Dk. Mwakyembe atoa misaada ya milioni 40/- jimboni

Dk. Mwakyembe atoa misaada ya milioni 40/- jimboni

kbm

JF-Expert Member
Joined
Oct 5, 2012
Posts
5,224
Reaction score
1,687
DR-Harrison-Mwakyembe.jpg

Waziri wa Uchukuzi, Dk. Harrison Mwakyembe

Waziri wa Uchukuzi, Dk. Harrison Mwakyembe, ametoa misaada yenye thamani ya zaidi ya Sh. milioni 40 jimboni mwake yakiwamo madawati 315 yatakayogawanywa kwa shule za msingi za jimbo la Kyela mkoani Mbeya.

Dk. Mwakyembe alikabidhi misaada hiyo jana mjini hapa ikiwa ni siku ya kwanza ya ziara yake ya siku tano jimboni mwakeyenye lengo la kuhamasisha maendeleo na kukamilisha ahadi alizoahidi wakati wa uchaguzi mkuu wa 2010.

Shule za msingi 14 zilizonufaika na msaada wa madawati 351 Maendeleo, Ikulu, Mbala, Ipyana, Ndola, Bujonde, Muungano, Lubele, Kasumulu, Malangali, Talatala, Kikuba, Gwato na Mahenge, kila shule itapewa madawati 24.

Dk. Mwakyembe pia alikabidi pikipiki 10 kwa vikundi vya maendeleo bodaboda ambavyo ni Nia Njema, Amani, Stendi, Tenende, Kyeluku, Transifoma, Mshikamano, Nyota njema, Kalumbulu na Ngyeke.

Alisema kikundi vya waendesha bodaboda kitakachoonyesha mafanikio zaidi kwa mradi wake kuwa na mtaji mkubwa kila baada ya miezi sita atakapofanya ziara jimboni mwake atakiongezea pikipiki nyingine mpya.

Dk. Mwakyembe ambaye ni Mbunge wa Kyela, pia alikabidhi vifaa mbalimbali katika Hospitali ya Wilaya ya Kyela ambavyo ni vitanda kwa ajili ya wanawake wajawazito na baiskeli maalum kwa ajili ya kuwabebea wagonjwa.

Pia alikabidhi mashine ya kisasa kwa kikundi cha vijana waosha magari kyela mjini na kuwataka vijana hao kujikusanya eneo mojamaalum ya kuoshea magari badala ya kufanya kazi hiyo maeneo mbalimbali katika mji huo hali inayosababisha uchafu wa mji.
Mbunge huyo alisema baada ya siku mbili kuanzia leo atakabidhi gari la kubebea wagonjwa (Ambulance) litakalotumika kwa ajili ya Hospitali ya wilaya Kyela.

Kwa upande wake Mwenyekiti wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) Wilaya ya Kyela, Dk. Hunter Mwakifuna, alisema misaada aliyoitoa Dk. Mwakyembe haina itikadi ya vyama badala yake itawanufaisha watu wote wakiwamo wa vyama vya upinzani.

Dk. Mwakifuna ambaye pia ni diwani wa kata ya Ipinda alisemavijana waendesha bodaboda wasikubali kushawishiwa na baadhi ya viongozi wa vyama vya siasa kufanya maandamano yasiyokuwa na manufaa kwao badala yake wajikite kujishughulisha na shughuli za uzalishaji mali.

CHANZO:
NIPASHE
 
Hiii haitamsaidia 2015 julubi mjrngoni, asitufanye watoto wanakyela alikua wapi siku zote,. Mwakyembe ha.tu.ku.ta.ki
 
Mshahara wa waziri unajulikana,sasa huyu bwana atatuambia hizo pesa nae kapewa na marafiki zake kama Lowassa? Siku hizi Lowassa ameanza kuwataja marafiki zake wanaomchangia kama alivyofanya kule Mwanza kwa kuwataja wakina Gachuma, Chegeni na wale waarabu wenye kiwanda cha kutengeneza mafuta; sasa na Mwakyembe nae awataje kama ndio hao marafiki waliomchangia ama sivyo tutajua kuwa nae ameishaanza mchezo wa kifisadi kuhujumu nchi!!!
 
Hiii haitamsaidia 2015 julubi mjrngoni, asitufanye watoto wanakyela alikua wapi siku zote,. Mwakyembe ha.tu.ku.ta.ki

Thnk big! Suala sio alikuwa wapi,Issue hapa ni kupongeza na sio kila MB anapofanya vitu anawaza 2015. Ni MB gani wa CDM amefanya hayo? Acha chuki binafsi wakati umefika watu kufanya vitu pale nafasi inapopatikana na wanaofaidika na mwananchi sio ww acha wivu wa kijinga.
 
Ninyi watu waajabu sn, mtu analeta maendeleo ww unahoji anatoa wapi. Km unatia shaka nenda mahakamani, pia ni changamoto kwa mb wako toka umemchagua kafanya nn. Acha kubeza wa wenzio
 
Nimeangalia TBC Mwakyembe anaongea na wapiga kura wake nimesikitika sana.

Kwanza wananchi wana ufahamu mdogo waziri anaongea kingine ila wao waliondoka pale na impression kwamba Mwakyembe amewaambia kuna mafuta yamegunduliwa ziwani na wao watanufaika.

Cha pili ahadi za Mwakyembe kuhakikishia kwamba wao watu wa kyela watanufaika ina undermine efforts za serikali kule kusini ilibidi awaambie point blank kwamba rasilimali za nchi ni za nchi pamoja kwamba watanufaika ila sio peke yao.
 
Mwakyembe ni waziri lakini pia anjua namna ya kutumikia wananchi wa jimboni kwake.
 
Ninyi watu waajabu sn, mtu analeta maendeleo ww unahoji anatoa wapi. Km unatia shaka nenda mahakamani, pia ni changamoto kwa mb wako toka umemchagua kafanya nn. Acha kubeza wa wenzio

Ukifumbia macho kwamba pesa ametoa wapi, unaendeleza mfumo wa ufisadi. Bado tunakumbuka kashfa nyingi za ufisadi na tunaona muendelezo wa jinsi mafisadi wanavyochangia makanisa na misikiti, ili mradi tu wapewe kura. Tuepuke sana viongozi kama hao. maendeleo katika jimbo huletwa na serikali kupitia sera na mipango yake, na kamwe si kazi ya wanasiasa, hususani wabunge.
 
Tulimwambia si tunataka bodaboda, kama we hujui mahitaji ya wanakyela na haupo kyela kaa kimya acha kimbelembele kwani we ni sekretari wake,. Kyela hawamtaki mwakyembe hutaki jiue
Thnk big! Suala sio alikuwa wapi,Issue hapa ni kupongeza na sio kila MB anapofanya vitu anawaza 2015. Ni MB gani wa CDM amefanya hayo? Acha chuki binafsi wakati umefika watu kufanya vitu pale nafasi inapopatikana na wanaofaidika na mwananchi sio ww acha wivu wa kijinga.
 
Ngoja wale vyake vya mwisho kyela hawamtaki fisadi hyu anaejificha nyuma ya pazia
Ninyi watu waajabu sn, mtu analeta maendeleo ww unahoji anatoa wapi. Km unatia shaka nenda mahakamani, pia ni changamoto kwa mb wako toka umemchagua kafanya nn. Acha kubeza wa wenzio
 
Walikua wanamzuga tu mkuu hawamtaki kabisa nyie hamuwajui wanyakyusa wa kyela nini wanaufahamu mkubwa sana
Nimeangalia TBC Mwakyembe anaongea na wapiga kura wake nimesikitika sana.

Kwanza wananchi wana ufahamu mdogo waziri anaongea kingine ila wao waliondoka pale na impression kwamba Mwakyembe amewaambia kuna mafuta yamegunduliwa ziwani na wao watanufaika.

Cha pili ahadi za Mwakyembe kuhakikishia kwamba wao watu wa kyela watanufaika ina undermine efforts za serikali kule kusini ilibidi awaambie point blank kwamba rasilimali za nchi ni za nchi pamoja kwamba watanufaika ila sio peke yao.
 
Hiii haitamsaidia 2015 julubi mjrngoni, asitufanye watoto wanakyela alikua wapi siku zote,. Mwakyembe ha.tu.ku.ta.ki

Alisema , misaada hiyo haina uhusiano wowote na ccm , je hapo alimaanisha nini ? Cdm inamtisha kinoma .
 
Thnk big! Suala sio alikuwa wapi,Issue hapa ni kupongeza na sio kila MB anapofanya vitu anawaza 2015. Ni MB gani wa CDM amefanya hayo? Acha chuki binafsi wakati umefika watu kufanya vitu pale nafasi inapopatikana na wanaofaidika na mwananchi sio ww acha wivu wa kijinga.

wala kilichomsukuma siyo upendo kwa wanakyela , bali ameogopa kitisho kikubwa cha chadema inayoenea kama moto nyikani ! Vijiji vyote ccm kwisha , wachache waliobaki wanamshawishi ahamie cdm maana anaweza kujikuta amebaki peke yake , mkuu niko kyela hivi sasa , cdm usipime !
 
Kama chadema hamwakubali hata matendo ya maendeleo madogo yanayofanywa na viongoz wa ccm.mtakimbiza wapiga kura 2015.hata mambo mazuri ni kupinga? Hata viongoz wazur ni kupinga tu? Kwa magreat thinker huo nao ni udhaifu tena mkubwa sana
 
katoa msaada wenye dhamani ya ml 40 leo atatoa ambulence! Ambulence nijuavyo haipungui ml 70 je hizi pesa kazipata wapo?
 
Attachments

  • pesa.jpg
    pesa.jpg
    25.7 KB · Views: 61
Msaada lazima useme pesa umepata wapi? Hasa ukizingatia yeye ni waziri...
MAMBO YA MAENDELEO KILA MTU ANATAKA.
 
Ule uhamasishaji wa maendeleo binafsi ya wananchi kutoka kwa mbunge wao hapa kyela hakuna kabisa , afya ni janga kubwa sana , hivi sasa kipindupindu kimetapakaa hadi aibu ! More than a hundred wameugua na kadhaa wamekufa , serikali imekataza mikusanyiko hata ya misiba kama njia ya kudhibiti maambukizo zaidi , lakini cha kushangaza mkusanyiko wake uliruhusiwa , je ni wangapi wamepata kipindupindu kwenye mkusanyiko huo ?
 
Bangoo .amepata wap hela kiongoz tena wazir mkubwa!na yupo chama tawala ? Tatizo lako kubwa ni huna elimu ya siasa wala kujitambua kisiasa chamsing jiulize swali? Nin maana ya mshahara?
 
Last edited by a moderator:
Back
Top Bottom