Mzito Kabwela
JF-Expert Member
- Nov 28, 2009
- 18,857
- 7,617
Nijuavyo Ubalozi ni utumishi wa Umma unaolindwa kwa sheria za utumishi za nchi.
Dk. Slaa aliyekuwa katibu Mkuu wa Chadema ana miaka 70 sasa, amevuka kikomo cha miaka 60 cha kuendelea kuwa mtumishi wa Umma.
Je si sahihi kuwa sheria imevunjwa kwa kumwacha aendelee kuwa balozi?
Kwa kuwa tayari amezeeka imefika wakati anapoteza kumbukumbu jambo ambalo ni hatari sana kwa shughuli za kidiplomasia.
Mathalan, Dk. Slaa wakati alipokuwa KM Chadema alizunguka nchi nzima kuikosoa Serikali, ana account hapa JF kwa jina lake ambapo kila mara alikuwa akidondosha 'madini' humu. Leo anakataza watu wasikosoe mtandaoni..amesahau kazi aliyokuwa akiifanya kwa miaka zaidi ya 15 alipokuwa siasa za Upinzani.
Dk Slaa ni msahaulifu sana kwa sababu ya Umri wake kiasi kwamba anafananisha siasa za Tanzania kama za Sweden, anadhani huku kwetu wapo wa kuwasemea wanaoishi kwenye nyumba za Tembe kama alivyokuwa anafanya, anadhani wanahabari wapo huru kufanya kazi, amesahau Marehemu Mwangosi alivyouawa na Hajui kabisa yaliyomkuta Kabendera.
Dk.Slaa amesahau alivyokuwa akiitwa Padri Mzinzi...alivyokejeliwa humu kwa kuwana PhD ya Kanoni na hakutikisika kwakuwa alisema yeye kuwa ana ngozi ngumu. Ameshindwa kuwashauri wanaomfanya ale vizuri hivi sasa na wao kuwa na ngozi ngumu.
Dk. Slaa amesahau alivyokuwa huru kumsema Katibu Mkuu fulani wa CCM kuwa alifumaniwa akimla mtoto wa Shule wakati KM huyobwa CCM akiwa Kigoma....alikuwa huru kusema.
Slaa amesahau alipokuwa anayaanika madudu ya Deep Green, Kagoda na mengineyo.....
Kwa nini anaendelea kuwepo ubalozini mtu aliyepitiliza umri wa kustaafu? Madhara ya kumweka mzee ofisi za umma moja wapo ni usahaulifu.