GeniusBrain
JF-Expert Member
- Nov 3, 2010
- 4,315
- 309
KATIBU Mkuu wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema), Dk Willbroad Slaa amewataka viongozi wa dini nchini kufanya utafiti kabla ya kutoa matamko yao katika vyombo vya habari.Kauli hiyo ya Dk Slaa imekuja siku moja baada ya Sheikh Mkuu wa Tanzania , Mufti Issa bin Shaaban Simba kukishutumu chama hicho kwamba maandamano yake kinayofanya hivi sasa yana lengo la kuvuruga amani ya nchi.
Katibu Mkuu huyo wa Chadema alisema ameshangazwa na kauli iliyotolewa na Mufti Simba kuwa chama chake kina lengo la kuvuruga amani nchini.Nimeshangazwa sana na kauli ya Sheikh Mkuu, Mufti Simba aliyoitoa kwa vyombo vya habari.
Kimsingi kama alitaka kujua undani wa maandamano yetu angetuuliza kuliko kutoa tamko bila kujua hata undani wa Chadema, alisema na kuongeza kuwa baadhi ya viongozi wa dini wamekuwa wakitoa tamko bila ya kufanyia utafiti jambo ambalo linawafanya watoe maelezo yasiyo na ukweli na yanayolenga kuwapotosha na kuchochea chuki kwa wafuasi wake.Dk Slaa alisema Chadema inajua inachokifanya, hivyo kama mtu anahitaji kujua madhumuni ya maandamano yao ni vyema akawauliza ili
kitoe ufafanuzi kwa kuwa kila jambo liko wazi kwa maslahi ya wananchi wenyewe.Sioni haja ya kulumbana na kujibizana kila kukicha kupitia vyombo vya habari. Kama wana hoja ya msingi wailete sisi tutaijibu kwa hoja siyo kuongea mambo kwa mtazamo na propaganda za kisiasa. Unapozungumza ni lazima kuwe na utaratibu wa kutafiti unachokizungumza, alisema Dk Slaa.
Aliwataka viongozi wa dini kuhudhuria mikutano ya chama hicho ili kusikia na kujua kinachozungumzwa na Chadema kuliko kusubiri kusimuliwa na watu na kisha kuyaamini maneno yao.Alisema amelazimika kumjibu Mufti Simba kwa kuwa amesikitishwa na kauli hiyo ambayo alisema badala ya kuwasaidia Watanzania, inachochea chuki na kuruhusu ufisadi kuendelea.
Akizungumza na waandishi wa habari ofisini kwake Dar es Salaam juzi, Mufti Simba alisema: Wanasiasa wanataka kuivuruga nchi kwa visingizio kuwa wanataka kuilinda amani, hivyo Waislamu tumeamua kuvunja ukimya uliodumu kwa muda mrefu na kuamua kukekemea vitendo hivyo.Mjadala wa uhalali wa mikutano na maandamano ya Chadema uliibuliwa na Rais Jakaya Kikwete alipolihutubia taifa kupitia redio na televisheni mwishoni mwa Februari kwamba chama hicho cha upinzani kina lengo la kuleta machafuko nchini.
Kauli hiyo ilifuatiwa na onyo kutoka kwa Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais (Uhusiano na Uratibu), Steven Wassira kuwa Chadema kisije kuilaumu Serikali itakapokosa uvumilivu na kuanza kutumia dola kukishughulikia.Wakatihuo huo; Dk Slaa amesema ziara zinazofanywa na Rais Jakaya Kikwete katika wizara mbalimbali ni matunda ya maandamano ya chama hicho katika mikoa ya Kanda ya Ziwa.
Alisema Serikali imeanza kutekeleza madai mengi ambayo Chadema ilitaka iyafanyie kazi ndani ya siku tisa. Hata hivyo, alisema chama hicho kitaendelea kutia shinikizo hadi mambo yote yatakapokamilishwa.Hayo ni matunda ya maandamano yetu japo utekelezaji wake hauridhishi kwa kiwango tulichotaka.
Lakini imedhihirika kwamba mambo hayo yanaweza kupatiwa ufumbuzi. Inashangaza kuona wengine wanayaita maandamano kuwa ni ya kuvuruga amani, alisema.Alisema kuwa matunda mengine ya maandamano ya Chadema yaliyofanyika mkoani Mwanza ni tamko la Rais la kupunguza bei ya sukari kutoka Sh2,200 hadi Sh1,700.Rais Jakaya Kikwete anatembelea wizara mbalimbali kukagua utekelezaji wa maagizo ya yake.
we Slaa mpuuzi sana acha kudharau dini za wenzako, Pengo alipotoa maoni yake kuhusu maandamano alifanya utafiti lini? yani nyie mnaposifiwa hakuna comment yoyote ila mkikoselewa tuu,ndo mnakuja na matamko ya kipuuzi! hiyo siasa badilikeni na acheni ulimbukeni coz mnatubero sana
we Slaa mpuuzi sana acha kudharau dini za wenzako, Pengo alipotoa maoni yake kuhusu maandamano alifanya utafiti lini? yani nyie mnaposifiwa hakuna comment yoyote ila mkikoselewa tuu,ndo mnakuja na matamko ya kipuuzi! hiyo siasa badilikeni na acheni ulimbukeni coz mnatubero sana
Wewe hujui kusoma, umeona wapi Dr Slaa akizungumzia juu ya dini bali anaongea juu na Shekhe; wewe ndio mdini sana na tena si msttarabu kwani kutukana ni part of argument. I wonder why mods keep people like you on this forum, you place should be vijiweni ambako unaweza kuwa huru ku gossip na kutukana japo nayo hiyo sio ustaarabu lakini kwa vile huna, such a place will surely suti you. Otherwise mods please ban this creature who insults and insults people we respect????? Abomination
Tunashukuru kwa kuwasilisha maneno ya kadinali Pengo kwa niaba yake, Slaa acha kutumika na wakatoliki
read btn lines anawezaje kusema muft hakufanya utafiti?? ana uhakika gani kama sio dharau kwa waislamu wote?? Slaa needs to ask for the apology,ule ulikuwa ni mkutano wa masheikh na maulamaa wa nchi nzima waliokuwa wakijdaili hali ya siasa nchini libya na Tanzania kwahiyo muft Simba alitoa hitimisho ya yaliyoongelewa kwahiyo slaa kwa maana nyingine ameudharau mkutano wote ule! lazima aombe msamahaWewe hujui kusoma, umeona wapi Dr Slaa akizungumzia juu ya dini bali anaongea juu na Shekhe; wewe ndio mdini sana na tena si msttarabu kwani kutukana ni part of argument. I wonder why mods keep people like you on this forum, you place should be vijiweni ambako unaweza kuwa huru ku gossip na kutukana japo nayo hiyo sio ustaarabu lakini kwa vile huna, such a place will surely suti you. Otherwise mods please ban this creature who insults and insults people we respect????? Abomination
read btn lines anawezaje kusema muft hakufanya utafiti?? ana uhakika gani kama sio dharau kwa waislamu wote?? Slaa needs to ask for the apology,ule ulikuwa ni mkutano wa masheikh na maulamaa wa nchi nzima waliokuwa wakijdaili hali ya siasa nchini libya na Tanzania kwahiyo muft Simba alitoa hitimisho ya yaliyoongelewa kwahiyo slaa kwa maana nyingine ameudharau mkutano wote ule! lazima aombe msamaha
Genetic Modified Brain
wakatoliki wamekukosea nini jamani....?
KATIBU
Katibu Mkuu huyo wa Chadema alisema ameshangazwa na kauli iliyotolewa na Mufti Simba kuwa chama chake kina lengo la kuvuruga amani nchini.Nimeshangazwa sana na kauli ya Sheikh Mkuu, Mufti Simba aliyoitoa kwa vyombo vya habari.
Kimsingi kama alitaka kujua undani wa maandamano yetu angetuuliza kuliko kutoa tamko bila kujua hata undani wa Chadema, alisema na kuongeza kuwa baadhi ya viongozi wa dini wamekuwa wakitoa tamko bila ya kufanyia utafiti jambo ambalo linawafanya watoe maelezo yasiyo na ukweli na yanayolenga kuwapotosha na kuchochea chuki kwa wafuasi wake.Dk Slaa alisema Chadema inajua inachokifanya, hivyo kama mtu anahitaji kujua madhumuni ya maandamano yao ni vyema akawauliza
.
you fool,read btn lines anawezaje kusema muft hakufanya utafiti?? ana uhakika gani kama sio dharau kwa waislamu wote?? Slaa needs to ask for the apology,ule ulikuwa ni mkutano wa masheikh na maulamaa wa nchi nzima waliokuwa wakijdaili hali ya siasa nchini libya na Tanzania kwahiyo muft Simba alitoa hitimisho ya yaliyoongelewa kwahiyo slaa kwa maana nyingine ameudharau mkutano wote ule! lazima aombe msamaha
we Slaa mpuuzi sana acha kudharau dini za wenzako, Pengo alipotoa maoni yake kuhusu maandamano alifanya utafiti lini? yani nyie mnaposifiwa hakuna comment yoyote ila mkikoselewa tuu,ndo mnakuja na matamko ya kipuuzi! hiyo siasa badilikeni na acheni ulimbukeni coz mnatubero sana
My friend, I am not a fool...and your insults wont do me any harm except they show me that you have no capacity to reason and follow arguments, and for that I truly pity you...to say that someone needs to do research of his utterance does not have any religious connotation...kwamba tu mtu ni mufti does not place such person in a position that all his utterances will be taken at face value...think about it, go to school, get wisdom and understanding...then write arguments na sio matusi...matusi ni dalili ya kukosa values..sijui ulilelewa magangeni?
hawa wameanza kuchanganyikiwa,Gadafi kungo'lewa unafikiri watakuwa na amani.kwani jeuri yote wameitoa huko.you fool,read btn lines anawezaje kusema muft hakufanya utafiti?? ana uhakika gani kama sio dharau kwa waislamu wote?? Slaa needs to ask for the apology,ule ulikuwa ni mkutano wa masheikh na maulamaa wa nchi nzima waliokuwa wakijdaili hali ya siasa nchini libya na Tanzania kwahiyo muft Simba alitoa hitimisho ya yaliyoongelewa kwahiyo slaa kwa maana nyingine ameudharau mkutano wote ule! lazima aombe msamaha
okey the WISEMAN,am asking you did Pengo make any research? how come his statement was not welcomed with doubts? be fair na sio kuegemea upande fulani
Tunashukuru kwa kuwasilisha maneno ya kadinali Pengo kwa niaba yake, Slaa acha kutumika na wakatoliki