DK. Mwakyembe: Nishaonja kifo siogopi kufa | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

DK. Mwakyembe: Nishaonja kifo siogopi kufa

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by MziziMkavu, Jun 9, 2012.

 1. MziziMkavu

  MziziMkavu JF-Expert Member

  #1
  Jun 9, 2012
  Joined: Feb 3, 2009
  Messages: 39,616
  Likes Received: 4,617
  Trophy Points: 280
  Ndio Waziri wa Uchukuzi, Dk.Harrison Mwakyembe hata mimi ninakuunga mkono fagio lako la chuma lazima lifanye kazi safisha kabisa Wizara yako hongera sana na Mwenyeezi Mungu akulinde na hao Maaduwi zako Mafisadi inshallah. Tunataka Viongozi Bora Mashujaa kama nyinyi katika nchi yetu iliyokuwa na viongozi Mafisadi.
   
 2. LiverpoolFC

  LiverpoolFC JF-Expert Member

  #2
  Jun 9, 2012
  Joined: Apr 12, 2011
  Messages: 11,001
  Likes Received: 153
  Trophy Points: 160
  Huyu ni jembe!

  Awe makini tu na mafisadi alioko nao
   
 3. MziziMkavu

  MziziMkavu JF-Expert Member

  #3
  Jun 9, 2012
  Joined: Feb 3, 2009
  Messages: 39,616
  Likes Received: 4,617
  Trophy Points: 280
  Mwenyeezi Mungu atamlinda tu inshallah. yupo kwenye haki na anatetea haki za walala hoi .
   
 4. k

  kitero JF-Expert Member

  #4
  Jun 9, 2012
  Joined: Feb 21, 2012
  Messages: 563
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Ni mpiganaji na mpammbanaji mzuri sana mampongeza kwa kazi zake.Ila huwezi kupambana na adui yako aliye nje na wewe ukiwa ndani ya chumba chako utapambana naye ukiwa katika uwanja wa mpambano.
   
 5. MziziMkavu

  MziziMkavu JF-Expert Member

  #5
  Jun 9, 2012
  Joined: Feb 3, 2009
  Messages: 39,616
  Likes Received: 4,617
  Trophy Points: 280
  Una maana gani unavyosema hivyo mkuu. kitero
   
  Last edited by a moderator: Jan 4, 2016
 6. The Boss

  The Boss JF-Expert Member

  #6
  Jun 9, 2012
  Joined: Aug 18, 2009
  Messages: 37,822
  Likes Received: 22,467
  Trophy Points: 280
  masifa boy again..
   
 7. Graph Theory

  Graph Theory JF-Expert Member

  #7
  Jun 9, 2012
  Joined: Jul 2, 2011
  Messages: 3,809
  Likes Received: 1,129
  Trophy Points: 280
  Hata Yesu kristo aliwahi sema Msiogope wauuao mwili wasiweze kuua na roho bali mwogopeni yeye awezaye kuua vyote, mwili na roho katika jehanamu.
  The unseen is illustrated by the seen.
   
 8. Inanambo

  Inanambo JF-Expert Member

  #8
  Jun 9, 2012
  Joined: Jun 26, 2011
  Messages: 2,867
  Likes Received: 1,149
  Trophy Points: 280
  Nakukubali Mwakyembe hakika wewe ni jembe la ukweli. Sijui walikuacha wapi siku zote hizo waziri wetu. Mungu akutangulie katika kila ufanyalo. usiache jiwe lolote bila kuligeuza. tembelea TAASISI zote za Wizaara yako na omba kuongea na wafanyakazi wote siyo unaishia kwa Mabosi. utayapata mengi anzia Promosheni, training na Nauli zetu za likizo.
   
 9. kibol

  kibol JF-Expert Member

  #9
  Jun 9, 2012
  Joined: Apr 24, 2012
  Messages: 3,142
  Likes Received: 382
  Trophy Points: 180
  Bila maamuzi magumu na viongozi walio-commited nchi hatutoendelea katu.bravo mwakyembe
   
 10. MziziMkavu

  MziziMkavu JF-Expert Member

  #10
  Jun 9, 2012
  Joined: Feb 3, 2009
  Messages: 39,616
  Likes Received: 4,617
  Trophy Points: 280
  [​IMG]

  Waziri wa Uchukuzi, Dk. Harrison Mwakyembe

  Moto wa mawaziri wa kuwashughulikia watendaji na watumishi wa serikali wanaotuhumiwa kwa makosa mbalimbali, ikiwamo kushindwa kuwajibika katika maeneo yao ya kazi, umezidi kusambaa, ambapo safari hii Waziri wa Uchukuzi, Dk. Harrison Mwakyembe, ametengua uteuzi wa Kaimu Mkurugenzi Mtendaji wa Shirika la Ndege Tanzania (ATCL), Paul Chizi.


  Pia amewasimamisha kazi watumishi wengine wanne wa vitengo vya uhandisi, sheria, fedha na biashara vya shirika hilo.


  Hatua hiyo imechukuliwa na Waziri Mwakyembe zikiwa zimepita siku chache baada ya mawaziri wengine; Dk. Abdallah Kigoda (Viwanda na Biashara) na Balozi Khamis Kagasheki (Maliasili na Utalii), kuwasimamisha kazi viongozi waandamizi wa sekta zinazogusa wizara wanazoziongoza.


  Katibu Mkuu wa Wizara ya Uchukuzi, Omar Chambo, alisema kupitia taarifa yake kwa vyombo vya habari jana kuwa hatua dhidi ya Chizi imechukuliwa kutokana na uteuzi wake kutofuata sheria, kanuni na taratibu za utumishi wa umma.


  “Hivyo, kupitia Sheria Na. 8 ya mwaka 2008 na kanuni za utumishi wa umma za mwaka 2003 Na. 17 (4), Mheshimiwa Dk. Harrison Mwakyembe, Waziri wa Uchukuzi ametengua uteuzi wa Kaimu Mkurugenzi Mtendaji wa Shirika la Ndege Tanzania kuanzia Juni 5, 2012,” alisema Chambo.


  Alisema kanuni hiyo inaeleza bayana kuwa kama mtumishi atakuwa ameteuliwa kwa kukiuka kifungu cha 17 (1) au (3) cha kanuni za utumishi wa umma za mwaka 2003, itakuwa na mamlaka ya uteuzi kutengua uteuzi wa utumishi wake mara moja.


  KAPTENI LUSAJO ATEULIWA


  Kutokana na hatua hiyo, Waziri Mwakyembe amemteua Kapteni Lusajo Lazaro, kukaimu nafasi ya Mkurugenzi Mtendaji wa ATCL kuanzia jana.


  Chambo alisema Waziri Mwakyembe pia amewasimamisha kazi watumishi wengine wanne wa ATCL, akiwamo Kaimu Mkurugenzi wa Uhandisi wa Shirika hilo, John Ringo, kutokana na ukiukwaji wa sheria, kanuni na taratibu za utumishi wa umma.


  Alisema ukiukwaji huo wa sheria, kanuni na taratibu za utumishi wa umma, ulitishia uhai wa chombo hicho muhimu cha taifa.


  Wengine waliosimamishwa, ni Amini Mziray (Mwanasheria), Justus Bashara (Kaimu Mkurugenzi wa Fedha) na Josephat Kagirwa (Kaimu Mkurugenzi wa Biashara).


  Alisema kupitia ukiukwaji huo, itaundwa kamati ya wajumbe watatu wenye uelewa wa mambo ya fedha na sheria ili kuchunguza matumizi ya fedha iliyopokelewa kuanzia mwanzoni mwa Mei, mwaka huu.


  CHIZI AZUNGUMZA


  Saa chache baadaye jana, Chizi alinukuliwa na Televisheni ya ITV akisema aliteuliwa kukaimu nafasi hiyo Agosti, mwaka jana, hivyo amepokea na anakubaliana na uamuzi uliochukuliwa dhidi yake.


  Kabla ya uteuzi wake, ATCL ilishindwa kuendesha shughuli zake, hivyo akateuliwa kurudisha hadhi ya shirika hilo na kwamba alijitahidi kufanya kazi hiyo kwa uwezo wake.


  “Kama uteuzi umetenguliwa nashukuru kwa hilo,” alisema Chizi na kuongeza kabla ya uteuzi wake kutenguliwa alikuwa tayari kishaingia mkataba wa kununua ndege ya pili ya shirika.


  “Nawashukuru Watanzania kwa ushirikiano, hususan vyombo vya habari na wote waliokuwa wakifurahia huduma za shirika. Nitachangia kwa njia nyingine ambazo nchi itaona zinasaidia,” alisema Chizi.


  Mei 17, mwaka huu, Waziri Kigoda aliiagiza Bodi ya Shirika la Viwango Tanzania (TBS) kumsimamisha kazi Mkurugenzi wake Mkuu, Charles Ekelege.


  Hatua hiyo ilichukuliwa dhidi ya Ekelege kupisha taratibu za kisheria, ikiwamo kufanyika uchunguzi dhidi yake.


  Waziri Kigoda alisema moja ya sababu iliyomfanya Rais Jakaya kikwete afanye mabadiliko ya uongozi katika wizara hiyo, ilikuwa ni TBS, baada ya kuwapo mjadala mkubwa bungeni kuhusu utendaji wake.
  Wakati akitangaza mabadiliko ya Baraza lake la Mawaziri Mei 4, mwaka huu, Rais Kikwete alizungumzia azma ya serikali kuchukua hatua kwa watendaji wengine wa serikali na taasisi zake ambao alisema ni chanzo cha mabadiliko hayo.


  Kikwete alisema mawaziri wamekuwa wakijiuzulu hata kwa makosa ambayo si yao na kwamba serikali itaanza kuchukua hatua kwa watendaji, wakiwamo makatibu wakuu, wakurugenzi wa wizara, watendaji wakuu wa mashirika na taasisi za umma pamoja na bodi za mashirika husika.


  Kadhalika, Mei 29, mwaka huu. Balozi Kagasheki ambaye awali alikaririwa akisema yuko katika vita kali dhidi ya wahujumu wa wanyamapori, aliwasimamisha kazi vigogo Mamlaka ya Hifadhi za Taifa (Tanapa) pamoja na askari 28 wa wanyamapori wa Hifadhi ya Taifa ya Serengeti (Senapa).


  Hatua hiyo ilichukuliwa na Waziri Kagasheki kutokana na vifo vya faru wawili vilivyoripotiwa hivi karibuni.

  CHANZO: NIPASHE
   
 11. Oluoch

  Oluoch Senior Member

  #11
  Jun 9, 2012
  Joined: Aug 30, 2010
  Messages: 134
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Kila la heri Ndugu Mwakyembe,Mungu azidi kukulinda na kukubariki. Naamini uzalendo wako utaleta tija kubwa kwa taifa kwani wewe u mtu wa vitendo zaidi kuliko maneno.
   
 12. B

  Bob G JF Bronze Member

  #12
  Jun 9, 2012
  Joined: Oct 5, 2011
  Messages: 2,354
  Likes Received: 10
  Trophy Points: 135
  Dr Mwakyembe jembe ila hofu yangu kuambiwa na wakubwa zake kuwa awe na huruma kama Dr magufuli alivofungishwa Break na wenyewe,
   
 13. B

  Bob G JF Bronze Member

  #13
  Jun 9, 2012
  Joined: Oct 5, 2011
  Messages: 2,354
  Likes Received: 10
  Trophy Points: 135
  Wapo viongozi wachache ccm wenye uthubutu Dr Mwakyembe ni mmoja ya viongozi wenye uwezo wa kufanya na kuamua na kusimamia kile anacho amini ni haki na sawa kufanya bila kutumwa, na mafisadi waliliona hilo wakaamua Kumtia Sumu, Wote tuna kufa na tuta kufa. Mwache Mungu aamue Hitima ya Maisha yetu na si Wezi na MAFISADI
   
 14. harakat

  harakat JF-Expert Member

  #14
  Jun 14, 2012
  Joined: Jul 4, 2011
  Messages: 2,908
  Likes Received: 761
  Trophy Points: 280
  BAADA ya kusafiri kwa treni kutoka Dar es Salaam hadi Dodoma, Waziri wa Uchukuzi, Dk Harrison Mwakyembe amebaini hujuma nzito katika Shirika la Reli Tanzania (TRL) ikiwamo ofisa mmoja kuwaibia abiria kwa kughushi viwango vya nauli na ameagiza afukuzwe kazi.

  Licha ya kuagiza kutimuliwa kwa ofisa huyo, pia alitangaza kuandaliwa utaratibu wa kufanya mabadiliko kadhaa katika kuboresha usafiri huo, ikiwamo kuondoa malipo ya nusu nauli kwa watoto wadogo kuanzia miaka mitatu hadi miaka 10 na pia kuondolewa kwa utaratibu wa malipo ya mizigo midogo ya abiria.

  Juzi, Dk Mwakyembe ambaye tayari amewang’oa vigogo wanne wa Shirika la Ndege Tanzania (ATCL), aliamua kusafiri kwa treni hadi Dodoma akitokea Dar es Salaam ili kujionea utendaji kazi wa shirika hilo.

  Offisa wa Serikali anawaibia watu vijisenti kwa kudalalia nauli ya Treni jamani huyu si ana kipaji cha udalali jamani si atadalalia hata tuuze vichwa vya treni ili ale cha juuuu,Mwizi ni mwizi tu haijalishi ni afisa wa ikulu au Trl wala nini .
  Tunahitaji watu wa maamuzi magumu zaidi ya haya ya mwakyembe ili keki ya Taifa hili ionekane na kila mtu.
   
 15. MANGUNGO

  MANGUNGO JF-Expert Member

  #15
  Jun 14, 2012
  Joined: Aug 30, 2011
  Messages: 1,538
  Likes Received: 5
  Trophy Points: 133
  Ni vizuri lakini vijidagaa ndio siku zote wanaangaika navyo!aanzie huko wizarani aje mpaka chini sio aanze chini aje juu,pongezi kwake ila magamba hawapendi utendaji wa aina hiyo hawe makini wasimfanye kama samweli 6
   
 16. harakat

  harakat JF-Expert Member

  #16
  Jun 14, 2012
  Joined: Jul 4, 2011
  Messages: 2,908
  Likes Received: 761
  Trophy Points: 280
  hawakuishia hapo waliendelea kugundua mahujuma mengine haya
  Hujuma
  Naibu Waziri wa Uchukuzi, Dk Charles Tzeba ambaye allimpokea Dk Mwakyembe alisema licha ya kuwepo hujuma katika nauli za abiria, pia wamebaini hujuma kubwa katika mizigo inayosafirishwa kwa reli katika mashirika yote ya TRC na Shirika la Tanzania na Zambia (Tazara).

  Alisema maofisa wasio waadilifu wa mashirika hayo, wamekuwa wakisafirisha mizigo mingi lakini inayoandikiwa na kulipwa serikalini ni ile yenye uzito mdogo.

  "Utakuta mzigo wa tani 40 hadi 60 unaandikiwa tani 10 au 20 fedha nyingine zinaingia mifukoni mwa wajanja, hatutakubali jambo hili," alisema Dk Tzeba
  Alisema yeye na waziri wake, pamoja na maofisa wengine, watakuwa wakisafiri kwa kushtukiza kwa reli mara kwa mara ili kubaini hujuma zote na kuwachukulia hatua wahusika mara moja.
  "Mimi nilikuja hapa Dodoma kwa kiberenge na baadhi ya wabunge wa kamati ya miundombinu na leo amekuja waziri kwa treni hii haitakuwa mara yetu ya kwanza, tutasafiri sana kwa reli ili kubaini hujuma zilizopo," alisema Dk Tzeba.
   
 17. kukumdogo

  kukumdogo JF-Expert Member

  #17
  Jul 31, 2012
  Joined: Feb 1, 2011
  Messages: 700
  Likes Received: 395
  Trophy Points: 80
  Ninawasiwasi mkubwa kwamba ndugu huyu mwenye maadili makubwa paka wengine wanamchukia, kunauwezekano mkubwa akafeli kisiasa kwa sababu ya sehem aliyowekwa. Hii sehem ni ngumu sana na watu wameota mizizi. Washauri wake ni wapotoshaji paka wanafanya mashirika kama reli na anga kutofanya vizuri. Budget inasemekana ni ndogo sana aliyopewa ambaya haina uwezo hata wa kununua ndege wala mabehewa ya treni. Je makeke yake yataendelea ?
   
 18. m

  mamajack JF-Expert Member

  #18
  Jul 31, 2012
  Joined: May 21, 2012
  Messages: 1,162
  Likes Received: 13
  Trophy Points: 135
  mwakyembe hawezi kuleta mabadiliko,kwanza utendaji wake siku hizi unanipa wasi sana,kila siku mara stand,mara tazara,mara kwenyedalala,najiuliza inamaana yeye haamini kuwa watu wanapata shida kwenye hizo sekta mpaka aende kushuhudia,haya toka kapanda hilo train nini kimefanyika mpaka sasa,hizo daladala ndo kabisamatatizo makubwa,mda wa kujaribi kujionea mwenyewe hauna tija,alipaswa aendelee na uwajibikaji wa vitendo sio maneno na kuuza sura kwenye tv.
   
 19. Codon

  Codon JF-Expert Member

  #19
  Jul 31, 2012
  Joined: Dec 16, 2011
  Messages: 629
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 35
  Awe makini sana,lasivyo kuna kila dalili hatofanikiwa!Binafsi naamini pale amewekwa kumalizwa kabisaaa!
   
 20. S

  Simbamwene JF-Expert Member

  #20
  Jul 31, 2012
  Joined: Jun 22, 2008
  Messages: 287
  Likes Received: 4
  Trophy Points: 35

  Mwakyembe anaweza kuleta mabadiliko, ikiwa ndege zinanunuliwa kwa dhamana ya serikali sio pesa taslimu, kitu muhimu ni kusafisha manejimenti ya ATCL na Tazara.
   
Loading...