[B
Wednesday, 29 September 2010 18:52
Joseph Lyimo, Simanjiro
MGOMBEA wa urais kwa tiketi ya Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema), Dk Willibrod Slaa kuwa gumzo kwa wakazi wa Mkoa wa Manyara imezidi kuwapa maumivu makali viongozi wa CCM mkoani humo na kusababisha kufanya vikao vya ndani hadi saa 7:00 usiku.
Viongozi hao wa CCM Mkoa wa Manyara wakiongozwa na katibu wake, Avelin Mushi, Katibu wa Wazazi Mkoa, George Kijaji, Katibu wa UWT Mkoa,Grace Maholelo na wabunge wateule wa viti maalumu mkoa huo, Dorah Mushi na Martha Umbulla na mgombea ubunge katika Jimbo la Simanjiro, Christopher Ole Sendeka wanakutana muda huo, kujadili hilo ni jinsi gani watakabiliana na Chadema.
Wengine wanaokutana katika mkutano huo ni kamati ya siasa ya Wilaya ya Simanjiro,wagombea udiwani wa CCM na wajumbe wa Halmashauri ya CCM katika Kata ya Mererani.
Katika vikao hivyo vilivyofanyika juzi kuanzia saa 11:00 jioni hadi saa 7:00 usiku kwenye ukumbi wa Manyara Inn uliopo mji mdogo wa Mererani wilayani Simanjiro, pia ulihudhuriwa na mkuu wa wilaya hiyo Khalid Mandia ambaye ni Mjumbe wa Kamati ya Siasa ya CCM wilayani humo.
Mmoja kati ya wajumbe wa vikao hivyo ambaye hakupenda kutaja jina lake kwa vile siyo msemaji wa chama hicho, alisema kuwa upepo wa kisiasa siyo mzuri mkoani Manyara kwa CCM, hivyo uongozi wa mkoa huo umejadili hilo ili kunusuru hali hiyo.
Alisema nyota ya kisiasa mkoani Manyara kwa mgombea urais wa Chadema - Dr. Slaa.
SOURCE: Mwananchi