading...