Mbunge wa Kyela (CCM), Dk. Harrison Mwakyembe, amejibu mapigo ya Mbunge wa Mbeya Mjini (Chadema), Joseph Mbilinyi maarufu Mr. II, kwamba hana ubavu wa kumngoa katika uchaguzi mkuu utakaofanyika 2015 katika jimbo hilo.
Dk. Mwakyembe amesema hayo ikiwa ni siku tano baada ya viongozi wa Chama Cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema) kufanya mkutano katika kijiji cha Njisi Boda Kasumulu ikiwa ni mwendelezo wa operesheni ya chama hicho kuzungumza na wananchi katika wilaya zote za mkoa wa Mbeya.
Katika mkutano huo Mbunge wa Mbeya Mjini, Mbilinyi, alisema atahakikisha anamungoa Dk. Mwakyembe katika uchaguzi mkuu wa 2015 kwa sababu ameshindwa kuyapatia ufumbuzi matatizo ya wakulima wa kokoa katika suala la bei kutokana na kuwa na maslahi na makampuni yanayonunua zao hilo.
Akijibu hoja hiyo, Dk. Mwakyembe alisema Mbilinyi hana ubavu wa kumngoa mwaka 2015 hata kama atavaa hereni masikio yote mawili kwa sababu wananchi wa jimbo la Kyela wanafahamu mambo ya maendeleo aliyowaletea katika kipindi cha miaka mitano ambacho amekuwa mbunge wa jimbo hilo.
Sugu (Mbunge wa Mbeya Mjini) hawezi kuningoa ubunge Kyela hata avae heleni masikio yote mawili, kwa sababu wananchi waishio Wilaya ya Kyela wanajua kupambanua, kuchana mistari na kuchochea maendeleo yao, alisema Dk. Mwakyembe.
Dk. Mwakyembe ambaye pia ni Naibu Waziri wa Ujenzi, alimshauri Mbunge wa Mbeya Mjini kwamba kwa kuwa bado ni mwanasiasa mchanga hivyo aelekeze nguvu zake katika kuwatumikia wananchi wa jimbo lake analoliongoza na siyo kukimbilia katika majimbo ya watu wengine kueneza propaganda ambazo haziwezi kumjenga kisiasa.
Dk. Mwakyembe alisema Mbilinyi kama mwanasiasa mchanga anayechipukia anapaswa kutambua kuwa hawezi akapata umaarufu kisiasa utakaomfanya aendelee kuaminiwa na wananchi wa Mbeya mjini kwa kwenda kwenye majimbo mengine.
CHANZO: NIPASHE JUMAPILI
ulishawahi kumuona akiivaa heleni?Kumbe Sugu ana vaa heleni sikioni! Mmmmmh hii ni aibu kwa watu wa mbeya mjini! Mbunge ana vaa heleni!
Huyo Mbiliyi sio mwanasiasa kwanza ni mwehumwehu tu hana lolote yeye akusanye hizo pesa za pension akipata aendelee na mziki wake.
haupo sahihi inamaana tumeshamsahau mwakyembe mda huu,amakweli mfali mbuzi binadamu atakuudhi tu
Malafyale ni mmoja ya watu waliompiga sana vita Mwakalinga aka Mtanzania wa JF kabla ya uchaguzi. Pamoja na kuwaeleza maelezo ya uhakika, ila wao bado walilala mstari mmoja kumtetea Mwakyembe. Wengi walimchagua Mwakyembe kwa sababu kadhaa:
1. Kuwakomoa Mafisadi ambao ilisemekana walikuwa wakitaka kumuondoa na kummaliza kisiasa.
2. Kumkomoa Mwakipesile ambaye ilisemekana kuwa alikuwa akimfanyia fitina Mbunge....
3. Kwa sababu wabunge wengi zamani walikuwa kwa miaka 10 , sasa Mwakyembe na kusoma ile ripoti kwa nini wamuondoe?
4. Wengi waliahidiwa vitu kibao na kuna Kibabu kiliweka sahihi hadi makaratasi kuwa kitapata gari ila sasa imekula kwake na kazi wamekifukuza kiaina. Ushahidi wote ulichomwa moto na hakubaki hata na copy............. Mnyakyusa Mjinga kumbe!!!!!
Sasa ona wanavyosema hawa vijana wake wa Tusk Force wa Jamiiforums kwa sasa:
Hebu soma walioshangilia ushindi wa Mwakyembe mwaka jana na leo wanasema nini? Nyambala bado upo? Bado wachekacheka kama mwaka jana? Hahahaaaaa 🙂
https://www.jamiiforums.com/tanzania-2010-2015/68676-kyela-elections-2.html
Hakika Mwakyembe hafai tena kuwakilisha wana-Kyela.
Huyu alitumia mamilioni ya kodi yetu kwenye kamati yake ya richmond, akaja na maazimio lukuki, lakini yote serikali ikayapuuza na kuyatupilia mbali. Serikali hiyohiyo iliyoponda kazi ya kamati yake ikamhonga uanibu waziri naye akakenua meno. Angekuwa mkweli ndani ya nafsi yake angekataa uteuzi ule uanomfanya awe sehemu ya hii irresponsible govt.
Fisadi sawa na anaowatuhumu ufisadi.
Mvaa heleni Sugu anataka kupambana na Mwakyembe(Phd) hopeless kabisa!
What is hereni......??? Kama ingekuwa ni issue basi wangemfanyia kama wale wa CUF waliowapa VIMADA pass za kusafiria............. Au wangemtimua kama Amina Chifupa alivyotinga na mavazi ya kiainaKumbe Sugu ana vaa heleni sikioni! Mmmmmh hii ni aibu kwa watu wa mbeya mjini! Mbunge ana vaa heleni!
Usionge ki2 usicho kijua, mbeya tumefanya right choice. Tunamwamin sugu,
Huyo mwakyembe wenu aache kutudharisha watu wa mbeya "kwani mwakyembe ni nani katika mbeya?"
hata elimu yake imeshindwa kumfanya aonge maneno ya Busara, ashindwe tena
hawezi kabisa kutufananisha na watu wa kyela. Mbeya kuna demokrasia.
Mwakyembe usilopoke tulia jibu kwa makini, busara na kwa kisomi usiwe kama watu walio ishia chekechea.
Kwa hiyo kwako wewe wamasai wa kiume wootee ni "ELTON JOHN".............????Mimi nikishamuona mwanaume mwenzangu anavaa hereni sikioni basi huwa namfananisha na Elton John yule mwanamuziki wa UK
Heh! Kumbe Watu wana Majimbo yao! Sijui nani amewauzia mpaka kuyaita ya kwao! Au wameshagawana, na sie wengine tuonataka kuwa viongozi itabidi tutengeneze majimbo yetu!Dk. Mwakyembe ambaye pia ni Naibu Waziri wa Ujenzi, alimshauri Mbunge wa Mbeya Mjini kwamba kwa kuwa bado ni mwanasiasa mchanga hivyo aelekeze nguvu zake katika kuwatumikia wananchi wa jimbo lake analoliongoza na siyo kukimbilia katika majimbo ya watu wengine kueneza propaganda ambazo haziwezi kumjenga kisiasa.
CHANZO: NIPASHE JUMAPILI