Dk.Philip Mpango, kwa habari hii ya kupokea ushauri wa Wakenya, umenishangaza sana

Salary Slip

JF-Expert Member
Apr 3, 2012
48,684
149,889
Nchi 30 za Ulaya zimeiandikia barua Serikali ya Tanzania zikiomba ifikirie upya Kodi ya Ongezeko la Thamani (VAT) kwenye shughuli za utalii iliyoanza mwezi huu au isianze kutumika hadi mwaka ujao.

Waziri wa Fedha na Mipango, Dk Philip Mpango amesema walipata wazo la kuanzisha kodi hiyo kutoka nchi jirani ya Kenya.

Wakati sheria hiyo ikianza kutumika nchini, nchi hizo za Ulaya ambazo ni wadau wakuu katika sekta ya utalii zimemwandikia barua hiyo Dk Mpango, naibu wake, Dk Ashatu Kijaji na Waziri wa Maliasili na Utalii, Profesa Jumanne Maghembe.

Chama cha Kitaifa wa Mawakala wa Usafiri na Wasimamizi wa Utalii (ECIAA) kutoka nchi 30 za Ulaya ndicho kinachoziwakilisha kampuni zaidi ya 70,000 za utalii barani humo.

Nchi hizo ndizo zinazotoa asilimia 50 ya watalii wote duniani.

Chanzo:Mwananchi online

Nimeshindwa kuamini hii habari hasa ukizingatia Wakenya ni washindani wetu wakubwa kwenye hii biashara ya utalii.

Alafu hivi hawa Wakenya wao wana hii kodi?Je,ni kweli wao hawana/waliifuta kama navyosikia?Hata kama wanayo, ilikuwa sahihi kupokea wazo hili?

Wabunge mlioridhia hii tozo naji mjitafakari kama mna tosha!
 
Ufaransa (French) inaleta watalii wengi sana Tanzania (Middle class) na Luxury wachache..... French Travel Agents reacted on sudden VAT...Abrupt kukurupuka ...French people do plan travel budget, Is not like Kuongeza bei ya sukari

Foreign body wades into tourism tax row

UK nao wamecomplain......TATIZO sio kulipa VAT, tatizo ni ghafla kukurupuka

{{metaTags.other['og:title']}}

Dr. Mpango anachukua ushauri Kenya

Maghembe anasema hafuati mambo ya Kenya....maana Kenya sio Koloni letu

Je..Rwanda ni Coloni letu?

Mwendo Kasi Economy Tourism

VAT Mwendo Kasi
 
Unazungumzia utalii tuh hata kwenye usafirshaji wa copper kutoka Zambia wameweka VAT kinachotokea sasa watanzania tumenyan'ganywa tender ya copper na sasa wazambia wanasafirsha copper yao kupita bandari ya Msumbiji mbona tunaisoma namba
 
mnh.....kali.
Lakini kwani hao wazungu shida yao nini si walipe kodi tu!!!
 
Kitu ambacho serikali haijazingatia ni kwamba watalii wanaotoka nnje asilimia zaidi ya 90% kufanya bookings zao angalau miezi 6 kabla ya safari, sasa ni vigumu kumwambia mgeni ghafla kwamba aongeze hela ya malipo zaidi ya aliyofanya hapo kabla. Inabidi gharama hizo za ziada zilipwe na kampuni za Safari pamoja mawakala wao hapa Tanzania.
 
Ufaransa (French) inaleta watalii wengi sana Tanzania (Middle class) na Luxury wachache..... French Travel Agents reacted on sudden VAT...Abrupt kukurupuka ...French people do plan travel budget, Is not like Kuongeza bei ya sukari

Foreign body wades into tourism tax row

UK nao wamecomplain......TATIZO sio kulipa VAT, tatizo ni ghafla kukurupuka

{{metaTags.other['og:title']}}

Dr. Mpango anachukua ushauri Kenya

Maghembe anasema hafuati mambo ya Kenya....maana Kenya sio Koloni letu

Je..Rwanda ni Coloni letu?

Mwendo Kasi Economy Tourism

VAT Mwendo Kasi
Huu mtifuano utatupeleka shimoni.
 
Watanzania tunapenda sana mteremko,embu tulipege tu hizo kodi ili taifa lipate mapato ya kutosha kujiendesha kuliko kulialial tu bial sababu ya msingi,mimi nadhani muhimu hapa na hivi vilio vyetu vingekuwa na tija kama tu serikali ambayo hivi sasa inakusanya kodi kila mahali ikashindwa kuhakikisha walu kila kijiji kina kuwa na zahanati ya uhakika hadi ifikapo mwaka 2020,ikashindwa kuhakikisha maisha ya watumishi wa umma yanakuwa nafuu hadi mwaka 2020,uchumi wa nchi unakuwa ikiwemo miundombinu ya kisasa hadi mwaka 2020,hapo tunaweza kulia tena sana na tutamlaami aliyepandisha kodi then pesa anakula yeye badala ya kuzitumia kwa jamii,ila kwa sasa chapa kazi lipa kodi kila inapostahili
 
mnh.....kali.
Lakini kwani hao wazungu shida yao nini si walipe kodi tu!!!

Hee, magazeti na magazeti yameandika bado huji tatizo ni nini?

Watanzania tuwe na tabia ya kujisomea

TATIZO sio kulipa ndugu.....Watu wapo tayari kulipa na kodi ni kila mahali duniani...

Tatizo ni kuwa wazungu walishalipia safari zao za Kuanzia July 01 had December 2016....Sasa ukikurupuka Mwendo kasi na kusema mzungu aongeze 18%.....ni kukosa uaminifu....

Serikali imepanga kuongeza VAT, sawa.......ni mpango mzuri.......ingeanza mafunzo kwa TRA, na Mamlaka zake zingejipanga kutoa risiti za VAT....... Tuache mwendo kasi
 
WATANZANIA TUNAPENDA SANA MTEREMKO,EMBU TULIPEGE TU HIZO KODI ILI TAIFA LIPATE MAPATO YA KUTOSHA KUJIENDESHA KULIKO KULIALIAL TU BIAL SABABU YA MSINGI,MIMI NADHANI MUHIMU HAPA NA HIVI VILIO VYETU VINGEKUWA NA TIJA KAMA TU SERIKALI AMBAYO HIVI SASA INAKUSANYA KODI KILA MAHALI IKASHINDWA KUHAKIKISHA WALU KILA KIJIJI KINA KUWA NA ZAHANATI YA UHAKIKA HADI IFIKAPO MWAKA 2020,IKASHINDWA KUHAKIKISHA MAISHA YA WATUMISHI WA UMMA YANAKUWA NAFUU HADI MWAKA 2020,UCHUMI WA NCHI UNAKUWA IKIWEMO MIUNDOMBINU YA KISASA HADI MWAKA 2020,HAPO TUNAWEZA KULIA TENA SANA NA TUTAMLAAMI ALIYEPANDISHA KODI THEN PESA ANAKULA YEYE BADALA YA KUZITUMIA KWA JAMII,ILA KWA SASA CHAPA KAZI LIPA KODI KILA INAPOSTAHILI

VAT inatakiwa ianze utekelezaji effectively 2017 July.....

Serikali imepanga kuongeza VAT, sawa.......ni mpango mzuri.......ingeanza mafunzo kwa TRA, na Mamlaka zake zingejipanga kutoa risiti za VAT....... Tuache mwendo kasi
 
mikurupuko ya mwendokasi
Ukiambiwa siku hizi chupi inavaliwa kichwani utavaa? unapokea ushauri wa kibiashara kutoka kwa mshindani mwenzio tena mwenye mtaji mdogo na wewe unakubali!! kumbe sisi bado sana tena sana yani hatuchanganyi na zetu.
 
Athari zinaonekana dhahiri. Magari ya utalii yanayoenda Ngorongoro na Serengeti yamepungua.....noma sana. Wajasiriamali wadogo na wakati wanaambulia patupu. Unajua hapa Arusha utalii haunufaishi wenye wakampuni ya tour alone...raia mob wanategemea michongo ya utalii kuendesha life. Hii mambo inazingua.....tatizo waTz na sisi mashabiki mandazi......whenever we are given opportunity to select leaders we select hyena to take care of goats. Hawa viongozi hawapo kusaidia wapo kutimiza ndoto zao waitwe fulani naye ni kiongozi. Watanzania tunataka "good life" sio kuvuruga mambo.
 
Mambumbumbu wa uchumi sio kila kitu kulaumu tu
Hizo nchi za ulaya mbona zinatoa subsidy kwa wakulima wao,bei za mazao zinaanguka duniania mbona hawasikilizi kilio chetu?
Uzuri wa Tanzania mlima kilimanjaro hauozi,wasipokuja watalii tutategemea gesi,sasa hivi tumegundua mpaka gesi ya kuendeshea mapigo ya moyo wa mwandamu!
 
Ukiambiwa siku hizi chupi inavaliwa kichwani utavaa? unapokea ushauri wa kibiashara kutoka kwa mshindani mwenzio tena mwenye mtaji mdogo na wewe unakubali!! kumbe sisi bado sana tena sana yani hatuchanganyi na zetu.
Kuna watu wanatakiwa kuongozwa milele. Naamini na nitaamini hili milele
 
TATIZO sio kulipa ndugu.....Watu wapo tayari kulipa na kodi ni kila mahali duniani...

Tatizo ni kuwa wazungu walishalipia safari zao za Kuanzia July 01 had December 2016....Sasa ukikurupuka Mwendo kasi na kusema mzungu aongeze 18%.....ni kukosa uaminifu....

VAT inatakiwa ianze utekelezaji effectively 2017 July.....

Serikali imepanga kuongeza VAT, sawa.......ni mpango mzuri.......ingeanza mafunzo kwa TRA, na Mamlaka zake zingejipanga kutoa risiti za VAT....... Tuache mwendo kasi
ni kweli,ingefaa kuwa hivyo mkuu,ila nadhani ni suala la muda tu na kuwaelewesha hao wadhungu ili wajue kuwa hali ya mambo imebadilika ,kama hawataelewa inawezekana wakaja hata hiyo mwakani pamoja na wenzetu wale wake kiratiba ,ila kama wanania wanakuja tu hata hiyo makani kwani mwaka hata hivyo si umeisha huu?
 
WATANZANIA TUNAPENDA SANA MTEREMKO,EMBU TULIPEGE TU HIZO KODI ILI TAIFA LIPATE MAPATO YA KUTOSHA KUJIENDESHA KULIKO KULIALIAL TU BIAL SABABU YA MSINGI,MIMI NADHANI MUHIMU HAPA NA HIVI VILIO VYETU VINGEKUWA NA TIJA KAMA TU SERIKALI AMBAYO HIVI SASA INAKUSANYA KODI KILA MAHALI IKASHINDWA KUHAKIKISHA WALU KILA KIJIJI KINA KUWA NA ZAHANATI YA UHAKIKA HADI IFIKAPO MWAKA 2020,IKASHINDWA KUHAKIKISHA MAISHA YA WATUMISHI WA UMMA YANAKUWA NAFUU HADI MWAKA 2020,UCHUMI WA NCHI UNAKUWA IKIWEMO MIUNDOMBINU YA KISASA HADI MWAKA 2020,HAPO TUNAWEZA KULIA TENA SANA NA TUTAMLAAMI ALIYEPANDISHA KODI THEN PESA ANAKULA YEYE BADALA YA KUZITUMIA KWA JAMII,ILA KWA SASA CHAPA KAZI LIPA KODI KILA INAPOSTAHILI
Ujinga peleka kwenu
 
Back
Top Bottom